Huyu ndiye Rais anayetufaa 2015

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
Wana jamii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana na kwa miaka kadhaa sasa Makala za Generali Ulimwengu, na katika upembuzi wangu wa mambo japo kwa upeo nilio nao, nimejiridhisha kuwa, kwa hali halisi ya Tanzania ilipofika sasa, General Ulimwengu ndiye Binadamu anayetufaa Watanzania Kuichukua na kuiongoza nchi mwaka 2015. Natoa hoja!
 
Kuchambua mambo ya kisiasa ni tofauti kabisa na kuwa mwanasiasa na kiongozi. Ndiyo maana maprofesa wengi wanaojua kuchambua mambo wamekuwa wakishindwa kwenye uongozi wa kisiasa; mfano mzuri ni Gbago.
 
Wana jamii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana na kwa miaka kadhaa sasa Makala za Generali Ulimwengu, na katika upembuzi wangu wa mambo japo kwa upeo nilio nao, nimejiridhisha kuwa, kwa hali halisi ya Tanzania ilipofika sasa, General Ulimwengu ndiye Binadamu anayetufaa Watanzania Kuichukua na kuiongoza nchi mwaka 2015. Natoa hoja!

Urais ni zaidi ya uandishi wa makala, hadithi, ripoti, maoni etc. Uwezo wa kuandika mapungufu ya uongozi uliopo madarakani ni kitu kimoja na kuongoza ni kitu kingine, labda kasma una vigezo vingine vyenye kumfanya Generali awe rais bora, otherwise uandisshi peke yake siyo kigezo cha kutosha.
 
Uongozi si kuandika makala,wazo lako ni zuri ila fikiria vitu kama uzoefu,utashi,utayari na mambo mengine kama hayo.
 
Kuandika Makala na urais wapi na wapi!!basi dokta ricky naye awe kocha wa taifa stars kwani mpira anajua kuuchambua.
 
Wanaotufaa tayari waliomba ridhaa ya kuongoza mwaka jana,cha muhimu ni kuwapa kura 2015,hawa wasanii wa villio,vicheko na kununa tunawatosa!
 
Wana jamii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana na kwa miaka kadhaa sasa Makala za Generali Ulimwengu, na katika upembuzi wangu wa mambo japo kwa upeo nilio nao, nimejiridhisha kuwa, kwa hali halisi ya Tanzania ilipofika sasa, General Ulimwengu ndiye Binadamu anayetufaa Watanzania Kuichukua na kuiongoza nchi mwaka 2015. Natoa hoja!

Ana hoja nzuri, lakini I wouldn't consider him for presidency.Uraisi sio embe la kuokota chini.
 
Anaye faa ni DR mwenyewe Slaa huyo ndo anaweza kuihandle nchi bwana, alafu ulimwengu ndo atakuwa mshauri wake.
 
Hivi unadhani nchi ni kutoa falsafa kwenye majukwaa au kwenye magazeti? Nadhani hujui dhamana ya uongozi na ugumu wa utumishi!
 
Rais siyo tija,wala mawaziri siyo tatizo lakini uongozi uliopo ndo kizungumkuti. Binafsi nimechoka na huu uliopo kwani hata akija mtu mzuri vipi, bado kuna mizizi haijang'olewa!
 
General na mwalimu ni watanzania. Hoja iwe ni uwezo wake na umri wake. Mpaka tufuke 2015 atakuwa si chini ya miaka 65. Ni mzee anapaswa apumzike na kuendelea kutoa ushauri. Wale wanaosem,a ufundi wa kalamu na mdomo sio vigezo sahihi sana za ufundi wa uongozi. Ingekuwa hivyo ndugu yangu Mchungaji Mtikila angekuwa Raisi wa nchi siku nyingi. DR Slaa naye mwaka 2015 atakuwa kibabu atkayefaa kukaa na kutoa ushauri kwa wanachadema. Kama sikosei atakuwa anaifukuzia miaka 70 kwa karibu sana. Naamini kuna watanzania wengi ndani ya CCM, CHADEMA, CUF na vyama vingine na hata wasio na vyama walio na sifa ya kuongoza nchi hii hatuna ulazima wa kungangania vikongwe.
 
Ulimwengu nadhani ni vema akabaki na kazi za taaluma yake ya uandishi wa habari. Hawezi kuongoza nchi kama alishindwa kuongoza Habari Corporation, kampuni iliyokuwa na wafanyakazi wasiozidi 150.
 
Sawa. Lakini nchi yetu ilipofikia inahitaji Rais mwenye roho ngumu na asiye na huruma kwa wanaoiangamiza nchi yetu. Mama Migiro being a woman sidhani kama atakuwa na uthubutu wa kuwashughulikia wahuni wa nchi hii.
 
Wana jamii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana na kwa miaka kadhaa sasa Makala za Generali Ulimwengu, na katika upembuzi wangu wa mambo japo kwa upeo nilio nao, nimejiridhisha kuwa, kwa hali halisi ya Tanzania ilipofika sasa, General Ulimwengu ndiye Binadamu anayetufaa Watanzania Kuichukua na kuiongoza nchi mwaka 2015. Natoa hoja!

tanzania hatuna wagombea binafsi, uimwengu hana chama, na mwanaharakati ingawa ni mpenda mageuzi sio NCCR
 
sawa. Lakini nchi yetu ilipofikia inahitaji rais mwenye roho ngumu na asiye na huruma kwa wanaoiangamiza nchi yetu. Mama migiro being a woman sidhani kama atakuwa na uthubutu wa kuwashughulikia wahuni wa nchi hii.

huyo ndo atatuangamiza, kwani naye fisadi. Haujaona thread ya kumlalamikia askari wa tz walioko darfur? Usione umaarufu wake ukadhani anafaa kuwa raisi
 
Back
Top Bottom