I got to say it..."Tumeuziwa Mbuzi kwenye gunia"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 6, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji JF Platinum Member

  #1
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,244
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 83
  yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana..

  Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda..

  Halafu kuna tetesi kuwa kuna watu wamelipa dola milioni 3... (stay tuned).. And then read my signature... It'll do u good.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,500
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 48
  Huoni kwa mbali kuwa hao ni mafisadi waliokubuhu kiasi wamefanikiwa kuunda mtandao wa kimataifa ,miradi na mikataba mingi huanzia kwenye vikao ya aina hii.
  Wanaotakiwa kuwa macho ni wananchi ,wajue ni nani na nani walihudhuria hapo na hata muhula wa Muungwana haujamalizika unaona watu wanakuja na biashara za uwekezaji na mikataba iliyokwisha farijiwa na viongozi wetu eti wanaotutakia maisha bor kila mmoja wetu.Vikao kama hivyo ni mwiba kwa Taifa changa.
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,389
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 38

  Kama wakenya wamenufaika basi inamaana sisi ndio tumeshindwa kuchangamka na sio kosa la hao " waswahili" wenzetu.
   
 4. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 18
  The whole thing was crap......
   
 5. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 1,580
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 38
  MKJ,

  Hapo sijakupata kidogo,hiyo $ 3,000,000 imelipwa na (a)wtz (kwa maana ya serikali or whatever govt authority) kwa ajili ya maandalizi ya hii Sullivan,au (b)wafanyi biashara ndo wamelipa (mf. ITV waliolipa $ 700,000 kwa ajili ya exclusive right ya matangazo)?

  Kama unachomaanisha ni option (a) ndo kusema sisi watz ndo tumeliwa na "wajanja" wachache serikalini ambao wametumia nafasi hii kuwekeza mifukoni mwao?
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,389
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 38
  Mimi nadhani cha msingi kufanyika baada ya Sullivan ni kutathmini udhaifu wote ulioonyeshwa na wafanyabiashara wetu na kubuni njia za kuuondoa udhaifu huo. Tukitumia muda mwingi kutafuta "mchawi" wafanyabiashara wetu wataendelea kuwa na udhaifu walioudhihirisha katika Sullivan.

  Tuendelee:
  1. Ilibainika kuwa wafanyabiashara wengi pamoja na waziri wao wa biashara hawakuwa hata na ratiba ya mkutano na shughuli za maonyesho! Kuinvest pesa katika shughuli bila kuwa na taarifa muhimu kama ratiba ya shughuli hiyo ni kosa kwa mfanyabiashara anayejali faida.

  Mapendekezo: Wafanyabiashara wapewe elimu ya biashara, vyombo vya habari Tanzania wekeni columns za elimu ya biashara kwa lugha rahisi ili ieleweke.Serikali isimamie elimu ya biashara kwa wafanyabiashara sio tu kwenye shule za biashara.Vyombo vya kufanya hivi vipo vitumieni ipasavyo.
  Wafanyabiasha wawe na hamu ya kujifunza.
  Kwa wale wenye access na internet nashauri kipindi cha elevator pitch cha MSNBC http://www.msnbc.msn.com/id/21134540/vp/24990860#24918070

  Mteja siku zoe kwenye biashara hana kosa, mfanyabiashara ndio mwenye wajibu wa kumfanya mteja aingie kwenye soko lake. Kwa hiyo katika Sullivan iwapo hatujanufaika basi tumeshindwa sisi sio "waswahili" na kitendo cha kusema tuachane nao tufuate wateja wengine toka Ujerumani etc kinafanya sisi tupunguze ukubwa wa soko letu. Tujielize, je wakati sisi tumeamua kuwaacha hawa "waswahili" nani atawachukua wawe wateja wake? Kama yeye ameweza kuwafanya wawe wateja wake sisi tumeshindwa nini???
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapa naona kuna tatizo kwani Mzee Mkjj, sijaona hata jema moja ulionalo afanyalo JK. Kunani? agenda za siri?
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,898
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ningefurahi kama ningepewa bajeti nzima ya mkutano huu pamoja na pesa imetoka wapi.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tatizo la sisi wa TZ ni misifa tunapenda sana kuliko kuchapa kazi.Mimi nilisha sema wakenya lazima wata tupiga bao kwenye huu mkutano nyie subirini mtaona wenyewe jamaa watakavyo anza kung'aa.
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,194
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ..
  Lawama kwa nani hapo mkuu? kama walinufaika wakenya sisi wabongo tulikuwa wapi?

