Ibada ya kumuaga Mhe Regia Mtema kufanyika kesho

Josephine

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
786
812
Kutakuwa na Ibada ya kumuombea na kumuaga marehemu Mhe Regia Mtema katika kanisa la RC Segerea saa tisa mchana siku ya kesho J3.

J4 kuanzia saa nne asubuhi mwili wa marehemu utakuwa Katika Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya salamu za mwisho kutoka kwa wananchi wote na baada ya hapo safari ya kuelekea Ifakara.

Karibuni nyote.
 
Kanisa la segerea liko barabara ya Tabata- changombe,viwanja vya karimje viko Posta katikati ya jiji.
 
maskini ningependa kushiriki na Watanzania wezangu kwenye ibada na mazishi ya da regia lkn sitoweza kutokana kuwa mbali ila nitashiriki nanyi kiroho kwenye maombi MUNGU AWAJALIE MMALIZE SHUGHULI ZOTE ZA MAZISHI KWA KHERI NA MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEPA PEPONI. Amen
 
Japo kimwili hatuko naye, naamini Kiroho tuko naye milele. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina la bwana libarikiwe, Amen! Ni vigumu kuamini kwamba ametuacha, lakini pia lazima tukubali kuwa kazi ya mungu haina makosa.
 
Kanisa la segerea liko barabara ya Tabata- changombe
Barabara inayotoka Tabata kwenda Changombe ziko nyingi, hivi mabarabara yetu hayana majina?

Na makanisa ya RC pia si moja Segerea. Kibongo bongo hatuyapi majengo majina wala anwani, kila kitu kinaenda kienyeji enyeji tu.
 
Kutakuwa na Ibada ya kumuombea na kumuaga marehemu Mhe Regia Mtema katika kanisa la RC Segerea saa tisa mchana siku ya kesho J3.

J4 kuanzia saa nne asubuhi mwili wa marehemu utakuwa Katika Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya salamu za mwisho kutoka kwa wananchi wote na baada ya hapo safari ya kuelekea Ifakara.

Karibuni nyote.

Source please
 
Japo kimwili hatuko naye, naamini Kiroho tuko naye milele. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina la bwana libarikiwe, Amen! Ni vigumu kuamini kwamba ametuacha, lakini pia lazima tukubali kuwa kazi ya mungu haina makosa.

Atafanya atakalo atafanya awezalo kwani dunia ni yake
 
Asante kutujuza. Kwa sie tulio mbali, tunaungana na nyie kumuombea dada yetu, mpendwa wetu marehemu Regia Mtema apumzike kwa amani.
 
Barabara inayotoka Tabata kwenda Changombe ziko nyingi, hivi mabarabara yetu hayana majina?

Na makanisa ya RC pia si moja Segerea. Kibongo bongo hatuyapi majengo majina wala anwani, kila kitu kinaenda kienyeji enyeji tu.
Kama ni kanisa la RC segerea basi njia rahisi ni kupanda gari mpaka segerea mwisho, ukishuka kutoka stendi uwe kama unaenda magereza nenda hatua kama kumi hivi utaona barabara ya vumbi inaingia kulia ifuate barabara hiyo ukiuliza kanisa la RC utoneshwa.
 
Back
Top Bottom