Hivi ni lazima sikukuu kupika pilau?

SR senior

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
358
67
Nimekua nikiona hulka hii ya kila sikukuu kupika pilau, kukata kachumbari, na lisipopikwa watoto tulikosa raha...je pilau ni chakula cha lazma sikukuu?
 
Pilau ni chakula kilicholetwa na waarabu tanzania!!!hatuna budi kukipenda kama vile tunavyopenda lugha ya kiswahili kilichosheeni maneno ya kiarabu
 
Pilau ni chakula rahisi kwa siku za sikukuu maana kimejumuisha mlo na mboga yake katika pishi moja.
pia kinahifadhika kwa muda mrefu hivyo hupikwa mara moja tu na kutoa nafasi kwa familia kwenda matembezi bila kulazimika kupika tena baadae
 
tena sio kosa dogo . yaani sikukuu ipite bila kula ubweche ? utashtakiwa na jamuhuri kwa kosa hilo .
 
ni kama tradition.kama kila kila mikoa,wana vyakula vyao,ambavyo ni maarufu.
 
watz ni wagumu sana kujaribu kitu kipya tofauti na walivyozoea. Bongo watu wanaishi kwa mazoea.
 
pilau aka wali mchafu ndo mpango mzima, ukishushia na coca walahi huli mpaka kesho bajeti safi kipindi cha sikukuu
 
Nimekua nikiona hulka hii ya kila sikukuu kupika pilau, kukata kachumbari, na lisipopikwa watoto tulikosa raha...je pilau ni chakula cha lazma sikukuu?

Kwenu huwa mnapika nini?Then utafahamu kama ni lazima au la!
 
pilau aka wali mchafu ndo mpango mzima, ukishushia na coca walahi huli mpaka kesho bajeti safi kipindi cha sikukuu

Kama hili hapa?

attachment.php
 
Mkuu nikila pilau navimbiwa hata kama nakula punje moja.Viungo viungo cyo kaka mkubwa.Lete,bonge la juic na ndizi zmechanganywa na njegere samaki o nyama karanga ndani yake!walai unataman kila cku iwe cku kuu
 
Mkuu nikila pilau navimbiwa hata kama nakula punje moja.Viungo viungo cyo kaka mkubwa.Lete,bonge la juic na ndizi zmechanganywa na njegere samaki o nyama karanga ndani yake!walai unataman kila cku iwe cku kuu
 
Mimi sili pilau ila naona isipopikwa siku hiyo watoto watanuna siku nzima (kwa hivyo lazima kipigwe)

Kids wanapenda hii kitu na chips sijui kwanini?
 
hapana, hiyo yako ni biriani sio pilau


.

Mkuu, naona mkuu unataka kuanzisha Ligi!

Wewe Biriani unaijua wewe? – unajua kuna aina ngapi za Pilau (Pilaf)? – sasa kuna aina zaidi ya 1200 za Pilau and the same goes to Biriani.

Sasa kwa nini unabisha mimi naposema kuwa hii ni Pilau (Pilaf) na wala siyo Biriani?

Sasa hii ni Pilau (Pilaf) ambayo ipo katika simplest form ambapo ime-consist mchele, karoti, onions na nyama pamoja na viungo kama quince, raisin, barberry, apricots, apples pamoja na countless spices – sasa wewe umeona rangi tu ukafikiri ni Biriani? – kwa hiyo kila rangi ni Biriani?

pilau_small.jpg


Tofauti kubwa kati ya Biriani na Pilau


Labda kwa kukuambia tu ni kuwa tofauti kubwa kati ya Biriani na Pilau ni kuwa hii nyingine (Pilau) kila kitu kinapikwa pamoja yaani mchele pamoja na viungo pamoja na kama ni nyama or whatever wakati kwenye Biriani huwa mchele (plain or Fried) hupikwa separately from the thick sauce (curry of meat or vegetables).

Baada ya hapo curry pamoja na wali huchanganywa pamoja na kutengeneza layers ambapo chakula huwa of contrasting flavors za flavored rice (ambayo ilipikwa separate na spices) and intensely flavored sauce na meat au vegetables.

Sasa wewe umeona kama kuna sauce iliyopikwa separate? Au vimepikwa vyote kwa pamoja.

Tofauti kubwa ya Pili ni kuwa Biriani huwekwa Yogurt (maziwa ya Mgando) wakati Pilau haiwekwi Yogurt.

Tofauti nyingine ya Tatu ingawa siyo muhimu sana ni kuwa Biriani hupikwa kwa kutumia mchele aina ya Bismati wakati mara nyingi Pilau hutengenezwa kwa kutumia hata mchele wa kawaida.

Sasa ukiangalia kwenye hiyo picha hapo kwanza hapo hicho chakula hakijatengenezwa kwa kutumia Yoghurt (maziwa ya mgando) – sasa kwa nini unataka kusema kuwa ni Biriani?


Sasa angalia hapa chini tofauti ya Pilau Na Biriani




1. Hizi hapa chini zote ni Biriani


Biriani
biryani_small.jpg



Biriani


biryani_small_2.jpg




Biriani

biryani_small_3.jpg





2. Hii hapa ni Pilau - Pilaf


Pilau

pilau_small.jpg




Sasa na wewe lete vigezo vyako ili kuthibitisha madai yako kuwa hii ni Biriani na wala siyo Pilau.

Pia siyo mbaya hata wana-JF wakatusaidia katika hii kwa kuongezea tofauti kati ya Biriani na Pilau.



.
 
Back
Top Bottom