nguvumali
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 4,923
- 1,325
Kwa nchi inayotawaliwa na USALAMA WA TAIFA usitegemee kutokea wazalendo wa kweli kwani wanazimwa kabla ya kufikia huo mlima wa uzalendo.
Dawa ni Moja tu. Tujitolee kutoa elimu kwa kizazi chetu ili wakifika zama zao wasiwe kama sisi wenye hekima na heshima za uoga. Tuhesabu kwamba kizazi hiki hakina jipya kwa future ya Tanzania ila kizazi kijacho ndicho tukipe majukumu ya kusimamia nchi vyema. Tumeuzwa live lakini hatujauzwa milele, tumedanganywa live but hatujadanganywa milele. tutakufa na machungu yetu moyoni but tupande mioyo ya faraja, matarajio, misimamo thabiti na jitihada kwa kizazi kijacho.
Kama hatutafanya hivyo naapa watanzania wataendelea kuchagua viongozi bomu kila ahsubuhi na kujutia jioni.
katika Yoote nayaona mabadiliko ya Umma, nawafeel Watanzania wanavyobadilika, waache kizazi cha Kikwete na kina Lowassa kife, kije kizazi cha nuclear, kwa vitisho hivyo wazalendo hawataogopa kama walivyo kizazi hiki cha kina Mgaya.
Mgaya kulinganisha na kizazi cha nyuma yeye ni shujaa.
yeye ameweza kusema maneno yaliyomkwaza Rais bila Woga, miaka kumi nyuma kwa maneno kama hayo kina Mtikila walilazwa ndani kwa kuitwa wachochezi..
hii inafanya baadhiya vijana leo kuanza kuzoea utamaduni wakuambiana makavu.....