ibada

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}

.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}
Nilkuwa sijaona ibada katika hekalu kama hili,sisi watoto tulikuwa tunazuiwa kabisa,kwetu sisi ilikuwa hekalu kuu,au moja ya mahekalu madogo,lakini hili,ambalo lilikuwa limechongwa chini kabisa juu ya majengo yaliyojengwa na binadamu,nilikuwa najiuliza ilikuwa ni nini walichokuwa wanafanya hapa. Kwa uangalufu,nikavuta joho langu kuzunguka kiuno changu ili nisijikwae,nikavuta mbele na kuchungulia nyuma ya kona.
.
Hii ilikuwa inapendeza sana,nilifikiria. Mbele yangu katika mduara walikuwepo lama tisa wote wamevaa mavazi ya saffron,wote macho yao yalikuwa yameelekea katikati ya mduara,na katikati katika jukwaa lililochongwa vizuri,kulikuwa na Kitu-Kitu ambacho sikuweza kukitambua vizuri. Ilkuwa kama vile kuna kitu,lakini pia ilikuwa kama vile hakuna kitu. Nilitetemeka ,na nywele zangu zilizonyolewa kwenye kichwa kichwa changu zilisimama wima kama walinzi katika paredi,kwa sababu vidole baridi vya woga vilijinyoosha na kunigusa,kunistua kiasi kwamba nilikuwa tayari kutoroka. Nilikuwa nafikiria kwamba kilichokuwa pale kilikuwa ni kiumbe kutoka kwenye ulimwengu wa kivuli,kiumbe ambacho kilikuwa hakipo hasa katika hii,dunia yetu,na pia kilikuwa hakipo sana katika dunia ile nyingine.

Ilikuwa kama vile ni duara ya kitu fulani,au duara lakini siyo ya kitu chochote;ilikuwa karibu haina umbo,na hata hivyo umbo lolote lililokuwepo lilikuwa katika hali kama ya mawimbi! Nilitamani kama ningeweza kwenda karibu zaidi ,na kuchungulia juu ya kichwa cha mmoja wa lama waliokuwa wamekaa pale, lakini hivyo ningekamatwa. Kwa hiyo nikakaa,na kuisugua mikono yangu katika macho yangu nikijaribu kuondoa usingizi,nikijaribu kuyafanya yaamke zaidi,nikijaribu kuyafanya yaone vizuri zaidi katika huu ukungu na giza.Baada ya kutosheka kwamba nilikuwa nimefanye yote niliyoweza kuhusu macho yangu,nilitambaa tena mbele kwa mikono na magoti,na kutazama,nikibadili nafasi yangu kidogo ili nitazame vizuri zaidi kati ya mabega ya lama wawili.

Nilitazama-na mara nikaelewa ghafla-kwamba hili lilikuwa ni jiwe kubwa la crystal,kamilifu,halina dosari. Lilikaa pale lilipopachikwa na lama walikuwa wanalitazama karibu sawa na kuliabudu. Walikuwa wanalitazama kwa makini ,na pia siyo kwa makini ili kutumia macho ya mwili,badala yake ilikuwa kama vile wanatumia jicho la tatu. Nikafikiria,kama ni hivyo,mimi pia ni clairvoyant. Kwa hiyo nikalitazama siyo tena na macho yangu ya mwili isipokuwa nikaruhusu kipaji changu cha clairvoyance kujitokeza,na katika crystal nikaona rangi, mawimbi ya rangi yanazunguka na moshi unafuka. Ajabu kabisa,kwa kutisha,nikaona kama vile nanguka,naanguka kutoka kilele cha juu sana;naanguka kutoka juu ya dunia mpaka katika shimo kubwa lisilokuwa na mwisho. Lakini,hapana,lilikuwa siyo shimo;badala yake,dunia ya aina fulani ilikuwa inajitokeza mbele yangu,dunia ambapo kulikuwa na rangi tofauti,viwango tofauti. Niliona kama aliyekaa kwenye muinuko watu ambao walikuwa wanatembeatembea hawana furaha,wamejaa huzuni;wengine walikuwa katika maumivu makubwa.Walikuwa ni roho zilizopotea,roho zisizo na mwongozo,roho zilizokuwa zinafikiria mbinu ya kutokana na masaibu yao.

Nilipokuwa pale nimeduwaa,kama vile nipo katika dunia iliyokuwa inaangazwa na jua,pambio za wale lama ziliendelea. Kila baada ya muda fulani mkono ulijitokeza na kupiga kengele ya shaba. Na hivyo wakaendela na pambio zao,muziki wao unapanda na kushuka siyo kwa staccato kama ilivyo katika mitindo mingine ya muziki duniani,lakini hapa sauti ziliingiliana ,moja inaingia katika nyingine,na kushikamana na kugonga ukuta na kuunda sauti nyingine mpya.

Kiongozi wa wale lama alipiga makofi na mikono yake,yule aliyekuwa karibu naye akapiga kengele,na wa tatu katika kundi akainua sauti yake huku akiimba pambio za ile ibada,'' Oh sikilezeni Sauti za Roho zetu.'' Na hivyo wakaendelea kutoka mmoja hadi mwingine wanarudia hizi beti za kale,kwanza mmoja kwa wakati mmoja,halafu wote kwa pamoja,sauti yao inapanda na kushuka,inapanda na kushuka,na kuniinua mimi kutoka katika wakati,kutoka ndani mwangu.

Halafu ikaja seti nzima ya sala kutoka kwa hili kundi:

Oh! Sikilizeni Sauti za Roho zetu,
Wote mnaokaa jangwani,bila ulinzi,
Sikilizeni Sauti za Roho zetu,
Ili tuwalinde wasiokuwa na ulinzi,
Kijiti cha kwanza cha udi kinapowashwa na moshi
unapanda juu
Roho yako na Imani yako vipande pia,
Hivyo mtaweza kulindwa.


Oh! Sikilizenu sauti ya Roho zetu,
Wote ambao mnajikunyata kwa woga usiku.
Sikilizenu Sauti za Roho zetu,
Kwa vile tutakuwa kama karabai ambayo inaangaza
katika giza
Ili tuweze kuwaongoza wasafiri walipotea.
Kijiti cha pili cha udi kinapowashwa na kuangaza Maisha
Roho yako iuone Mwangaza tunaoangaza ili uongozwe.


Oh! Sikilizenu Sauti za Roho zetu,
Wote ambao mmekwama katika Ghuba ya Ujinga.
Sikilizeni Sauti za Roho zetu,
Msaada wetu utakuwa kama daraja kuvuka ufa,
Kuwasaidia zaidi katika Njia.
Kijiti cha tatu cha udi kinapowashwa na moshi unafuka,
Roho yako ipige hatua kishujaa katika Mwangaza.
.
Oh! Sikilizenu Sauti za Roho zetu,
Wote ninyi ambao mnazimia kwa uchovu wa Maisha.
Sikilizenu Sauti za Roho zetu,
Kwa vile tunawaletea Mapumziko,ili baada ya kupumzika Roho yenu
ivinjari tena upya.
Kijiti cha nne cha udi kinapowashwa na moshi unazunguka kivivu,
Tunaleta Mapumziko,ili kwa kupumzika,mnaweza kuinuka upya.

Oh! Sikilizenu Sauti za Roho zetu,
Wote ninyi mnaopuuzia Maneno Matakatifu.
Sikilizenu Sauti za Roho zetu.
Tunawaletea Amani! Ili mfikirie Kweli za Milele.
Kijiti cha tano cha udi kinapowashwa na kuleta harufu njema kwa Maisha,
Fungueni akili zenu ili Mfahamu.

Sauti ya pambio ikafifia na kufa. Lama mmoja akainua kengele yake na kuipiga polepole;wengine wakachukua kengele zao na kuzipiga. Kwanza wote kila mmoja akapiga peke yake,halafu,kufuatana na mpango waliopanga ,wote wakapiga kwa pamoja,na kufanya sauti maalum ,iliyovuma,na kushuka na kupanda. Wale lama waliendelea na kuimba pambio yao kwa sauti nzito,wakirudia tena''Oh! Sikilizenu Sauti za Roho zetu,'' na kupiga kengele zao,na kuendelea na pambio. Athari yake ilikuwa kubwa sana kwa anayesikiliza .

Niliendelea kutazama watu walionizunguka-au walikuwa wamenizunguka?Je,nilikuwa katika dunia nyingine? Au nilikuwa natazama katika crystal. Hisia yangu kali ilikuwa kwamba nilikuwa katika dunia nyingine ambapo majani yalikuwa kijani zaidi na anga ilikuwa bluu zaidi,ambapo kila kitu kilikuwa kinaonekana vizuri zaidi,kinatofautika vizuri zaidi na kilicho pembeni yake. Kulikuwa kuna fungu la majani chini ya miguu yangu,na ajabu kabisa nilikuwa naweza kuhisi umande na vidole vyangu vya miguuni! Niliweza kuhisi umande uliokuwa unaingia katika joho langu pale ambapo magoti yangu yalipogusa ardhi. Mikoni yangu pia,nilipoishika kwa upole ilihisi kuwa ni majani na pengine hapa na pale jiwe moja au mawili. Nilitazama kila pahali kwa shauku kubwa Kulikuwa na majabali makubwa mbele yangu,ya jiwe la aina ya kijani,hapa na pale lilikuwa na rangi nyeupe. Majabali mengine yalikuwa rangi tofauti;moja ambalo lilinivutia sana lilikuwa na rangi nyekundu,nyekundu pamoja na rangi nyeupe kama maziwa imechanganyika. Lakini nililoona sana ni jinsi ambvyo kila kitu kilivyokuwa kinaonekana wazi wazi,jinsi ambavyo kila kitu kilivyokuwa kawaida kuliko kawaida,na rangi kali zaidi,na maumbo yanaonekana vizuri zaidi.

Kulikuwa kuna upepo unapuliza kidogo,niliweza kuuhisi juu ya shavu langu la kushoto. Ilikuwa ajabu kidogo kwa sababu upepo huo ulikuwa na harufu kama ya udi na uvumba.Mbele kidogo niliona kitu kilichoonekana kama nyuki. Alikuwa anaruka,na akatua na kuingia katika tarumbeta ya ua dogo lililokuwa linaota katika majani. Yote haya niliyaona bila kuhisi wakati unapita,halafu nikastuka,nikaingia wasiwasi,kwa sababu kulikuwa na kundi kubwa la watu linakuja kuelekea kwangu. Niliwatazama na nilikuwa sina uwezo wa kuondoka;walikuwa wanaelekea kwangu na nilikuwa takriban katika njia yao. Hapa nilipowatazama nilihisi kwamba kuna tatizo fulani. Watu hawa wengine walikuwa ni wazee walioegema kwenye fimbo na waliochechemea mbele bila viatu,wamevaa matambara. Wengine dhahiri walikuwa watu matajiri,lakini bila kuwa na hali ya faraja ambayo utajiri kwa kawaida unaleta,kwa vile jambo moja lilionekana dhahiri katika hawa wanaume na wanawake-walikuwa na huzuni,wanaogopa,kitu kdogo tu kiliwafanya wastuke na kujishikilia vifua. Walitazama huko na huko kwa wasiwasi,na hakuna aliyeonekana kuelewa kwamba jirani yake yupo;walijiona kama vile wako peke yao,wamesahauliwa,wenye ukiwai,na wametelekezwa katika ulimwengu wa kigeni.


Waliendelea kuja,kila mmoja anajijua hali yake tu mwenyewe,lakini walikuja kama kundi,bila yeyote kumgusa mwingine,bila mmoja kujua kwamba mwingine yupo. Walikuja wakivutwa na sauti ambazo mmi pia niliweza kuzisikia''Oh! Sikilizeni Sauti za Roho zetu wote ninyi mnaotembea bila uongozi'' Pambio na sauti ziliendelea na watu wakaja pia,na walipofika sehemu fulani-sikuweza kuona vizuri jambo gani linatokea-kila uso ulionekana una furaha ambayo kama vile siyo ya dunia hii,kila mtu akaonekana kusimama wima zaidi kama vile alikuwa amepata ahadi na kwa hiyo alikuwa anajisikia vizuri kwa hiyo. Waliendelea na kupita upeo wangu wa macho. Ghafla,nilisikia kama navutwa kama vile mtu alikuwa ananivuta na kamba,kama vile mimi nilikuwa kishada na mtu alikuwa ananivuta katika kimbunga kilichokuwa kinajaribu kuzuia.

Nilipokuwa natazama ile ardhi ya jajabu nilikuwa na hisia kwamba usiku ulikuwa unaingia,kwa vile anga iliingia giza na rangi zilikuwa hazionekani vizuri. Vitu vilikuwa vinaonekana kama vanakuwa vidogo. Vinakuwa vidogo?Vingewezaje kuwa vidogo? Lakini bila shaka vilianza kuwa vidogo,na siyo tu vilianza kuwa vidogo lakini pia ukungu kama mawingu ulianza kuufunika uso wa ile dunia,na nilipokuwa natazama kwa woga mkubwa jinsi vitu vilivyokuwa vinazidi kuwa vidogo ukungu ukabadilika kuwa mawingu meusi yenye radi.

Dunia ilikuwa inazidi kuwa ndogo,na mimi nilikuwa napanda juu zaidi na zaidi. Na nilipotazama chini niliweza kuiona inazunguka chini ya miguu yangu,halafu nikaamua haiwezi kuwa inazunguka chini ya miguu yangu kwa sababu nilikuwa katika hekalu kwenye magoti na mikono yangu. Au nilikuwa wapi?Nilikuwa nimechanganyikiwa ,halafu tena,kwa mara nyingine tena nikapata mstuko,mstuko mkbwa,mstuko ambao karibu uutoe ubongo wangu kutoka kwenye kichwa changu. .

Nilikuwa naona kizinguzungu,na nikainua mikono yangu kuyasugua macho yangu,na nikaona mbele yangu kwamba crystal ilikuwa ni crystl tu tena,siyo tena dunia,isipokuwa crystal tu imekaa haina lolote au uhai ,bila mwangaza wowote ndani. Ilikaa pale katika stand yake kama vile ilikuwa ni jiwe au sanamu ya kuchonga,au kitu chochote,siyo kama chombo kizuri cha kuona mambo ya ajabu. Polepole lama mmoja akasimama na akatoa kitambaa kilichokuwa chini,kilionekana kama vile kitambaa cheusi cha hariri. Kwa heshima akakikunjua hicho kitambaa na kuifunika crystal na hicho kitambaa. Akasujudu mara tatu upande wa crystal,na akageuka kuelekea alipokuwa amekaa. Alipofanya hivyo akashangaa kuniona mimi. Kwa muda wa nukta chache kila mtu aliduwaa,wakati ulikuwa umepoozwa. Niliusikia tu moyo wangu unapiga kwa nguvu mara moja''thump'' halafu basi. Kulikuwa na hisia kwamba maumbile yote, wakati wote,ulikuwa unasikiliza kwa shauku kubwa kujua jambo gani litafuatia.
 
eeh!
mzee nikipoteza taim nasoma hili gazeti si nitafukuzwa kazi?:D
 
Ni kwa sababu hatutaki kupoteza time ndio tunasoma haya mambo. Lakini hii imeandikwa ili isomwe na watu ambao hawana kazi.
 
Inamvuto fulani wa kuijua hii story ila ni mpaka mda wa kuisoma upatikane.
 
Back
Top Bottom