HUYU pia ATASENSWA?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Shemeji yangu(mke wa kaka) amejifungua mtoto wa kike leo saa tano asubuhi. Kwa mujibu wa matangazo na taarifa zihusuzo sensa,watakaohesabiwa ni wale waliolala tar. 25 kuamkia 26. Je,huyu mtoto na wa aina ya yake watasenswa?
 
Hapana hatahesabiwa maana amezaliwa baada usiku wa kuamkia sensa.. Yaani sensa imemkuta bado hajazaliwa

Ila kama angezaliwa saa tano usiku hapo angehesabiwa maana saa sita ingemkuta tayari amezaliwa


Hata mtu atakayekufa saa tano usiku hatahesabiwa pia mana sensa imemkuta ameshakufa

NOTE: SENSA INAANZA SAA SITA NA DAKIKA MOJA USIKU
 
Back
Top Bottom