Huzuni - Uongozi gozi gozi

Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
71,254
105,367
Huzuni
Viongozi watukejeli kwa uhuni
Huzuni
Hotuba zimejaa habari za kubuni
Huzuni
Watunyonya vibaya kuliko kunguni
Huzuni
Ashakum, kidole cha ********
Huzuni


Muda umefika, kuanzisha vita ka Peron, Evita
Kwenye mada kukita, bila kusita ka Samwel Sitta
Katika pitapita, hasira zazidisha ndita
Napanda kijeshi ka vile Brigedia Mbita
Haya machungu, huwezi msingizia mungu au mzungu
Unaweza kukufuru kwa nini umezaliwa hili fungu
Viongozi wetu butu kuliko Mobutu
Wakati tunamuhitaji Tutu mtukutu aso kutu
Nani kawaweka? Au hii ndoa ya mkeka?
Siamini masikio na macho, wote vibweka!
Kama hamna anayedinda, wote makinda ya Makinda
Kikwete kiwete, Shein kasheheni, Pinda kapinda
Salim ka-Salim, Mwandosya katutosa
Warioba kala roba
Mijizi inatamba Yarabi toba!
Malecela kwenye machela kaanza kurithisha mikoba
Mgosi kawa bosi wa mafiosi anatuzidishia mkosi
Nani kiongozi, nani gozigozi
Nani brazameni wa mapozi na nani anayajua yetu machozi
Nani mchapakazi nani jambakazi
Na nani atinga mjengoni kwa shoo za mavazi
Nani anapanda ngazi ka Cinderellah
Huku akitafuta utukufu na mahela, beef na Rockerfellers
Nani ana nia ka Ngoliga bila kuiga
Nani bubu ka kashonwa kwa masharubu
Nani aweza majaribu ka ya Ayubu
Ni wachache sana wataweza vuka hatakama Atacama
Wakitazama zama bila hofu ya kuzama bila pama
Au bahari ya mchanga uso fahari wa Kalahari
Bongo bunge bange, bajeti mdumange
Nchi inapiga U-Turn ka blog ya Mange
Kwa viwango vya maua ya Okavango nashika bango
Hili ni jambo la jando, watoto kaeni chonjo
Tofautisha upofu, makengeza na chongo
Bongo fyongo, mpaka Ikulu uongo
Bado kidogo puto litapasuka kwa usongo
Hamna chanya, mambo hasi ka udongo
Wanafikiri ukubwa haukutoka kwenye udogo
Machela, wanahamisha Jolly Club bila tabu
Masela, hatuwezi sema twakosa sababu
Kuwashikisha adabu mujarab kiajabu
...
 
Huzuni
Viongozi watukejeli kwa uhuni
Huzuni
Hotuba zimejaa habari za kubuni
Huzuni
Watunyonya vibaya kuliko kunguni
Huzuni
Ashakum, kidole cha ********
Huzuni


Muda umefika, kuanzisha vita ka Peron, Evita
...

Du! Hiyo mistari mikali sana naona uwauzie jamaa wa Bongo flava. Itakuwa No. 1 hit instantly!!!

Kwa kweli hiyo ni njia ya uhakika ya kuondokana na uovu na umafia huu uliokithiri. Huwa wananishangaza sana raia wa nchi za kiarabu, kwani for whatever reasons, wananchi wakiamua huamua kweli bila ya kujali utawala uliopo au maisha yao. Nawa-admire sana hawa watu. I wish we were like them. Huu uhuni usingeendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom