mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
JE,UNAMFAHAMU PROF.ABDULRAHAMAN MOHAMED BABU?
Leo nimejikuta namkumbuka sana Mwalimu wangu Prof.Haroub Othaman Miraji.Prof.Haroub Othaman alifariki tarehe 28/06/2009,moja kati ya vifo vilivyowahi kunigusa sana katika maisha yangu.Huyu kwangu alikuwa zaidi ya Mwalimu,msomi,mwanaharakati,mnyenyekevu,asiyependa makuu,mwenye busara na mjamaa wa kweli.
Prof.Haroub ndiye aliyenifanya nimfahamu japo kiasi Komradi Prof.Abdulrahaman Mohamed Babu.Kuna vitu vingi sana ambavyo watu hawa wanafanana,lakini ni Prof.Haroub ambaye alikuwa inspired na Prof.Mohamed Babu,hasa ikizingatiwa kwamba Prof Babu alikuwa mkubwa kwa Haroub kwa zaidi ya miaka 18.Prof.Haroub ameandika mambo mengi sana kuhusu Prof.Babu kwenye kitabu kiitwacho WHEN I SAW BABU.
Si rahisi sana kuandika mengi kwa huyu Babu.Lakini historia ni mwalimu mzuri sana,lakini kwa bahati mbaya sana,katika historia ya taifa letu (Tanganyika na Zanzibar) kuna watu watu ambao wamesahaulika sana kwa bahati mbaya au kwa makusudi.Kwa mfano,Oscar Kambona (alifukuzwa uanachama wa TANU mwaka 1968,na hivyo muda mwingi aliishi uahamishoni Uingereza),historia yake inapotoshwa sana ,na taswira waliyonayo watu wengi ni kwamba alikuwa ni muasi,kwa sababu tu walikuwa na mitazamo tofauti na Mwalimu Nyerere.Pengine hicho ndicho kilimkuta Prof.Mohamed Babu huko Zanzibar kwa kutofautiana na Sheikh Abeid Karume kwa upande mmoja na Mwalimu Nyerere kwa upande wa pili.
Prof.Mohamed Babu alizaliwa mwaka 1924 huko Unguja,Zanzibar,kati ya wasomi wa aina yake katika historia ya Zanzibar.Si tu kwamba Babu alikuwa ,Msomi,bali alikuwa mwanamapinduzi,mwanasiasa,mchumi na mjamaa wa kweli.
Prof.Babu alishiriki hasa katika harakati za ukombozi wa Taifa la Zanzibar.Ni moja kati ya wanzilishi wa chama cha ZNP ambacho kilikuwa kinaendesha harakati za kuikomboa Zanzibar katika mikono ya Sultan na Utawala wa Kiingereza.
Akiwa kama Katibu wa ZNP,inasemekana Babu alisaidia sana kukijenga chama hicho,japo hakikuwa na support kubwa kama ya chama cha ASP.Harakati zake pamoja na wenzake zilisaidia sana kupatikana uhuru wa Zanzibar (tarehe 10 Desemba,1963,hivyo sasa ni miaka 48 ya uhuru wa Zanzibar).Hata hivyo uhuru huo haukudumu sana,na baadae ndipo yalitokea Mapinduzi ya Mwaka 1964.
Aidha,inasemekana chama cha Umma (Umma Party) kilichoanzishwa na Prof.Babu na wenzake,kilichangia sana katika mapinduzi hayo (Japo Prof.Shivji katika kitabu chake cha Pan- Africanism or Pragmatism?,Lessons for Tanganyika and Zanzibar Union hakubaliani na hilo).Wanachama wa Umma Party wengi wao walikuwa wamepata mafunzo ya kijeshi katika nchi ya Cuba,hivyo ndio waliokuwa wanaendesha mafunzo ya kutumia bunduki na namna ya kuipindua serikali ya Shamte na Sultan kwa wenzao wa ASP.Pamoja na kwamba John Okello anasemwa kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo,lakini wanachama wa umma party walishiriki sana,ndio maana hata kwenye Baraza la Kwanza la Mapinduzi,wanachama kadhaa wa Umma Party walikuwemo,akiwemo Prof.Abdulrahaman Mohamed Babu.
Inasemekana Chama cha Umma,kikiongozwa na Prof.Mohamed Babu kilisaidia sana katika harakati za kuunganisha Tanganyika na Zanzibar,ambayo leo tunaita Tanzania.Wakati huo Zanzibar ilianza kuyatisha mataifa ya Magharibi na Marekani,hasa kwa uhusiano wake na Cuba na Uchina (umma party ndio waliokuwa na mahusiano na nchi hizo,na sio ASP),mataifa ambayo yalikuwa ya kijamaa.