  Hakuna lawama hapo fanyeni kazi!
  ..
  Kwako wazungu ndio wawekezaji sh**
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,194
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kabisa mkuu sometimes lazima tuambiane ukweli
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,035
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Kabla hajaning'nizwa mtu, wakati serikali ikijipanga kueleza jinsi nchi ilivyofaidika na mkutano huu, ninatakla CTI na TCCIA nao waje kutueleza, si kwa maneno ya blah blah, bali kwa data za uhakika, ni jinsi gani wafanyabiashara wa ndani wamenufaika na mkutano huo. Business deals anmd partnership agreements which have been established. Wakianza kuleta siasa, sitawaelewa.
   
 13. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 610
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  To me this whole thing has been more about JK than TZ...
   
 14. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2008
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata Ingekuwaje Matunda Sio Ya Siku Moja Tume Kaa Kinjaa Mno. Na Mipango Ya Leo Wala Sio Ya Muda Mfupi Wala Mda Mrefu. Mission Startment Ndio Sifuri Kabisa
   
 15. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lengo la mkutano huu ni kuisaidia Afrika kujikwamua kiuchumi. Kama tumeshindwa kunufaika na huu mkutano lengo hilo litafikiwa? Jibu ni hapana, tulitakiwa tunufaike na huo mkutano. Je ni kwa nini hatukunufaika? Ni kukosa ubunifu wa watanzania ambao unaitaji elimu na upeo wa kufikiri. Je hii elimu ya ubunifu tutaipata wapi? Je tathmini ya wenyemkutano wanasemaje? lengo limefikiwa au siyo? Kama hawa jamaa wanania ya kweli tuendelee wanahitajika basi kutufundisha namna ya kubuni biashara na siyo kutuambia tukauze bidhaa zetu marekani kwa mpango wa AGOA hali wakijua kabisa hatuwezi.
   
 16. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wakoloni wakati wakija Afrika walikuwa na lengo la kuiendeleza Afrika? Jibu ni hapana. Je tunauhakika gani hawa wawekezaji wanalengo la kuiendeleza Afrika? Hapa jamani ni lazima tukubali kusuka au kunyoa hawa jamaa lengo si kuiendeleza Afrika bali leongo lao ni kuja kufanya biashara full stop. wanatumia maneno mazuri kuwa wakiwekeza tutanufaika lakini wapi. Leo hii Holiday Inn hatuko nayo tuna jitu lingine tu sijue muda wa kulipa kodi ulikuwa umekaribia? tulikuwa na sheraton-royal palm-move n pick. Je huu ndiyo uwekezaji wa kutunufaisha? They came to do business so when we are talking with them say they are business people and not wawekezaji wakutunufaisha moja kwa moja.
   
 17. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukoloni ni bora kuliko wawekezaji. walijenga shule ili wapate watu wa kufanyanao kazi, walijenga barabara, reli, nyumba nk wawekezaji kila kitu wanatumia vyetu, barabara, nyumba za wafanyakazi wao, reli, shule, wasomi wetu, wao wanachota tu.
   
 18. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,142
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Mwanakijiji kwa hii umechemsha, tena sana, for the first Summit this is a milestone, usiwalaumu waandaaji au wageni waliofika, bali pia watu kama wewe ambao hamna knowledge summit kama hizi huwa sinakuwaje. Kwanza kabisa kwa hii summit I may suggest kuwa media coverage imekuwa ndogo kidogo. Pili usilaumu serikali kuwa watanzania hawakufaidi, ila ulaumu kuwa waTanzania ni ma-mbumbu; ndivyo tulivyo! Hakuna summit, symposium au conference kama hizi wenye hela wanakwenda, only brokers, agents, financial instutions na makampuni yanayowakilisha wenye pesa. Hawa wakirudi kwao waTawaambia wenye pesa nao wata-assess situation na in a next summit or an event wanaweza wakaja. Watanzania wenzangu we expect too much from putting nothing, it is impossible; we must put our efforts to realise the best output!
   
 19. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poorest Countries in the World
  Rank Country GDP - per capita
  1 Malawi $ 600
  2 Somalia $ 600
  3 Comoros $ 600
  4 Solomon Islands $ 600
  5 Congo, Democratic Republic of the $ 700
  6 Burundi $ 700
  7 East Timor $ 800
  8 Tanzania $ 800
  9 Afghanistan $ 800
  10 Yemen $ 900

  Source: CIA World Factbook

  Ktk hii list nchi ya Tanzania haikupashwa kuwapo kabisa kwani kila kitu tunacho. Kinachotuweka ktk hii list ni "u ndiyo mzee" kila mtu akiingia TZ akijitambulisha kuwa ni muwekezaji tunamchekea na kumpatia kiti kirefu. Sullivani pia imetu cost kwa vicheko hivyo hivyo. Kukimbilia misaada imekuwa ni tatizo kubwa kwetu pia. kila siku rais ni njia na mkuu kuomba wakati vitu vyote tunavyo. Yaani inatia kinyaa mno basi tu.
   
 20. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 18
  Wajasiriamali wadai kutapeliwa
  Wamtupia lawama Luhanjo  na Mwandishi Wetu  WAJASIRIAMALI waliokuwa wamehamasishwa na serikali kuja kufanya maonyesho ya shughuli zao wakati wa Mkutano wa Nane wa Leon Sullivan, wameitupia lawama serikali wakidai kuwa imewatapeli.

  Wajasiriamali hao, kutoka mikoa kadhaa hapa nchini na nchi jirani, walidai kutozwa fedha nyingi kwa ajili ya kupatiwa mabanda ya maonyesho, lakini wakatelekezwa.

  Wakiongea na waandishi wa habari jana katika viwanja vya maonyesho ya Nane Nane eneo la Njiro, wajasiriamali hao walisema kuwa serikali kupitia kwa viongozi wa Chama cha Maonyesho ya Kilimo na Mifugo Tanzania (TASO), wamewasababishia hasara kubwa na wanajiandaa kutafuta wanasheria, ili wafungue kesi.

  Akiongea kwa niaba ya wenzake, Thomas Mollel, alisema kuwa kuna kina mama wametoka Mkoa wa Iringa na wamekodi gari aina ya Fuso kwa gharama kubwa, lakini hadi jana walikuwa hawajauza kitu hata kimoja na wala hakuna mtu aliyetembelea mabanda hayo.

  Aidha, alisema kuwa kuna wajasiriamali wengine wametoka nchi jirani ya Kenya na wengine Zanzibar na wote hivi sasa hawajui watarejeaje makwao baada ya kupoteza gharama kubwa wakiwa mkoani Arusha, bila hata kupata chochote.

  Alisema katika mabanda hayo, kuna wajasiriamali waliolipa kiasi cha dola za Marekani 4,000 ambao wametoka Kenya na Watanzania kulazimika kulipa sh 75,000 kwa siku tangu Mei 28 hadi jana bila mafanikio yoyote.

  Wajasiriamali hao wametaka serikali kulipa gharama zote walizoigia kusafiri kutoka makwao hadi Arusha na hasara waliyoipata kutokana na maonyesho hayo.

  Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa TASO, Peter Ngasa, ambao ndio wasimamizi wa maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alikiri kutokea kwa hasara hiyo na kutupa lawama zote kwa wizara ya Mambo ya Nje.

  Ngasa alisema utaratibu mzima wa maandalizi ulihusisha kuwepo kwa maonyesho katika viwanja hivyo vya TASO, lakini wanashangazwa na wizara hiyo kutoweka ratiba ya wageni hao kutembelea maonyesho hayo.

  Aidha, akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa maofisa itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa utaratibu mzima wa mandalizi ya mkutano huo umeharibiwa na wajumbe wa kamati waliokuwepo mkoani Arusha kwa kipindi cha miezi sita kabla ya mkutano.

  Alisema walichofanya wajumbe wa kamati hiyo ni kuandaa malazi ya wageni na si kushughulikia masuala mengine.


  I think its too much ndio mana watu wamechokaaaa
   
 21. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #21
  Jun 6, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 797
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 18
  Mkuu, najua hauko serious na hayo maandishi yako. Najua unataka tu kuwachokoza wana JF waanze kububujika mambo. Najua unatafuta point kwa ajili ya Jumapili.

  Cha msingi kwa wale wote watakaochangia, wazingatie yafuatayo:

  "The Leon H. Sullivan Summits bring together political and business leaders, civil society and multinational leaders as well as members of academic institutions to focus attention and resources on Africa’s development. The Sullivan Summit was inspired by Rev. Sullivan’s belief that the development of Africa is a matter of global partnerships.

  Africa needs partners who bring skills, expertise, and resources to the challenges Africa faces. It is through these partnerships that Africa can realize its full potential.
  " http://www.thesullivanfoundation.org/summit/

  The bottom line ni kuwa, katika kujadili lolote juu ya hili, tuwe tunajiuliza kama summit ni exhibition, trade fair, open market, investment forum, au kitu gani?

  Otherwise kuanza moja kwa moja bila kuzingatia haya tutakwama.
   
 22. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #22
  Jun 6, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 797
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 18
  Pole pole Ufunuo...ukiwa muangalifu, utagundua kuwa tax holidays zimefutwa siku nyingi. Wengi tunatawaliwa na imani mbaya kuliko facts, japo ni kweli kuwa woga huu umesababishwa na kuingizwa mjini kwa miaka mingi. Lakini isiwe sababu ya kutufanya tuache kufikiri na kuanza kuamini tu kwamba.

  Kuhusu Sullivan , tembelea web site yao, na kama unaona uvivu, soma hapa na uchambue kuanzia hapo.

  "Our mission is to carry on the spirit and legacy of Reverend Leon H. Sullivan, the great African American international humanitarian, by leveraging the commitments and resources of the African Diaspora and Friends of Africa for positive change in the world...."
   
 23. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #23
  Jun 6, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,306
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aibu kubwa sana kwa viongozi wetu na rafiki zao mafisadi, wakati wakitamka kila siku jinsi uchumi unavyopaa. hapa mimi nachukulia kuwa sisi ni wa mwisho, kwa sababu ukitoa malawi tu wengine wote wana matatizo ya kivita, sisi hawa MAFISADI wanatwambia kila siku, ni watu wa uwazi na ukweli na pia kisiwa cha amani wakati watu wakifa kwa kukosa huduma muhimu.
   
 24. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #24
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo mambo yanayoturudisha nyuma kutetemekea wawekezaji mpaka unasahau na lengo lake. Maonyesho yalitakiwa kupewa kipao mbele maana ndiyo lengo hasa la mkutano huo. Jamaa walikuwa busy kuhakikisha mito ya kuegamia wawekezaji imetuna vizuri. Ovyo halafu wamekuwapo miezi sita? wakila perdeem? Ovyoo
   
 25. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #25
  Jun 6, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,695
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I believe in order to make best arguments relevant to the topic we need to arguing by throwing facts lather than personal opinions.

  For those who believe the summit was failure, please explain why? If you don't have idea about how is it a failure, then there is no problem if you will skip to the next thread.

  I personal believe the summit was succession for tourism sector in Tanzania, i also believe the ground economy received stimulus. I believe the hospitality industry receive a huge boost. I don't believe the government received anything, lather than spending TVT airtime.

  I respect those who believe kwamba mkutano haukuwa na succession kwa Tanzania, however nashindwa kuelewa why sababu no one is telling me why? Jee kwa nini Sullivan ni failure?

  Kila kitu kina mwanzo, i don't expect Tanzania iwaboost wafanyabiashara wake over night, i think pananapo fanyika maendeleo tuwe na tabia ya kusifia badala ya kuwa kama GOP.
   
 26. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #26
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Who are the friends of Africa? Sullivan and black Americans? or Investors?
   
 27. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #27
  Jun 6, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,505
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  ...Membe membe membe membe
  who else?

  anyway yalisemwa tangu awali lakini badala ya boriti kukaa machoni safari hii serikali ikahamishia boriti masikioni....

  Ombeni usahauri mtapewa.. acheni ujuvi ninyi ohooo

  Mzee Mwanakijiji tunasuburi kwa hamu kujua nani alijimwaga tujisenti twa dola milion 3
   
 28. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #28
  Jun 6, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,480
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  On a more positive note.... nadhani Tz tulikuwa na bahati ya kujifunza lessons from past summits ukizingatia hii ilikuwa ni ya nane na hufanyika biannually kama sikosei. Sasa ilikuwa kazi kwa yeyote aliyetaka kutaka advantage afanye utafiti mdogo kuona in other countries kama vile Ghana.. walivyo host walinufaikaje au walipata hasara gani ili kuepuka kurudia kosa. Nadhani imefikia wakati watz pia tujifunze kujilaumu wenyewe kwanza kabla ya kuhamishia lawama kwa wengine.Kuna various sources of information na mtu ungeweza kabisa kutafiti na kupata habari ili kufanya informed decisions.Ni upuuzi kulaumu serikali ati imewaingiza wajasiriamali kwenye mkenge!
  Isitoshe hii summit hakustukizwa kama upepo wa kimbunga...kulikuwa na muda mrefu wa maandalizi..na ulipigiwa debe sana tu... CSOs na wengine walikuwa wapi wasi raise flag na kusema...this is a scum if at all??
   
 29. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #29
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,732
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  HUU WIMBO WA WAKEZAJI KARIBU UTANIKERA.julius nyerere alijenga viwanda vitatu vikubwa vya cement hapa TZ, ytabgu tumeanza kuimba huu wimbo hakuna hata mmojawapo aliyekuja kujenga kiwanda chake, sana sana kununua hivi hivi. wawekezaji wanakuja hapa na briecase wanako[pa kwenye mabenki ya ndani wanageuka kuwa mabilionea. tumeshindwa nini kukopa kwenye mabenki na kujenga viwanda? ninaamini wazalendo wakipewa fursa kama wageni katika nyanza zote, huu wimbo wa kutafuta wawekezaji utakuwa umepitwa na wakati
   
 30. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #30
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,381
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  Mnaposema "the whole thing was crap" muwe mnatoa sababu za msingi! Na sababu za msingi katika kila hoka ndizo zinazoipa JF heshima na umaarufu.

  Tuangalie tusije kumomonyoa heshima iliyojengwa na forum hii ndani ya nchi yetu.
   

Share This Page