Hvi kuna tatizo kuoa msichana aliyekuzidi elimu?

kikwakwa

Senior Member
Dec 20, 2011
105
12
mimi nna mchumba ambaye kanizidi elimu yeye ana shahada na mimi nna stashahada,wana jf naomba ushuri wenu je?kuna tatizo nikimuoa kwa kuwa amenizidi elimu?
 
Usitake kutawaliwa na inferiority complex my brother,ukiiruhusu tu hiyo umepotea...mnaweza mkaoana bila matatizo. Kinacho matter ni uzito wa penzi lenu baaasi! Hakuna kingine...
 
ebwana wee hapa cha msingi ni kuangalia je huyu dada ana hekima na anakumbaliana na kuwa mume ndio kichwa cha familia?
kama ndio basi u need not worry bwana.
 
wanamme wanaoa walowazidi elimu na kipato wavulana hawawezi.
Jipime wewe ni mvulana au mwanamme?
 
Usitake kutawaliwa na inferiority complex my brother,ukiiruhusu tu hiyo umepotea...mnaweza mkaoana bila matatizo. Kinacho matter ni uzito wa penzi lenu baaasi! Hakuna kingine...

thanx kwa ushauri sister
 
Jiamini tu kaka,
kabla ya yote lazima ukubali kua nyie ni watu wawili tofauti ambao mnaweza kutofautiana kimawazo.
Hilo ni jambo la kawaida ila usipojiamini utahisi ni dharau wakati hata mtoto anaweza kutofautiana na mzazi japo anampenda na kumheshimu.
 
halafu hajakuzidi sana, advanced diploma ni equivalent to degree. kamua twende man, ila songa na masters, akikuzidi na hapo basi labda ndo litatokea la kutokea
 
Tambua kuwa milege yake imekwenda so gari za muundo huo zinahitaji spaner safarini na ufundi wa ziada....zaidi ya hapo jiamini 6/6....ukilegea tu mafundi wa mwembe chai wapo
 
mimi ni mwanaume bt kuomba ushauri muhimu pia

Mimi ushauri wangu usimuoe. Si kwamba yeye ana tatizo, bali wewe huna capacity ya kumuoa msichana wa hivyo.

Utajiuliza kwa nini nasema hivi:
Nasema hivi kwa kuwa tayari umeshaonesha kuwa na udhaifu mbele yake. Kitendo cha kuja tu kuuliza hapa ni dalili kuwa huna maamuzi. Kama wewe mwenyewe huoni vigezo vinavyokuwezesha kumu-handle huyo mama vipi kuhusu utekelezaji wa mambo mengine ya mahusiano, nayo utakuja kutuuliza?

Huyo demu nipe mimi, nimeishia darasa la 7 lkn kwangu mimi mwanamke ni mwanamke tu, hata awe waziri mkuu, mume ni mimi. Nitafanya makamuzi na watoto atazaa, kamwe hutasikia nauliza watu eti 'nimnanihii staili gani kwa kuwa kanizidi elimu'
 
mimi nna mchumba ambaye kanizidi elimu yeye ana shahada na mimi nna stashahada,wana jf naomba ushuri wenu je?kuna tatizo nikimuoa kwa kuwa amenizidi elimu?

ndugu yangu...kama huyo mwanamke ni mchamungu wa kweli we oa tu hamna shida... Ila kama ndo aki dada wa siku hizi (santa kikwetere)kazi unayo.. Make mwanamke akishakuzidi elimu akaongezea na kukuzidi kipatao au mkalinganana atakusumbua sana..unajua mwanamke hapaswi kukuzidi akili maarifa na busara...maana itafika kipindi litatokea jambo kwenye familia yeye kwa sababu an akili na busara..ataliona(focus) kabla yako kuwa baadae litaleta shida akianza kukushauri we utamaindi utahisi kakudharau hakueshim kisa kukuzidi elimu au pesa.. Lakini yeye yuko right..ndo mgogoro utaanzia hapo...mi nkushauri mtafute uliemzidi elimu na hela ila awe na akili ili msipate watoto vilaza.. Si unajua mama anachangia asilimia kubwa ya akili ya mtoto??
 
thanx kwa ushauri sister

Karibu sana... Jiamini,usikatishwe tamaa na elimu yake.. Nina ushahidi tosha wa kaka yangu kuoa mwanamke mwenye masters angali yeye ana diploma. Na maisha yao matamuu,wapo kwenye ndoa karibu miaka 12 sasa... Na yule mwanamke akamshinikiza kaka yetu
aendelee na degree mpaka akamaliza,na ana mheshimu sana mumewe yule dada...# So usiogope...
 
Back
Top Bottom