Huyu ndiye tatizo katika nchi ya Tanzania na sio Ngeleja, Mkulo wala Maige

de'levis

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
1,222
1,567
Nimeona thread ya invisible

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/266433-mkulo-maige-ngeleja-kikaangoni-takukuru.html

Inayozungumzia waliokuwa mawaziri 3 kuwa wanachunguzwa na TAKUKURU na kuwa wameamUliwa kuwa wanaripot kila siku saa 3 asubuhi...

Hawa jamaa(Ngereja, Mkulo na Maige) hata wakichunguzwa na hata wakiamliwa kuwa wanaripori TAKUKURU kila baada ya dakika 5 hawawezi kuchukulwa hatua yoyote.

Nasema hawawez kuchukuliwa hatua yoyote maana mali niyngi walizopata kwa njia ya udanganyifu zina Baraka toka kwa rais kikwete.. na pengine niseme kwamba kuondoka kwa hawa mawaizri ni pigo kwa kikwete mwenyewe maana sasa mtiririko wa deal alizokuwa akifanya kupitia kwa hawa jamaa zimeingia doa na inabidi aanze upya.

Mali haramu walizochuma hawa mawaziri zina baraka ya mkuu wa nchi kwa sababu nae anashiriki katika kuiibia nchi kupitia baadhi ya mawaziri anaowaweka hasa kati wizara nyeti..
Ngoja nitoe mfano juu ya maige

Mwaka jana kuna taarifa zilipatikana juu ya maige kuwa ameuza vitalu bila kufata taratibu..taarifa zile zililazimu uchanguzi wa kina nawa kiinteligensia kufanyika..mwaka jana hiyo hiyo mwezi wa 8 huko arusha katka hotel ya Kibo palace maige alikabidhiwa pesa taslimu mil 600(TSH) kama malipo ya vitalu alivyogawa kwa kampuni hiyo. Ndani ya hoteli kulikuwa na vjana wa TISS maana taarifa walikuwa nazo juu ya deal hilo na mara baada ya malipo hayo kufanyika; vijana waliingia chumban na kumuweka maige chini ya ulinzi...maige alijawa na uoga sana baada ya hapo alihojiwa kwa zaidi ya saa mbili..maelezo ya maige yalitoa picha kuwa mkuu wa nchi anahusika maana maige alisema kwa mdomo wake kuwa ni kweli amegawa vitalu lakin hata yeye amekuwa akipokea maagizo toka kwa mkuu wa nchi ..alieleza jinsi mkuu wanchi anavyohusika na kusafirisha pembe za ndovu hasa katika mbuga ya ruaha kazi inayosimamiwa na ISSA ASSASI..

Maige pia alieleza jinsi mkuu wa nchi pamoja na viongozi wengine wa nchi kama lukuvi,luhanjo(aliyekuwa katibu mkuu kiongozi)yeye mwenyewe maige na katibu wake, jinsi wanavyofanya biashara ya kupasua mbao na kusafirisha kutoka msitu wa Sao Hill huko Iringa pasipo kulipia garama zozote za msitu...alieleza mengi lakini mwisho wa siku taarifa hiyo ilipofikishwa makao makuu ilileta mtafaruku mkubwa hali ambayo ilipelekea mmoja wa wakuu wa idara kuondolewa kweye idara na kupelekwa nje ya nchi katika moja ya balozi zetu huko kwa kile kilichodaiwa kuwa kwa nini amefatilia na kutuma vijana kwenda kumkamata maige..

Ngereja nae vivyo hivyo,ngereja amefanikiwa kwa kias kikubwa kwa mkuuwa nchi kupata migodi au kuwa mmoja wa wamiliki wa migodi..ngereja amefanikiwa pia kuhakikisha mkuu wan nchi anapata dhahabu toka kwa kila mgodi uliopo hapa nchi unaomilikwa na kampuni za kigeni...sasa ni katika deal hizo na wao wanapiga cha juu ..

Mkulo amefanikisha kwa kiasi kikubwa kununua na kusafirisha na kuyaingiza nchini magari ya mizigo na mafuta amabayo yote ni mali ya mkuu wanchi...leo mnapoona hizo vogue na vx zimepak ni sehemu ndogo sana ya kile alichoiba .....

Leo ninapoona TAKUKURU wanafatilia swala hili ni kiini macho maana najua hakuna lolote watakalofanywa na TAASISI KIBOGOYO hiyo...

Mwiba mkali na mbaya uliomo katika nchi ni huyo Rais wa nchi..huyu ndiye anapowachagua hawa mawaziri huwachagua akiwa na maslahi binafsi kwa kuwambia '' HAKIKISHA Napata hiki au kile..hili neno HAKIKISHA ndilo huwapa kiburi mawaziri na wanaposhika nyazifa hzo huanza kuiba na kufanya ubadhirifu mkubwa maana wanatii lile neno ''HAKIKISHA'' na wakati huo huo na wao wakinufaika na hilo neon HAKIKISHA na ndio maana mnaona wananunua majumba, wanatoa mil 500 majimboni kwao, na wengine wananunua apartments na mengine mengi. Lakini anayebaka nchi hii kinyume na maumbile bila huruma ni mkuu wa nchi..anzeni na huyu ambaye ndiyo tatizo maana hata juzi kashauriwa kutowangiza katika baraza la mawaziri baadhi ya wabunge lakini alikataa mmoja wa wabunge hao ni steven masele....

Bado kuna giza nene katika uongozi wa nchi
 
Du hili gazeti lako silielewi limejaa hasira zako km vile hukuchaguliwa ww au nduguyo au mtu wa Chama chako
Kila bi-adamu ana mapungufu MUNGU anayajua
Nakushauri acha Nchi iendeshwe km tulivyomchagua atatupangia uongozi utakaotufikisha 2015
 
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh.
Sina la kusema nawasubiri wadau,mm,pasco,philipo,paka jimmy,molemo,ritz,mzee wa rula,mkuu max,mnyika,kweleakwelea,mungi,mr liverpool,rutunga,invisible,mama porojo nk.
 
JK anaweza kuwa fisadi lakini hawezi kuwa mpumbavu kiasi hicho cha kuamini watu aliokutana nao ukubwani na kuwapa deal hatari kama hizo!
 
Du hili gazeti lako silielewi limejaa hasira zako km vile hukuchaguliwa ww au nduguyo au mtu wa Chama chako
Kila bi-adamu ana mapungufu MUNGU anayajua
Nakushauri acha Nchi iendeshwe km tulivyomchagua atatupangia uongozi utakaotufikisha 2015

Wizi ni uhalifu si upungufu wa kibinadamu kama unavyodai. Otherwise, kwa nini watu hufungwa, si wangeachwa tu kwa kuwa hakuna binadamu mkamilifu?
 
yote tisa lakini hili la kuuza ardhi chonde mkuu wangu rais wangu mpendwa mhe dr. jakaya, angalia uamuzi wako kwa mapana na marefu kwani hawa wamarekani si wakuchezea hata kidogo watakuja kutuangamiza sisi na vizazi vyetu vijavyo...
 
Huyo Issa Assasi, ndiyo mwenye yogourt za ASSASI toka Iringa? Kuna mtu aliuliza hapa jamvini kuhusu ziara za mara kwa mara za mkuu wa kaya huko Iringa!
 
umeamua kumaliza chuki zako za kukosa ukuu wa wilaya na uwaziri hapa jf.tuache tufikirie mambo ya nchi sio hasira zako
 
JK anaweza kuwa fisadi lakini hawezi kuwa mpumbavu kiasi hicho cha kuamini watu aliokutana nao ukubwani na kuwapa deal hatari kama hizo!
NasDaz, sio kwamba Kikwete anawaamini hao watu ila anapowateua wanapewa kitu kinaitwa an offer one cannot refuse! Mfano mzuri wa karibuni ni ule uteuzi wa Dr. Mwakyembe, kwa hali ya kawaida ya common sense, Dr. Mwakyembe angetegemewa kusita au hata kuzira! Lakini kumbe kitu common sense ni bidhaa adimu sana na si common kama wengi wanavyofikiria. Usishangae yaliyowakuta akina Maige, Ngeleja na Mkulo yakimkuta na Dr. Mwakyembe kama atasahau huu usemi...Loose Lips Sink Ships!
 
huyu jamaa chuki imemtawala moyoni anataka kutuambukiza na sisi,hatudanganyiki

Ndugu yangu mtu mzima akiambiwa kitu atatafakari kabla ya kusema sio au ndio. Jamaa katoa fact zake wewe pia toa zako kujibu hoja. Kusema chuki imemjaa moyoni ni kushambulia mtu si hoja. Cha maana ni kufanya uchunguzi na kuangalia nchi inavyokwenda. Mi nafikiri jamaa yuko karibu na ukweli kama sio kweli yote.
 
Wewe Tamuchungu unachopinga ni nini mbona haya mambo yako wazi hebu jaribu kufuatilia, kila mtu anajua tatizo la nchi hii ni KIKWETE na wizi wote unaofanyika hapa nchini una baraka zake na kwa kuongeza kafuatilie wizi unaofanywa na jamaa wa HOME SHOPPING CENTRE una baraka zake pia ni mambo mengi na ya aibu anafanya huyu ******. kama hizi habari una uliza siyo tu kusema jamaa ana chuki, kuwa mkuu wa wilaya bora ukauze mchicha kwani una kazi gani zaidi ya kuwa kibaraka wa rais

umeamua kumaliza chuki zako za kukosa ukuu wa wilaya na uwaziri hapa jf.tuache tufikirie mambo ya nchi sio hasira zako
 
NasDaz, sio kwamba Kikwete anawaamini hao watu ila anapowateua wanapewa kitu kinaitwa an offer one cannot refuse! Mfano mzuri wa karibuni ni ule uteuzi wa Dr. Mwakyembe, kwa hali ya kawaida ya common sense, Dr. Mwakyembe angetegemewa kusita au hata kuzira! Lakini kumbe kitu common sense ni bidhaa adimu sana na si common kama wengi wanavyofikiria. Usishangae yaliyowakuta akina Maige, Ngeleja na Mkulo yakimkuta na Dr. Mwakyembe kama atasahau huu usemi...Loose Lips Sink Ships!

Mag3,
Sina tatizo kabisa na maelezo yako; u're 100% correct ingawaje naogopa ku-comment hilo la Mwakyembe kwa hofu ya ku-divert mjadala, jambo ambalo ni donda ndugu humu JF! Usishangae, kesho hapa ukija tukakuta mjadala huu umehamia kwa akina 50 Cents!

Hata hivyo, ukiangalia anachokisema mtoa mada ni zaidi ya hiyo "an offer one cannot refuse!" Kuna sehemu anatuambia kwamba Maige alipewa Cash Money TZS 600M na TISS walipomkamata akatoa maelezo yanayoashiria kwamba mzigo umepata go ahead ya Mzee coz' mzigo ulitokana na uuzaji vitalu isivyo halali na uuzaji huo ni agizo la mkulu! Kwamba Mkullo ameagiza magari kibao tu ya mafuta ambayo ni ya Mkulu wa Kaya! Sasa hapo an offer one cannot refuse! ipo wapi?! Kikwette might be Very Bogus, But Not Bogus Enough 2b such Reckless!! And trust me, JK might be not a Good Leader but very smart in dealing with his evil issues....!!
 
Wewe Tamuchungu unachopinga ni nini mbona haya mambo yako wazi hebu jaribu kufuatilia, kila mtu anajua tatizo la nchi hii ni KIKWETE na wizi wote unaofanyika hapa nchini una baraka zake na kwa kuongeza kafuatilie wizi unaofanywa na jamaa wa HOME SHOPPING CENTRE una baraka zake pia ni mambo mengi na ya aibu anafanya huyu ******. kama hizi habari una uliza siyo tu kusema jamaa ana chuki, kuwa mkuu wa wilaya bora ukauze mchicha kwani una kazi gani zaidi ya kuwa kibaraka wa rais

Ya nini kumtaka mtu akafuatilie wakati unafahamu fika kwamba inaweza kuwa ngumu kwake kufanya hivyo?! Kama wewe una uhakika na unachokisema, weka hapa huo ukweli unaoufahamu ili wote tuujue! Kumtaka mtu akafuatilie inaonesha basi hata wewe huna uhakika na unachokisema au hauna dhamira ya kweli ya kufichua madudu yanayofanyika nchi hii! Weka hapa huo uozo unaofanyika HSC kwa msaada wa JK!
 
Ndugu yangu mtu mzima akiambiwa kitu atatafakari kabla ya kusema sio au ndio. Jamaa katoa fact zake wewe pia toa zako kujibu hoja. Kusema chuki imemjaa moyoni ni kushambulia mtu si hoja. Cha maana ni kufanya uchunguzi na kuangalia nchi inavyokwenda. Mi nafikiri jamaa yuko karibu na ukweli kama sio kweli yote.

Ni fact gani aliyoitoa mleta mada?! Labda tu mie nitumie akili ya kawaida isiyohitaji shahada yoyote! Sh. 600M, kama zote zitakuwa ni denomination ya Sh. 10,000/= then TZS 600M ni sawa na Bundles 60 zenye TZS 10M kila moja! Kama atatembea na briefcase kubwa kubwa, angehitaji si chini ya brief kubwa kubwa 5! haiingii akilini kuona waziri akiingia hotelini na mabegi ya kawaida au viroba kisha vitu hivyo vinatoka vikiwa vimetuna! Ina maana alifuatana na watu wake?! Sizani kwamba MAige anaweza kuwa foolish kiasi hicho....unaenda kuchukua mzigo haramu halafu unafuatana na watu!!! Angesema alipewa cheki au STG or Euros, at least ingeleta sense!
 
huyu jamaa chuki imemtawala moyoni anataka kutuambukiza na sisi,hatudanganyiki
chuki wakati ushahidi umeonekana nchi inaliwa? Au wewe unafaidika nini? Kila tetesi kwasasa ihusuyo ufisadi si ya kubeza bali kufanyia kazi kama kweli hudanganyiki
 
Back
Top Bottom