Kwa hiyo uhusiano wa Babu (socialist) na mataifa ya Uchina na Cuba,yalifanya mataifa ya Magharibi na Marekani kumtumia sana Mwalimu Nyerere ili aikomboe Zanzibar isiwe mikononi mwa Cuba na China.
Lakini kwa bahati mbaya sana,Karume alikuwa anaiendesha Zanzibar kibabe na kama taasisi binafsi bila kuzingatia utawala wa sheria.Na kwa kuwa lengo lake lilikuwa kuwatawala milele,hivyo hakujali tofauti zilizokuwepo kati ya yeye na Babu pamoja na wenzake.Hivyo Karume alikuwa katika tishio la kuangushwa,hivyo ili aweze kujinusuru,aliweka uhusiano usio rasmu na Tanganyika hasa Nyerere.Na ikumbukwe kwamba ,Zanzibar kulikuwa na zaidi ya wanajeshi 300 wa Tanganyika ili kulinda amani.
Kutokana na pressure ya Mataifa ya Magharibi na Marekani kuidhibiti Zanzibar na siasa za ujamaa,na kutokana na tishio la Karume kupinduliwa,ndipo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliwezekana.Muungano ulimsaidia sana Karume (kuliko wazanzibari) kujiimarisha zaidi na ndio maana Karume alikuwa anauita Muungano kuwa ni kama koti,likikubana unalivua.
Kilichotea baada ya Muungano,wale wote ambao walikuwa na Mlengo wa kushoto (hasa wa umma party) na ambao walikuwa tishio kwa utawala wa Karume na Mataifa ya Ulaya na Marekani,waliteuliwa kushika madaraka katika serikali ya Muungano chini ya Rais Mwalimu Nyerere ambae alionekana anaweza kuishi nao na kuwadhibiti tofauti na Karume.Hicho ndicho kilichotokea kwa Mohamed Babu kuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya Muungano na baadae kuwa waziri wa mipango.
Katika jambo la kushangaza Prof.Babu,pamoja na usomi wake,hakuweza kupata nafasi ya kutumia mawazo yake/taaluma yake katika kuisaidia Tanzania kiuchumi.Nafasi aliyopewa ilikuwa ya kisiasa zaidi,na kifupi alikuwa anapingana na sera ya kiujamaa ambazo Mwalimu Nyerere alikuwa ameiga Uchina.
Mchango mkubwa wa Prof.Babu ilikuwa ni kuanzishwa kwa Reli ya TAZARA.Ikumbukwe kwamba Wachina walikuwa na imani sana na Babu kuliko hata Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mjamaa lakini pia alikuwa na uhusiano mkubwa sana na Waingereza (wabebari).Babu alipofanya ziara ya kwanza kabisa huko China,inasemwa ndipo alipowaomba Wachina kusaidia katika ujenzi wa reli hiyo.Mwaka 1972,Babu alipokuwa katika mkutano wa Mawaziri wa OAU (sasa AU),huko Adis Ababa,huku nyuma,Mwalimu Nyerere alimwondoa katika nafasi ya uwaziri.
Baada ya kifo cha Sheikh Abeid Karume,ambaye aliuwawa kwa kupigwa risasi mwaka 1972,Prof.Babu na wenzake hasa wale wanzilishi wa chama cha umma party walikamatwa na kuwekwa ndani kwa kuhusishwa na kifo cha Karume.Hivyo Mohamed Babu alikaa kizuizini kutoka mwaka 1972 hadi mwaka 1978 ambapo aliachiwa na Mwalimu Nyerere katika kuadhimisha miaka 14 ya Tanganyika na Zanzibar.
Prof.Babu alikaa uhamishoni Uingereza ambapo aliendeleza shughuli za kitaaluma hadi mwaka 1995 aliporejea nyumbani,na safari hii aliibukia kwenye chama cha NCCR-MAGEUZI,ambapo aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Augustino Mrema ambaye alikuwa anagombea urais,lakini tume ya uchaguzi ilimwondoa kwa kile kilichoitwa kukosa sifa,hasa kutokana na historia ya nyuma.
Hatimaye Prof.Abdulrahaman Mohamed Babu alifariki dunia tarehe 5 Agosti,1996 huko Uingereza na kuzikwa nyumbani kwao Unguja.Swali ambalo najiuliza,ni kwa nini Mwalimu Nyerere alishindwa kuishi na watu aliokuwa anatofautina nao kimawazo na itikadi? Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyomfahamu Prof.Abdulrahman Babu.Je,wewe unasemaje?