I oppose paying DOWANS S.A; its not just illegal...

2.jpg



I believe the payment to Dowans will be one of the most audacious and contemptuous action by the government against its people. I for one opposes these payments not just because they are illegal but because they are inherently immoral. A nation such as ours coming out of so many financial scandals of the past few years we can not and must not reward corruption.

If CCM and its government decide (as it seems they would) to pay Dowans they will do so because they can not because they can not fight it. What our government has decided to do is surrender to the forces of corruption. They payments would embolden corrupt elements in Tanzania.

I for one denounce everyone and every person who in his clear mind taking into consideration all the facts of the Dowans deal would support paying this company billions of Tanzanian shillings while our people are still struggling to improve the quality of the mortal existence. I reject totally and absolutely any attempt to justify this corrupt deal solely based in the legality of the issue without considering the morality of such payments.

I call upon Chadema, it leaders and members and everyone of goodwill to take a stand against these payments. Let us draw a line once again between those who support this scheme of corruption and those who reject it. Let us be willing to take a stand and be ready to pay the price for that stand. For evil can not be rewarded nor excused.

I dedicate myself once again to oppose these elements for as long as I know how and as long as Providence allows me. But, I will not excuse, defend, explain or in any way or shape try to "understand" why we have to pay corrupt deals. We made a mistake in bringing in Dowans, we should not make the second one - of rewarding it. For once we pay Dowans under this "legality" circumstances we should be prepared to pay more and more in other corrupt deals for the same people who brought us Loliondo, Meremeta, EPA, CIS, Tangold, Richmond, and Dowans are still in power and as long as they know that Tanzanians are soft-hearted and weak in opposing corruption they will do it again and again. We can not let that happen indefinitely.

Chadema as the leading Opposition party in the country should not wait until the payments are made for them to come strong for once the payments are made Dowans Tanzania Limited and Dowans Holding SA will go into insolvency or liquidation. After the companies go into insolvency of some sort any investigation later will be unnecessary and illusion of the first kind. I for one will oppose any investigation after Dowans are paid up as they are already lined up to! We can not play this game of 'hide and seek' with corrupt elements in the country for we (the people) will come out losing!

For its not corrupt people we are dealing with but a very orchestrated organized crime in Tanzania which has infiltrated even the very core of our government and civil society.

Lets stand UNITED IN OPPOSITION TO DOWANS PAYMENTS. The payments are illegal and indeed stronger than that they are immoral.

I stand to be counted.

M. M. Mwanakijiji (BGM).

Meanwhile.. Wakati huo huo...

Monday, 17 January 2011

Gedius Rwiza (Mwananchi)

BAADHI ya wanafunzi katika Shule ya Msingi Misewe iliyopo manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, wamelazimika kufika shuleni na khanga au viroba kwa ajili ya kukalia, kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wakati wanafunzi hao wakikaa kwenye viroba na khanga hizo, wengine wamelazimika kufuatilia masomo wakiwa wamechuchumaa au kukaa kwenye vumbi.
Mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo aliliambia gazeti hili jana kuwa kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule umewataka wanafunzi wote wa kuanzia darasa la kwanza hadi la tano, kufika shuleni na viroba au khanga kwa ajili ya kukalia.

Mzazi huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema, anasikitishwa na kitendo cha walimu hao kuwalazimisha wanafunzi kwenda shuleni na khanga na kuwachapa wanaoshindwa kutekeleza agizo hilo. “Inasikitisha sana kuona wazazi tunaandamwa wakati kuna sera inaamuru kuwepo na ruzuku ya Sh 15,000 kwa kila mwanafunzi. Je fedha hizo zinafanya kazi gani,”alihoji mzazi mwingine.


Read Here: WANAFUNZI WAKALIA VIROBA DARASANI




sounds to me like you r callin up on CHADEMA leaders to take it to the streets/demonstrate,But from what i hear is that you reside in the US,why dont you take the next flight to your motherland to join the demo....dont get me wrong though...hoja zako huwa zina mashiko..leaders lead by example and for me u r some sort of a leader,...enjoy the snow..the sun is burning hot in here
 
Wildcard, don't be fooled by it.. JK akizungumza tu na kusema tuwalipe hakuna mwana CCM atakayeleta fyoko.. si umeona wote walivyojipanga mstari baada ya yeye kuimbisha "katiba mpya".. hadi wengine wakatufanya sisi mazuzu..

DOWANS hawatalipwa. Hili linafanana sana na lile la Vallambia na BOT/TPDF. Mbaya zaidi limekuwa politicized mno. Litaiua kabisa CCM.
 
Wildcard, don't be fooled by it.. JK akizungumza tu na kusema tuwalipe hakuna mwana CCM atakayeleta fyoko.. si umeona wote walivyojipanga mstari baada ya yeye kuimbisha "katiba mpya".. hadi wengine wakatufanya sisi mazuzu..

Mapambano yaendelee tu kama watalipwa kwa shinikizo la mkuu au vinginevyo, nikuwawekea tahadhari watu hawa tuwachukulie hatua hata kama ni hatua za wananchi wenye hasira kali zikafuata wakishalipwa. tu demonstrate ili iwe funzo kwa wengine. nguvu ya umma itumike hapa, hakuna jinsi. sheria mimi sijui, ninachokiona hapo ni unyang'anyi tu. kama jambazi anakuingilia na wewe unataarifa na mikakati yake unaiona kwanini usitafute silaha yako na kuikoki? maana naona hata vyombo vya usalama wa raia vinawalinda hawa majambazi.
 
Serikali iliyopo ni ya kidhalimu, Hata hiyo kampuni ya Dowans inahusishwa nao. Ni vigumu sana kutegemea mtu yeyote toka serikalini kupinga ukiwatoa Mh Sitta na Mh Mwakyembe ambao kwa sasa nahisi wako hatihati.
Uongozi wa juu akiwemo Rais wanataka malipo yafanyike.
Njia muafaka zingekuwa ni maandamano ambayo yangeongozwa na wafanya kazi,maana hao ndio walipakodi wakubwa.Kama Tucta wakiitisha maandamano ya wafanyakazi na wananchi kwa ujumla basi kungekuwa na ufanisi maana litakuwa jambo la kijamii zaidi kuliko Chadema wakiitisha maandamano litafanywa la kisiasa.
 
DOWANS hawatalipwa. Hili linafanana sana na lile la Vallambia na BOT/TPDF. Mbaya zaidi limekuwa politicized mno. Litaiua kabisa CCM.


Kuna namna moja tu ya Dowans kutokulipwa nalo itakuwa by an executive order ya Rais na hilo litamtengeneza JK kuwa ni shujaa. Hakuna lolote litakalotokea baada ya hapo. Lakini nje ya hapo lazima walipwe na my thinking hadi sasa ni kuwa walipwe kabla ya Kikao kijacho cha Bunge ili waharakishe insolvency. Jamaa wanasubiria hizo fedha ziingie kwenye akaunti na kutawanywa mara moja kuliko mnavyofikiria.

Hivi tukishawalipa halafu ikajulikna kuwa hayo makampuni hayakuwepo tutamshika nani shati?
 
4360527_orig.jpg


Shule ya Msingi Juhudi - Kigoma Vijijini, Tanzania

Picha za kinamama waliolala chini zilinisikitisha sana lakini hii inanipa hasira.

Kwani tunaandamana lini? Hip Hip Huraaaaay!!!!!!!!
Waandae mabomu ya nyuklia safari hii maana ya machozi hayatafaa kabisaa.
 
My take on Dowans goes like this: A guy brutally rapes your daughter and unfortunately she gets pregnant. The baby is born and a few years down the road the very same guy comes and demands "his child!" Indeed the child may legally be his but that child is a result of a very illegal act. How can you as a parent morally give away that child to the person who brutally raped you? I ask? What difference does this analogy has with DOWANS? The fact is that Tanzanians are a victim of "rape" by some conmen masquerading as businessmen- cum-politicians and as sovereign people we should not be hoodwinked or even coerced into paying the very people who raped us in the first place. We should speak in unison against this immoral blackmail couched in legal semantics! At one time one Minister suggested that Tanzanians were capable of eating grass. Indeed, there is no better time to eat the grass like over the DOWANS nonsense just in case the international community decides to side with the "Rapists" and I believe no rational donor will do that. Like the infamous Kihaya slogan goes: " TUBAGAMBILE STUPID!"
 
Kuna namna moja tu ya Dowans kutokulipwa nalo itakuwa by an executive order ya Rais na hilo litamtengeneza JK kuwa ni shujaa. Hakuna lolote litakalotokea baada ya hapo. Lakini nje ya hapo lazima walipwe na my thinking hadi sasa ni kuwa walipwe kabla ya Kikao kijacho cha Bunge ili waharakishe insolvency. Jamaa wanasubiria hizo fedha ziingie kwenye akaunti na kutawanywa mara moja kuliko mnavyofikiria.

Hivi tukishawalipa halafu ikajulikna kuwa hayo makampuni hayakuwepo tutamshika nani shati?

Na hivyo ndivyo atakavyofanya JK wetu. Huoni alivyolirukia usoni suala la KATIBA? Hili la DOWANS limeikalia vibaya CCM na serikali yake. Wakilipa, mwaka huu hadi 2015 mambo yatakuwa magumu sana kwao hata kwa kutumia nguvu yote ya dola.
 
Mzee Mwanakijiji, naomba niji qote mahali
wana jf wenzangu mnaoitakia mema nchi hii, hii issue ya malipo kwa Dowans ina pande mbili.
  1. Hoja ni ya kisheria, hapa tumefungwa kisawasawa, back, front, left and right, hakuna mahali pa kutokea, mkataba ule ni mkataba mbovu hata mwanafunzi wa mwaka wa sheria linakofundishwa omo la law of contract, ataling'amua. Kisheria Dowans wana haki asilimia 100% kulipwa. Licha ya kuwa ni kampuni feki, wamiliki feki, usajili feki na kila kitu feki, yale majenereta, ni majenereta kweli na yanafua umeme kweli, hivyo fidia ni kufidia hizo genereta, haijalishi ni za nani, lakini zipo ndio maana ICC wakatupilia mbali uhalali wa kampuni na kuzingatia tuu mkataba.
  2. Kisheria naamini wanasheria wa Tanesco na wale wa Mwanasheria Mkuu, sio vilaza ki vile, kupitisha mkataba ule kama ulivyokuwa, wamekuwa taken care vizuri ndio maana wakapitisha madudu yale.
  3. Naamini timu ya defence ya Tanesco kwenye shauri la ICC, sio butu kivile kwenda na hoja nyepesi nyepesi ili Tanesco washindwe, wamekuwa well taken care off ili mambo yaende.
  4. Watu wanantaja taja fisadi Rostam as as if ni yeye ndie atakayeyachukua hayo mabilioni ya fidia, mimi nasema no, sio Rostam, yeye Rostam ametumika tuu kama front, kama ilivyo kwa Kagoda, ni front tuu ya kuchotea pesa llakini wafaidika wakuu ni wengine, na amini nawaambieni, siku mkisikia who is behind Rostam, mtashindwa kuamini!. Kikulacho ki nguoni mwako.
  5. Sasa hao walio behind Rostam, ndio waliomtuma mwanasheria mkuu kukubali tulipe, na kumtuma Ngeleja kulitangazia taifa tutalipa, hata bili kulipitishia baraza la Mawaziri, maana kina Sitta, Mwakiembe, Magufuli etc wasingekubali upuuzi huo.
  6. Kwa vile kisheria limesimama, bodi ya Tanesco, haina njia bali kujipanga ili mahakama kuu ikisha thibitisha tuu faini ilipwe, Tanesco walipe papo hapo, tena kwa kukopa CRDB!.
  7. Lengo la Tanesco kulipa papo kwa papo ni kuepuka ongezeko la Shilingi Milioni 25, kila siku ya Mungu itakayopita, tangu siku Mahakama Kuu imeiamuru Tanesco kulipa. Hiyo inamaana deni linaongezeka kwa milioni 100 kila baada ya siku 4, na zikifika siku 40, ni bilioni moja nyingine.
  8. Ubishi wa kina Sitta na wote tunaopinga malipo hayo, hatuna hoja za kisheria bali za kisiasa, kina Sitta na Mwakiembe wanataka kuleta siasa kwenye sheria ambayo pia inawezekana.
  9. Tanzania tunaweza tukapinga kulipa hizo pesa na tukajitoa kwenye ICC, hata kama hao wawekezaji Wazungu, watakosa imani na nchi yetu na kususa kuwekeza, wafungashe na kwenda zao kwao, tuone hao Baric watachimba dhahabu gani Canada etc. Madini ni yetu, sio jukumu letu kuwabembeleza wawekezaji, kwa sababu wenye mali ni sisi, ni jukumu la wawekezaji kuja kutubembeleza sisi ndio tuwape madini yetu, waneemeke wao na kutuachia mashimo. Kwa Tanzania its the other way round, sis ndio wenye mali, ala tunawalamba miguu hawa jamaa wanaokuja kutukanyaga.
  10. Na mwisho, vunjilia mbali mikataba yote ya kimataifa isiyo na maslahi kwa taifa, wachina wapo tayari kuendesha kila kitu kwa mikataba yenye maslahi kwetu, na hata tukiwafukuzia mbali wazungu wote, watalii wa kichina pekee wanaweza kushibisha soko la utalii maradufu kuliko wazungu ambao fedha yote ya maana, huilipia huko huko, hapa hubakisha fedha ya kulipia shanga, vinyago, karanga na kuwalipa madada zetu kwa zile huduma!.

