Ianzishwe vita- Rage.na mimi namuunga mkono

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Rage aapa kutokanyaga Kinshasa
7303.jpg
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
MICHAEL MOMBURI, KINSHASA MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, ameapa kwamba timu hiyo haitakanyaga Kinshasa milele na wakipangiwa watajitoa kwani si sehemu salama na amesema watashtaki kwa Serikali ya Tanzania. Simba ilifungwa mabao 2-0 juzi Jumapili katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DCMP ya hapa na kuondoshwa katika mchezo huo uliogubikwa na fujo za kila aina ndani na nje ya uwanja. Baada ya mchezo huo, maelfu ya mashabiki walivamia uwanja kwa lengo la kuidhihaki Simba jambo ambalo lilifanya askari wa usalama kuwatuliza wachezaji na viongozi kwenye benchi la ufundi na kuwazunguka kuwaepusha na fujo hizo zilizodumu mpaka usiku. Dakika chache baadaye wachezaji hao walisindikizwa tena hadi vyumba vya kubadilishia nguo na kutulizwa kwa zaidi ya saa moja hadi hali ilipotulia, lakini hata mitaani askari walitumia nguvu za ziada na vitisho vya hapa na pale kufungua njia ingawa bado walikuwa wabishi. Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema; "Wametufanyia mambo mabaya sana, hizi ni hujuma ambazo hazivumiliki, ndiyo maana nasema Simba haitakanyaga milele Kinshasa. "Hatutakuja kucheza mechi yoyote hapa kwa vurugu hizi, tutagawa pointi za bure. Labda Serikali itoe tamko na tupewe ulinzi maalumu au tucheze nje ya hapa. Na tutakwenda kushtaki Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu unyama tuliofanyiwa hapa Kinshasa. "Tungeshinda tusingetoka hapa uwanjani, wangetuua hawa," alisisitiza kiongozi huyo, ambaye amependekeza ianzishwe vita dhidi ya raia wote wa DR Congo wanaoishi nchini kinyume cha sheria. Simba iliwasili jijini Dar es Salaam jana Jumatatu, saa 12.45 jioni kwa ndege ya KQ.
NOte: vita anayomaanisha hapa ni kuwakamata wakongo wanaoishi kinyume na sheria.wazamiaji
 
Naunga mkono hoja...............
Watanzania tuna mambo ya ajabu sana ambayo inabdi yakemewe kwa nguvu zote. tuna mtindo wa kuwahusudu sana wageni wakati ukienda kwao wewe wanakudharau na kukuona kuwa wewe si lolote si chochote. kuanzia kwenye ajira hatupendi kuweka uzalendo mbele ,wakongo wamejazana humu nchini na sisis tunawahusudu na kuwapigia makofi kila siku na dada zetu wakiwa mstari wa mbele kutoka na hawa wapata wanja wanaojichubua...tusipopendana wenyewe na kulindana hatutafika mabali.(ukiondoa ushabiki wa mpira)
 
Kuna wanaotoka DR Congo kuja kwetu, eti ni ma expert wa kupamba maharusi...kana kwamba sisi hatuwezi kazi hiyo!!
 
huu kweli si usanii uleule, wa siku zote na wa aina ileile wa maha-RAGE ya "gamba party"??

maana maha-RAGE kwa visingizio........
 
Mwenzenu anatwatuliza munkari kiaina baada kuchezea kichapo kwa DCMP.Msanii huyo msimwamini sana anajua sana kuupepeta mdomo uwanjani zero.Muungwana ukifungwa unatia akili na mbinu zingine za kujipanga.VIPI RUFAA SAFARI HII HAINA MASHIKO?
 
Kama vp naye ajivue gamba2 tatizo rage maneno mengi alf hakuna ki2 apunguze usanii bwana! Aya akate rufaa tena!
 
tukianzisha vita na wakongo ikiisha tugeukie Wasomali pia! Hivi huyu Rage ataweza kweli Ubunge na Uenyekiti wa simba!??? Time for excuses is no more!!
 
Mimi najiluliza, hao washabiki ni wa DCMP au ni wale TP Mazembe wakitaka kulipa kisasi kwa fitna ya Simba?
Tufanye TP Mazembe ndiyo Simba, wale fans wao wangefanyaje?
 
Rage nae anachemsha sasa ,tuanzishe vita na DRC tutapigwa hawa jamaa wamezoea vita .Vita dhidi ya Uganda hadi leo imetugharimu halafu uanzishe vita na DRC.Vurugu katika soka hasa barani Africa ni kawaida unakumbuka ugomvi ya Misri na Tunisia
 
tukianzisha vita na wakongo ikiisha tugeukie Wasomali pia! Hivi huyu Rage ataweza kweli Ubunge na Uenyekiti wa simba!??? Time for excuses is no more!!
NOte: vita anayomaanisha hapa ni kuwakamata wakongo wanaoishi kinyume na sheria.wazamiaji
 
rage hasira hazifai, hivi sikuzote ukujua kama mpira wa kiafrika fitna muhimu, nawewe subiria wakija uku miaka ijayo mjipange tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom