I beg to differ about BSS

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
6,832
14,192
Du nimekuwa naangaria mashindano ya vipaji vya kuimba maarufu kama bongo star search,kwa muda mrefu sasa.vijana wengi wanaoshiriki mashindano haya,huvunjika mioyo wanapokosa nafasi ya kusonga mbele,na wengi wao hufikiri kwamba bila kupitia BSS, basi hawataweza kuingia katika tasinia ya uimbaji,au kuwa wasanii wa bongo fleva na kujikwamua kimaisha,

Nimefanya utafiti kidogo,nimegundua kwamba wana muziki wengi ktk bongo fleva hawakupitia BSS,Na kila siku wapo underground kibao wanaibuka ktk bongo fleva kwa juhudi zao tu,si lazima upite BSS,BSS ni njia mojawapo lakini ukishindwa huko,si mwisho wa dunia

Maana kuna vijana kibao wanashiriki BSS kila mwaka,yupo mmoja ameisha toa single moja,lakini mara hii tena ameshiriki,

Au it is all about money! nawasilisha,think out of the box,
 
niambieni hapa ni nani alieshinda BSS tangu kuanzishwa kwake na akaendelea kuwa nyota wa mziki.

kiukweli BSS inawaua wasanii. ni wachache sana ndo wanaoskia ila wengi wao wanavuta pafu mtaani

kidogo tursker project tunayaona mafanikio yake
 
BSS ni wasanii tu hawana lolote if anaything ni mradi wahuyo mama wa kinyarwanda na mabwana zake kwenye mitandao ya simu ya jinsi ya kula hela basi!! Huyo tom boy Salama na huyo mwanaume wa kichaga kazi yao kuwaenjoy washindani kwa comments zao za kijinga ambazo mara zote ni za kuwakatisha tamaa washiriki!! Maisha plus is far more educative and beneficial to the youth!! Kep it up Masoud Kipanya &co!!!
 
I stand to be corrected, nadhani Masoud na wenzie wameanza kuwatafuta contestants.

Yah ahsante Mtu Mzima, nimecheki hapa google nimekuta stori kibao toka blogs tofauti tofauti.....

Kikubwa nilichokiona kwenye taarifa ni kuwa ameenda kutafuta watu wilayani kabisa nadhani idea yake ni kupata watu wa vijijini kiasi fulani.

Jamaa ni mtu wa tofauti sana na anastahili heshima sana kwa kipaji chake tofauti na wapuuzi wengi wasio na vipaji wala nini ila ila wanabebwa-bebwa
 
Masoud Kipanya ni mmoja kati ya artists wachache ambao ni wazalendo na wanatumia kipaji chao kwa manufaa ya wengi!!
 
Inakujia hivi karibuni, stay tuned na fuatilia TBC maana wameshaanza kutoa matangazo.

TBC hawana program watamzingua tu, ila sababu hamna jinsi inabidi tu avumilie tu na hao jamaa ambao hawawezi kusimami ratiba zao.
 
Masoud Kipanya ni mmoja kati ya artists wachache ambao ni wazalendo na wanatumia kipaji chao kwa manufaa ya wengi!!

Nina imani na Kipanya kuna siku atafanya kitu na dunia nzima itatambua kuwa Tanzania kuna watu bado na hawa mastaa wetu feki watajua nini maana ya kuwa na kipaji na kukitumikia kipaji chako badala ya tumbo.
 
TBC hawana program watamzingua tu, ila sababu hamna jinsi inabidi tu avumilie tu na hao jamaa ambao hawawezi kusimami ratiba zao.

Umeona ee, baada ya TIDO kuondoshwa TBC kwishney kabisa yani. But what to do maana maisha plus tuna i LIKE
 
BSS ni biashara, primary role ya wao kuwa pale sio kumsaidia msanii yeyote.
Wasanii washiriki wakilielewa hilo wala hawataumiza kichwa wala kukata tamaa.
 
niambieni hapa ni nani alieshinda BSS tangu kuanzishwa kwake na akaendelea kuwa nyota wa mziki.

kiukweli BSS inawaua wasanii. ni wachache sana ndo wanaoskia ila wengi wao wanavuta pafu mtaani

kidogo tursker project tunayaona mafanikio yake

Labda Peter Msechu
 
Yah ahsante Mtu Mzima, nimecheki hapa google nimekuta stori kibao toka blogs tofauti tofauti.....

Kikubwa nilichokiona kwenye taarifa ni kuwa ameenda kutafuta watu wilayani kabisa nadhani idea yake ni kupata watu wa vijijini kiasi fulani.

Jamaa ni mtu wa tofauti sana na anastahili heshima sana kwa kipaji chake tofauti na wapuuzi wengi wasio na vipaji wala nini ila ila wanabebwa-bebwa

Mkuu nashukuru wewe umeliona hilo kwamba huyu bwana kipanya anastahili pongezi za kipekee. Ilikuwa katika thread ya kusimamishwa kazi Mafuru wa NBC nikasema kuna vijana ambao ni role models na wanastahili sifa. Nikamtaja Mafuru,Mchechu mk na kuna watu walipinga sana kuwa kumuweka kipanya amongst the guys seemed to be on the drive seat of the giant corporations was wrong. Kiukweli huyu jamaa ni role model na ni mchapakazi hasa. Naisubiri Maisha Plus nione mambo mapya.
 
Usiwe na matarajio makubwa sana Mkuu, sababu watu wa namna ya Kipanya ambao wanaamini katika ndoto zao huwa wanakumbwa sana na changamoto wanapokutana na wafanya biashara..... Ndio maana ukichek mihela inayomwagwa kwenye upuuzi kama BSS ni mingi kuliko zawadi za Maisha Plus.
Wakati mafunzo yanayotolewa kwenye Maisha Plus ni makubwa sana kuliko BSS.....
Hivyo tuwe na matarajio ya wastani huku tukimuombea kijana azidi kuwa na nguvu na kuboresha kipaji chake bila kukata tamaa.
 
Wabongo bana kazi ni moja tu kuponda

Hivi mlitaka madam rita awapige marufuku wale wasilie wala kujiangusha?
Au mlitaka awalazimishe watu kuwakubali washindi wa bss?
Au mlitaka aanzishe shindano lile asi make hata shilingi?

Hivi unafikiri kumtoa mtu from ziro hadi kumtambulisha kwenye tasnia kwa njia ya bss na bado ukampa milioni 45 ambayo hata mzazi wangu alilitumikia taifa hili miaka yake yote hajapata pesa kama hiyo kama kiinua mgongo na bado mnaponda tu

Msikae mnaponda toeni basi hayo masuluhisho tuyaone
 
Nadhani bss ni matapeli wanao tumia vipaji vya vijana kujinufaisha

Kuna tangazo moja huwa naliona mara kwa mara ITV mshenzi mmoja anamwambia mshiriki, "nilichokipenda kwako ni nguo yako ya ndani tu!" Mwe, huu si ni udhalilishaji wa wazi kabisa? Halafu kipande hicho kama haitoshi ndo kinatumika kama tangazo!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom