I go down, You come with me!

PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,997
1,997
Ilikua 'saturday before the last',
Niliwaalika rafiki zangu watatu (with spouses if they liked) waje home tuangalie EPL pamoja. Nikawahi kutoka job nikawa nimelala kidogo. Bahati mbaya/nzuri rafiki zangu wakaja na wake zao(mmojawapo na mchumba wake)...

Wakakaribishwa wakawa wako sebuleni wanaongea na kunisubiri kwa sababu nilimuomba wife asiniamshe hadi nilale 1.5 an hour....Baadaye anakuja kuniamsha akaniambia nikifika sebuleni nianzishe mazungumzo mengine nisishiriki kwenye maongezi yao kwa sababu, wanagombana na spouses wao.

Kweli nikafika baada ya salamu nikakaa kimya kusikilizia...the ladies walikuwa wanamind kwamba wameambiwa wanakuja kwenye get together+ mtoko kumbe tunakuja kuangalia mpira! Basi mi nikajua hapa nikibishana nao kama rafiki zangu tunaweza tusiangalie mpira bure so nikabaki kimya.

Lets say rafiki yangu ambaye hajaoa kati yao anaitwa Jimmy...Mchumba wake Jimmy tunafanya kazi pamoja. Yeye ni secretary wa doctor mmoja hivi. Tulivyokutana kwa mara ya kwanza ilikuwa kwamba nilisafiri kikazi kufanya research. Niliporudi ili kuanza mchakato wa kusubmit report nikakuta doctor ana secretary mpya ambaye ndo huyo shem wangu. Dada kanipiga, 'Huwezi kumuona sasa rudi keshokutwa!'. Kanizungusha hadi ikabidi inicost mwezi na nusu kukamilisha submission. Nikasikia watu kazini wanamsema kwamba ukienda ofisini kwa doctor yeye ndo anakuwa kama ndo doctor. Nikawa nimepanga kummind balaa. Bahati yake ndo weekend moja akatambulishwa kwangu kama shemeji sasa. Akawa close family na nikawa mpole.

Turudi sebuleni basi huyu dada kwa jinsi alivyo waruwaru akaaza kupik on me. Kanimind balaa kwa kitendo changu cha kuingilia ratiba za gud time za watu. Moyoni nammind(Natamani niseme kila mtu achukue zake time) lakini wife akaninong'oneza nitulie. Mpira ukaanza dada bado anaongea, mapumziko! dada bado anaongea!

OOh! Bora sisi ladies tungepatiwa cha kufanya nyie muangalie huo mpira wenu sio kutushushia weekend spirit hapa!
(Hapo rafiki zangu wote walishatulia na mwenye mchumba ndo kama hayuko vile kwa aibu iliyomjaa)

Basi nikasema sisi wanaume tuondoke tukawatch sehemu nyingine tuwaachie nyumba.
Wife akasema, Jamani kama ni Dstv nimenunua nadhani nnastahili kutaka mume wangu atulie home basi!

Kipindi cha pili nikashindwa kumvumilia nikammind mwanzo mwisho from the day ananizungusha kumuona doctor hadi kukosa adabu+aibu nyumbani kwa watu. Ndo get together ikaishia hapo kila mtu karudi kwao

Jumatatu kanifata ofisini akilia kwamba nimemvunjia uhusiano wake na mshikaji kwa sababu nisingemsema pale home asingeachika. Mi nikamuambia she asked for it. Basi kaniambia niitishe get together nyingine na nimuombe msamaha mbele ya watu wote ambao kwao nilimuaibisha. Nikamuuliza what makes her think nitakubali kufanya hivyo. Akaniambia if you love your job you will do it, akaondoka.

Mi sikupuuza neno lake la mwisho. Katika kuchunguza kiburi chake kazini kinapotoka ndo nikagundua kumbe yule doctor ambaye tunareport kwake alimuajiri hawara/small house wake. Basi tulipokutaka tena na huyu dada nikamuuliza kwa nini anmfanyia vile rafiki yangu? akanijibu simple tu kwamba nimind ndoa yangu. Nikaondoka nikiwaza whether nimwambie rafiki yangu ama sivyo. Basi mi najua nina leverage kwa Mchumba wa jimmy kwamba ataniogopa kwa sababu najua siri yake.

Jumanne kaja tena ofisini...akanikumbushia siri yetu ya kazini kwa wife wangu....( Hospital anayofanyia wife ni mojawapo ya sources ya data zetu. Sasa huyo mdada aliagizwa na bosi wake kuchukua data hapo. Akamkuta wife wakawa wanaongea then wife akawa alipewa jukumu la kuprepare na kuzihand over, akampa. Dada akamletea bosi wake na zikachanganywa na nyingine zikapublishiwa na kutumwa nje ya nchi. Basi katika data audit phase nikaagizwa nifuatilie kama uchakatuaji wa data uko sawa...Ndo nikagundua kwamba data zilizotoka katika hiyo hospital zilijigawa mara tatu kinyume na inavyotakikana, nikamuuliza secretary wa doctor akasema mkeo alinipa hivyohivyo...nikajaribu kufiacha ila akagundua kwamba mke wangu alifanya makosa na report zimefika mbali sana kiasi kwamba hospital anayofanyia wakijua kawahujumu kihivyo watamfukuza kwa sababu mgao utakuwa theluthi moja. Basi tukala kiapo cha silence. Siri ya watu watatu).

So Shem akasema, niombe msamaha or you and your wife loose your jobs mkauze juisi za azam beach na muangalizie mpira ITV tena kwenye tv ya jirani.
Mi ndo niko crossroad, kuna moral obligation ya kumuambia rafiki yangu kwamba asibip kumuacha amuache kabisa na Najua mimi kupoteza kazi ni ngumu ila sasa wife atafukuzwa
 
Ngoja nichukue kesto laiti ya tatu kwanza,naona mawenge tu.
 
Kaka pole sana, ningekuwa mimi ni wewe ningemreport kwenye vyombo husika, unajua its not only money that we are looking for kila siku, hakuna kitu kikubwa kama amani, yeye nani awakoseshe amani wewe na wife wako? let your wife akose kazi si atapaka nyingine one day? ila huyo dada anahitaji full dose, we mwambie rafiki yako ukweli atapembua mwenyewe unafki hausaidii
 
mkeo si kasoma? Ana elimu yake? Atapata kazi kwingine mwambie aanze kutafuta........

Huyo anayewablackmail mtafutieni tiba ya kumfaa, akitoka hapo asirudie tena.......

umenena mkuu, mpumbavu mmoja asitawale maisha yenu.
Fanyia kazi ushauri huu.
 
Nimekuelewa........mpumbavu fulani anataka kuwaharibia amani yenu...............msikubali
 
Hata sikubaliani nanyi Wakuu,ni kwamba kweli mnakuwa wagumu kuelewa au mnajifanya hamjaelewa ili msisumbue vichwa vyenu kufikiria ushauri wa kumpa!!!!?????story inaeleweka ila ina matukio mengi sana,nyumbani kwa mdau,ofisini kwa mdau and the so called mchumba wa mshkaji na ofisini kwa mke wa mtoa mada..
Mi nimekuelewa mueleze rafiki yako kila kitu na ukweli mtupu,kuhusu mkeo kufukuzwa kazi si mbaya atapata nyingine tena usimuunganishie kwa ofisi mnazofanya kazi pamoja kama ulivyofanya mwanzo madhara yake ndio kama hayo.
 
Inaonekana umepigia msuli library hadi kuelewa
Kama roketi sayansi

Ngoja nikupe ujanja...........kabla ya kusoma unaangalia kwanza jina la mwandishi...........kwa mfano huyu ni PetCash, kwa hiyo kila sentensi ina hitimisho lake la kipekee!! halafu unaingia kwenye kichwa cha habari kama kimeandikwa kizungu basi jua muktadha wake utakuwa kwenye aya ya pili kutoka juu na aya mbili za mwisho. Halafu usitumie nguvu nyingi kufikiri wakati unasoma aya nyingine.........wewe jikite kwenye maneno kuntu yaliyopo kwenye aya tajwa. Upo hapo?
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha

Kumbe kabla ya kusoma unamwangalia mwandishi usoni??

Hii fomula naichukua kama ilivyo, naenda kuiweka kwenye post za Fang.

Ngoja nikupe ujanja...........kabla ya kusoma unaangalia kwanza jina la mwandishi...........kwa mfano huyu ni PetCash, kwa hiyo kila sentensi ina hitimisho lake la kipekee!! halafu unaingia kwenye kichwa cha habari kama kimeandikwa kizungu basi jua muktadha wake utakuwa kwenye aya ya pili kutoka juu na aya mbili za mwisho. Halafu usitumie nguvu nyingi kufikiri wakati unasoma aya nyingine.........wewe jikite kwenye maneno kuntu yaliyopo kwenye aya tajwa. Upo hapo?
 
Back
Top Bottom