Tusitafute majibu ya kisiasa kwenye issues za kisheria, tukifuata sheria, lazima tulipe, no way out. Tukiamue tusifuate sheria ndio tufuate siasa kwa kuvunjilia mbali hiyo sheria, mbona Sudan wameigomea mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita na Kenya wako njiani kugoma!.
 
This issue ni mto Yordan ya Tanzania ambayo wana wa Israel walitakiwa kuuvuka kufikia nchi ya ahadi. Wakati huo (wanawa Israelwalipotakiwa kuvuka) ulikuwa umefurika mpaka kwenye kingo zake. So we have to choose makuhani waliobeba sanduku la agano wakanyage maji ili maji ya tindike raia tu vuke tukiwa salama. Amasivyo makuhani waamue kulidondosha sanduku la agano na wate tuchukuliwe na mafuriko mpaka dead sea where the river empties its waters.
Heri walio amua kuhesabiwa maana thawabu yao ni kubwa. Natamani kuwa miongoni and indeed Iam. Nitasimama kwa zamu yangu nahakika kama Mungu aishivyo watanzania lazima tutavuka salama. Tukifika ngambo lazima maadui wazame bahari ya Shamu. Ole wenye kugeuka nyuma wote mtakuwa nguzo ya chumvi. This is a decree written with my own hands I the princes in the kingdom of Zion in Jesus name. Mwenye sikio na asikie.
 
MMM asante kwa hili pia.

Tatizo letu watanzania wala sio hao Dowans, tatizo ni kilongola (kiongozi) hajui njia na hataki kuambiwa kwamba haijui na hataki kuijua.

Kukimbilia kwenye sheria hao Dowans wapo huko siku nyingi hata kabla hatujafikiria.

Linawezekana ni kwa vyama vikuu kama CDM na CUF kuwaunganisha watanzania kufanya maandamano ya amani kumwonyesha kiongozi mkuu wa nchi kwamba hata kama atawalipa Dowans mioyo yetu inauma na hatujafurahishwa nae.
Wakiamua kutupiga risasi tena na iwe hivyo, ni heri kufa wakati tunajaribu!
 
usibeze sauti ya wanyonge maana ndio wengi.

Kuilipa DOWANS ni faida kwetu ama hasara? Linki unayoitaka ipo wazi, una macho huoni. MAFISADI wetu wa hapa nchini ndio wameiingiza nchi kwenye mkataba na DOWANS.

Unaweza kua umeridhika sana na utendaji kazi wa MAFISADI mpaka hapa tulipofikia, lakini wengi tunaumia kuona walifanya na wamekua wakifanya kazi mbovu na sasa inabidi tulipie gharama za kufidia.
Mkuu naomba urejee post yangu sababu am sure haujanielewa..... Point yangu ni kwamba kujua kwamba RA au nani anausika pekee haisaidii inabidi tupate Link (proof) ambayo itamuhusisha ili kuwa na Case ya kuhujumu Uchumi.... hata kama akishikwa kaiba peanuts wananchi tukimbana tunaweza kumfilisi/kuwafilisi hawa mafisadi...

Kutokulipa pekee ni kwamba inakuwa hatujaondoa kansa ambayo bado inakula mwili.... IT ABOUT TIME WE TAKE THE WEEDS FROM THE ROOTS AND NOT ONLY CUTTING THE LEAVES.
 
I SALUTE YOU M.M... WE NEED STARTER AND I THINK DOWANS INATOSHA KABISA KUIFURUMUSHA HII SERIKALI DHALIMU MADARAKANI.. I BELIEVE IN PEOPLES POWER...SOMETIMES NAFIKIRIA NIKAJIPIGE KIBERITI MBELE YA IKULU AU MJENGONI KUWAAMSHA WATANZANIA NA KUTAKE ACTION.....SIJUI TUMELAANIWA???? YAANI HUU UJINGA UNAFANYIKA WAZI WAZI HALAFU TUKO KIMYA TU.. AU NI UOGA NDIO UNAOTUCOST WATANZANIA WA LEO..BUT MBONA ARUSHA WATU WALISIMAMA IMARA...DR SLAA (phD) ONGEA TUINGIE BARABARANI NCHI NZIMA KAMA TUNISIA.
 
how, you stand to be counted where? Where the heck are you, Waterloo, Iowa?
We are all fighting the same battle does not matter where you are..... I can honestly say Mwanakijiji by trying to bring those Dowans documents and starting this topics about DOWANS he is doing his fare share
 
Hivi chenji ya rada ilishalipwa au bado ?, mwenye taarifa juu ya hili atujulishe. Isije kuwa ndio malipo ya hawa dawans na washirika wake. Basi na wewe shetani tuhurumie japo kiduchu. Watanzania tuna safari ndefu sana, na hatuwezi kuwa na umoja hata kidogo kwani tumetofautiana shida, wapo wanao angaikia kula ya siku, wapo ambao hawajawahi hata kuona taa ya umeme, wapo hambao hata neno serikali halipo vichwani mwao, wapo ambao leo wewe ukinunua gari yeye anachimba msingi kwenye njia ili gari lisipite, Kwa kifupi matatizo yameigawa jamii ndio maana serikali inasema kelele za chura hazimzuii ngombe kunywa maji.
 
Kwenye hili Regia,kila mwanasheria atasema kisheria inapaswa kuwa hivyo.Nina imani kubwa kwamba wananchi wengi wanaumizwa sana na hili kulinganisha na wanasheria na wanasiasa 200+,nashauri tusitegemee majibu bungeni wala kwa wanasheria,wananchi wahamasishwe zaidi na nguvu ya umma itumike,there is no other options,the judiciary is corrupt and weak,the same applies to most parliamentarians and the Executive is the worst......Watanzania kwa umoja wetu tuseme hapana,najua inawezekana kabisa....Mungu aliyeweka uozo huu kwenye fahamu zetu yuko upande wetu!!!:amen:

Mkuu Michelle nakubaliana na wewe kwa asilimia zote. Tukianza kuwasikiliza wanasheria, wanasiasa na wajanja, tutakuwa tumeingia kwenye mtego wao wa kutaka tuwasikilize. Cha muhimu hapa ni vizuri tukisema hatutaki hela zetu zitumiwe kuwalipa Dowans. Picha zinaonesha wazi hali tuliyonayo, tunahitaji sana hela hizo kwa ajili ya shule, barabara na hospitali zetu.
 
Kuna namna moja tu ya Dowans kutokulipwa nalo itakuwa by an executive order ya Rais na hilo litamtengeneza JK kuwa ni shujaa. Hakuna lolote litakalotokea baada ya hapo. Lakini nje ya hapo lazima walipwe na my thinking hadi sasa ni kuwa walipwe kabla ya Kikao kijacho cha Bunge ili waharakishe insolvency. Jamaa wanasubiria hizo fedha ziingie kwenye akaunti na kutawanywa mara moja kuliko mnavyofikiria.

Hivi tukishawalipa halafu ikajulikna kuwa hayo makampuni hayakuwepo tutamshika nani shati?
Mzee Mwanakijiji, executive order ya Rais yupi?.
Hivi kumbe na wewe Mzee Mwanakijiji na superior intuition sense yako yote hujagundua mchezo hapo?.
Nawe uko kwenye kundi linaloamini ni RA, EL peke yao?!.
Haya na tuisubiri hiyo executive order ya Rais itoke, tusije onekana tunawawangia watu humu.
Nasisitiza kikulacho ki nguoni mwako, sio RA, yeye ni just front, wenyewe wapo na siku mkiwajua, mtashindwa kushangaa!.
 
Mimi nadhani its a question "doing things right, or doing the right thing". Lawyers say we have to pay. Thats probably doing things right. But is it the right thing to do?? Dowans/Richmond was wrong right from the start... so jamani...how can we legitimise that wrong? I remember Dr. Mwakyembe's historic presentation and the anger, disbelieve and dissapointment that followed au tumesahau?
Poetik Justice, nimeipenda sana hii doctrine ya doing the thing right vs doing the righ thing. Ni ukweli usiofichika kuwalipa is doing the things right and it is not the right thing. Mara ngapi tumewahi kufanya things wrong kwa kisingizio cha doing the right thing?. Kama huko nyuma tuliweza mpaga kuyagomea masharti ya IMF na kunyinwa mikopo ya WB, itakuwa ICC?.

Tatizo letu sisi Watanzania, we are beggars, and beggars are not chooses, we have no choice but to pay ili tuendelee ku beg!.
Tusipolipa, wale wategemezi wetu watatukasirikia!, hivyo acha tuu tujilipie ili tuendelee kuomba!.
 
Regia,

You are one of a few fortunate Tanzanians who could champion what MM is suggesting, pls mobilize your fellow MPs and start the riot, we will be behind you and we will suffer with you.

Do not complain like the lot of us, do the it. ANZISHA HARAKATI ZA KUPINGA KWA NGUVU ZOTE WIZI HUU!!!!!!!!!!!!

Hakika Mh. Regia, chondechonde unganeni na wenzenu (kina Mh. Esther Bulaya) na wengine wenye nia njema na taifa letu.Tuko pamoja nanyi!
 
Back
Top Bottom