Huyu Said Juma Nkumba CV yake kumbe iko hivi... Na makelele yote yale Bungeni!

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1206.jpg
First Name:Said
Middle Name:Juma
Last Name:Nkumba
Member Type:Constituency Member
Constituent:Sikonge
Political Party:CCM
Office Location:P.O. Box 9, Sikonge - Tabora
Office Phone:+255 787 770707
Ext.:
Office Fax:-
Office E-mail:
Member Status:
Date of Birth
EDUCATIONS
School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
Moshi Technical Secondary SchoolO-Level Education19821985SECONDARY
Isike Primary SchoolPrimary Education19731981PRIMARY
Bunda Teachers' Training CollegeCertificate in Teaching19861988CERTIFICATE
CERTIFICATIONS
Certification Name or TypeCertification No.IssuedExpires
No items on list
EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFrom DateTo Date
Secretary General Regional Admin. & Local Govt.Division Secretary20002000
The Parliament of TanzaniaMember - Sikonge Constituency20002015
Ministry of EducationTeacher Grd. III A19882000
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
CCM-Chama Cha MapinduziMember of Parliament2000Todate
CCM-Chama Cha MapinduziMember of National Executive Committee1997Todate
CCM-Chama Cha MapinduziMember of National Executive Council19921997
PUBLICATIONS
DescriptionPublished Date
No items on list
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionYears ExperienceAcquired ThroughSkill Level
No items on list

RECOGNITIONS
Recognition TypeRecognition DateReasonAction TakenIssued by
No items on list


Hivi Sikonge Mbunge wenu ndio mmeona CV yake inatosha hapa?

Sina nia mbaya ila nilijua ana Masters degree.....
 
Mkuu kwani bungeni anakwenda kuandika thesis, kutoa lecture au ?

Mi nadhani kazi yake ni kuwatetea wananchi na kujua matatizo ya wananchi na kusikiliza matatizo yao is not rocket science
 
Na kazi ya kuwatetea wananch anaifanza wapo wap wenye elimu kubwa wanafanza nin?umefilisika kimawazo ukiwa unatoa hoja jaribu kumuulza jiran yako je hii ni sawa
 
Kuna uwezo wa kuongoza na upeo wa kuelewa vitu. Kweli elimu inapanua upeo wa kuelewa vitu. Kwa mtun kama huyu hamna kitu
 
Hawa ndio madomo bwaja wazee wa "NDIOOO" na ushabiki wa chama bungeni kuliko maslahi ya kitaifa. Kwa elimu hii miswada ya sheria atajua nini huyu mwalimu. Kwake kazi yake ni kupayuka na kukilinda chama kilichompa ulaji kwa gharama yoyote hata ku-lusinde ikibidi.

Yes, sometimes you need these empty heads to run your business smoothly, that's all ccm tycoon guys do!
 
Hayo ndiyo matatizo ya kupiga kura kwa mazoea. kwa nini tusiwalaumu pia waliompeleka huko bungeni?
 
Kama ulidhani ana degree basi anafaa. Kwasababu kilichokufanya udhani bila shaka ni utendaji wake. Wapo maprofesa, kama akina Sarungi, Kapuya lakini hakuna kitu wamesaidia
 
Majimbo ambayo wabunge wake ni maprofesa yanaendeleaje kimaendeleo? Nadhani tunatakiwa kuaacha huu ujinga wa kuhusisha vyeti na uwezo wa uongozi kama kwamba vyeti vya juu=uongozi uliotukuka!
 
kiko wapi chuo cha ubunge na mimi nikasomee UBUNGE maana ndio kazi inayolipa zaidi kwa sasa pamoja na tra!
 
Wakuu huyu ndo kilaza mbunge wa Sikonga ambaye anachukiwa na wanasikonge kupita maelezo huku akiitisha mikutano na kuwatukana wananchi wake

Wanamwita mwl.wa Primary asiyejua kitu make naambiwa hata Form4 alifeli sana,huyo ndo Nkumba kilaza ambaye alipata kurudi bungeni 2010 kwa kununua ushindi toka aliyekuwa ameshinda kupitia CUF kupiga bei 100m huku Nkumba akimtisha endapo atakataa kumuuzia ushindi basi mbunge mteule asingeishi maisha katu

Mie niko Sikonge wadau lakini ukweli halmashauri imeoza kupita maelezo na Mbunge hana ukaribu na wananchi zaidi ya ndumila ku2 wachache wa CCm

Mkitaka mengi ya huyu kilaza ntawapeni pia wakuu.

Rweye,sign off.
 
Inaelekea kuna makosa mengi kwenye hizi CV za waheshimiwa wetu. Inawezekanaje huyu mbunge kusoma shule ya msingi kwa miaka TISA?
 
Majimbo ambayo wabunge wake ni maprofesa yanaendeleaje kimaendeleo? Nadhani tunatakiwa kuaacha huu ujinga wa kuhusisha vyeti na uwezo wa uongozi kama kwamba vyeti vya juu=uongozi uliotukuka!

elimu ina uhusiano mkubwa na kujenga misingi ya maendeleo. kwa mfano, kwa nini sheria zetu zimekuwa mbovu kiasi kwamba hazitusaidii kuupinga umaskini wa pato la taifa na binafsi? rasilimali tunazo lakini bado HOHE HAHE, wapi tumeanguka?

moja ya sababu ninazo amini kuwa zimetufikisha mahali tulipo, ni kuwa na viongozi ambao elimu hawana, hivyo linapokuja swala la kuchanganua faida na hasira za mambo fulani, wao ni kufuata mkumbo. Ndio wabunge wengi wa CCM, kwani hawana uwezo wa kusoma sheria, na hivyo siku zote wako upande wa serikali ambao kimsingi wamekosea kabisa, lakini wabunge hao wanapitisha sheria hizo ambazo zikianza kutenda kazi ni kilio kitupu

Mnyika, Lissu, majimbo yao yanaweza yasiwe na maendeleo kwa maana ya ujenzi wa barabara, hospital na shule kutokana na fitina za serikali kuu ambao ndio wanaogawa pesa, lakini mchango wao katika kujenga mazingira ya kisheria na kiutendaji ni mkubwa mno.

ukiwa CCM na huna elimu, wanaweza kukuhakikishia bajeti ya kutosha na hivyo kutengeneza barabara za kutosha, lakini kwa habari ya mchango wa kitaifa huna msaada wowote.

na ikumbukwe maendeleo si majengo na barabara, bali ni watu kuishi vizuri kabisa kupitia sera na sheria zake makini.

 
Sikonge tunamwandaa member mmoja anaitwa SIKONGE achukue kiti kupitia CDM!

Inasikitisha mkuu!
Nasikia hiyo wilaya inaongoza kuwa ya mwisho kimkoa kila mwaka ktk upande wa elimu. Na majuzi Mkuu wa Mkoa wa Tbr mama Fatma Mwasa amempandishia Afisa Elimu (W) kwa kutowajibika ipasavyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom