I love you V/S Nakupenda

kiswahili lugha ya mahaba jamani
kiswahili ukikitumia vizuri walahi haikuachi njiani
nambie nakupenda itaswihi kwangu moyoni
kunambia i love yu hiyo iache vyuoni!
 
kiswahili lugha ya mahaba jamani
kiswahili ukikitumia vizuri walahi haikuachi njiani
nambie nakupenda itaswihi kwangu moyoni
kunambia i love yu hiyo iache vyuoni!

Kumbe nawe umo kilingeni
Kudadavua lugha ya kiswahili
Hakika lugha hii hamu haiishi

Tena inagusa kwenye hisia
Utamu ukisimuliwa
Kweli titi la mama li tamu nimeelewa
Na rafiki yangu nitamwambia yupo sawia
 
Kumbe nawe umo kilingeni
Kudadavua lugha ya kiswahili
Hakika lugha hii hamu haiishi

Tena inagusa kwenye hisia
Utamu ukisimuliwa
Kweli titi la mama li tamu nimeelewa
Na rafiki yangu nitamwambia yupo sawia

yallait ndio tamu acha kuniita switi
hapo sijui sukari lau pipi ya kijiti
niite wa ubani au nyongo mkalia ini
sitaki kuitwa darling katu siniite hani

nambie wa barafu nakupenda
taitika kwa mahaba nikujibu bila kutinda
naitaka nakupenda najiona wako nyonda
siitaki yako bebi kwani nala viazi vya kuponda?
 
hapo kwenye pole hata mimi sijui naonaje kusema sorry. hata rafiki zangu ambao hawajui kiswahili wanajua neno pole kwa sababu yangu. siwezi kusema sorry labda kama naomba msamaha
 
kiswahili lugha ya mahaba jamani
kiswahili ukikitumia vizuri walahi haikuachi njiani
nambie nakupenda itaswihi kwangu moyoni
kunambia i love yu hiyo iache vyuoni!
tukuwoni mlongo wangu.
kumbe na wewe vina vinapanda? ha haaaaaaaaaa
 
tukuwoni mlongo wangu.
kumbe na wewe vina vinapanda? ha haaaaaaaaaa

unafikir kingoni tu kamwali!kwakweli mi nakipenda sana kiswahili,sana kwa kweli,napenda nimkute mtu anajieleza kwa kiswahili naamini anakuwa amejieleza kifasaha kabisa na maelisema lile hasa alikuwa analikusudia.japokuwa ni mwalimu wa lugha zote mbili lakini kiswahili ndio lugha naamini ni sahihi kuitumia hasa katika anga hizi za mahaba,au we unaonaje wangu?
 
Back
Top Bottom