I hate my Ex-

Jamani hebu niambieni namsaidiaje huyu kiumbe.
Few years ago nilikuwa na boyfriend where we loved each other to death, yeye mwenzangu alikuwa ni mtoto wa mama(familia bora, mboga saba),school international mi nimetokea kule swahili academy a.k.a mtakuja primary school.

After sometimes huyu mwenzangu akawa alcoholic bila ya kwao kujua,na mpaka walivyokuja kujua wakawa wanamuadhibu kwa kumnyima hela za matumizi, kwao walivyoanza kumtenga akaanza kuni abuse flani hivi, i mean nikiwa na hela basi nimpe yote akanywe pombe, nisipompa tunapigana.

siku zikaenda miaka ikapita,alivyomaliza chuo kila akitafutiwa kazi(hawezi kutafuta kazi mwenyewe coz of ulele mama) baada ya muda lazima afukuzwe kwa ajili ya ulevi.
Nikaanza kumchukia huyu kijana,maana akawa ni mlevi wa matapu tapu.

Mungu si asumani wala rajabu, nikafanikiwa kuja ulaya kubeba box hapo ndipo nilipopata nafasi ya ku move on na maisha yangu na kumsahau.

Tatizo ni kwamba anazidi kunisumbua na kila nikijaribu kumwambia abadilike hanielewi, he is about 30 bado yupo yupo tu anaishi na mama, mlevi wa gongo,ana kila aina ya kituko.
Kila nikimwambia mimi na wewe tumemalizana hanielewi, eti anasema nimebadilika sababu nipo ulaya ana beep mchana na usiku.
Now namchukulia kama best friend,nataka kujaribu kumsaidia angalau labda aache pombe.
Nikampa condition kwamba akitaka turudiane basi aache pombe, akakubali, after two month naongea nae, nikamtania kwa kumuuliza"vipi leo haujanywa? alichonijibu ni kwamba eti hana hela,kama vp nimtumie hela ili akapate beer 2.. sasa hii ni akili kweli? alishasahu kwamba aliahidi atabadilika.
i cant change my contacts na nataka awe out of my life forever nafanyaje? nisaidieni jamani.:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:
i just hate him

You sound like still in LOVE with him!!
and if thats the case then, I have only one sentence for you "FOLLOW YOUR HEART NOT YOUR EMOTIONS!"
 
Sirudi Bongo ng'o:msela::msela:hapa nimeshafika

una shida gani kama huna mpango wa kurudi home
 
Mara nyingi uwa na wasiwasi na AKILI ya WANAWAKE!

Huyu mtu amekutenda, mpaka ukachukua uamuzi wa kwenda nje ya nchi...

Baada ya kufika nje ya nchi unapata ki-simu cha kichina halafu unamtumia CONTACT...!!!!!!!!!!!!

Nadhani aliyesema uhawala hauwezi kuisha alikuwa mkweli! kha!!

Wewe mwenyewe ndiye uliyeanzisha mawasiliano baada ya kufika huko nje ya nchi, sasa unataka msaada gani?

rafiki, hata mimi lilikuwa linaniumiza kichwa hilo swali. yeye alikuwa amekusudia kabisa kuachana na huyo jamaa kabla hata hajaenda kubeba hayo mabox, ilikuwaje sasa ampe namba zake za huko? anatuzingua tu huyu, aendelee tu kumsumbua
 
Tatizo nimesha achana nae na neno ITS OVER kwake nadhani imekuwa kama wimbo wa taifa, anapotea kwa muda then anaibuka tena na ku beep na msg za hapa na pale za kudanganya kwamba amebadilika..

Atiiii??

Wewe bado UNAMPENDA sana tu ila unatuzingua.

Kuna mambo ya kuomba ushauri ila sidhani kama hili ni moja wapo.

Hujapata boyfiend mwingine tu tangu uachane na huyu ''mtoto wa mama na mlevi wa kutupwa??
 
Umesema ni U hate your EX?? Sasa unataka kusema kuwa una mwingine huko??? Hana wivu??

Uliondoka nchini kwa ajili yake ukafika huko ukampatia contact zako za nini??

Acha kutuzuga hapa bana wewe bado unampenda huyo jamaa yako endelea naye

mlete huko ulaya aje anywe vodka mpaka alale kwenye barafu maana bado unampenda sana

sina mbavu Dena kwa hii comment
 
Huwa nasikia wakisema heri kichaa uliyemzoea kuliko mpya. Kiukweli kuachana kimapenzi nje kusikosababishwa na ku cheat kunauma. Huyu dada anatamani huyu jamaa kama angekuwa na uwezo wa kuacha pombe na kuwa nadhifu tena then warudiane. Ila kama kweli anataka kutowasiliana nae tena na kwa kuwa hawezi badili line, kuna simu siku hizi waweza block individual. Dada tafuta simu hizo preferably samsung. Tafuta mtu akuelekeze how to block someone, kwa msg na calls
 
Back
Top Bottom