Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

fakenology

JF-Expert Member
May 3, 2012
999
668
briandeacon.jpg

Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi.

Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.


Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''

Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.


Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

7284-NWSKZD.jpg

Watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

jfp07_jesusfilmproject_web.jpg


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.


Watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.

Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.

This is Brian Deacon who starred the Jesus Film 1979

Brian Deacon (born 13 February 1949) is a British actor. Born in Oxford, he trained at the Oxford Youth Theatre. He appeared with his brother Eric Deacon in the Peter Greenaway film, A Zed & Two Noughts (1985), as Heumac in The Feathered Serpent (1976, 1978) and as Frank Miles in the TV series Lillie in 1978.

He has been married twice: first time to Rula Lenska (1977–1987), with whom he had a daughter Lara Deacon, and the second time to Natalie Bloch (1998 to present).

Deacon's major claim to fame is that in 1979 he starred in the title role of the film Jesus. This film was made by an evangelical organization, the Jesus Film Project.
 
Wakuu Habari,

Miaka nenda rudi naangalia Movie ya Yesu hata sasa nimekaa naitazama ni movie ambayo haichoshi kutazama ila mpaka sasa sijajua ni nani aliyeigiza kama muhusika mkuu Yesu.

Ujinga Busara Naombeni Kujua.
 
Wakuu Habari,

Miaka nenda rudi naangalia Movie ya Yesu hata sasa nimekaa naitazama ni movie ambayo haichoshi kutazama ila mpaka sasa sijajua ni nani aliyeigiza kama muhusika mkuu Yesu.

Ujinga Busara Naombeni Kujua.
Kama unaangalia movie inayoitwa the passion of Jesus ilichezwa na mmarekani Mel Gibson. Lakini kama unaangalia Jesus of Nazareth hata mimi simfahamu aliyeicheza let us-hope wadau wengine wanakuja kutujuza.kejeli mwiko hii issue ni serious.
 
Kama unaangalia movie inayoitwa the passion of Jesus ilichezwa na mmarekani Mel Gibson. Lakini kama unaangalia Jesus of Nazareth hata mimi simfahamu aliyeicheza let us-hope wadau wengine wanakuja kutujuza.kejeli mwiko hii issue ni serious.


  • briandeacon.jpg
    Millions



    82012.jpg
  • of people came to know Jesus through Brian Deacon
icon.jpg
Christianity.com - Brian Deacon stepped into the role of Jesus Christ on over 20 years ago on location in the Middle East.

?Everyone get down!? came a shout.

Like a reflex action, the Israeli actors and film crew knew what to do. They groveled into the soil and covered their heads. Englishman Brian Deacon, dressed like Jesus Christ, joined his fellow actors.

Only minutes before, they had been filming the Jesus film with Campus Crusade for Christ. They were on the northern border of Israel. During the filming, Deacon pointed to the lilies of the field and taught his disciples the Lord?s Prayer.

Now in the middle of the filming, suddenly a second missile from Lebanon sailed over their heads, then exploded in a nearby empty schoolhouse. The two Arab missiles brought modern-day life into focus, while the crew filmed the life of Jesus Christ as depicted in the Gospel of Luke. After the initial scare, Deacon continued his role as Jesus.

The missile attack had happened during the filming 21 years ago, when Deacon was 30 years old. He was the only British actor among a totally Israeli cast. A member of the prestigious New Shakespeare Company, Deacon was chosen from thousands of actors who were interviewed and more than 260 who were screen tested.

The second son of a mechanic and nurse from Oxford, England, Deacon had performed in theater and film before accepting the role of Jesus Christ. ?My agent discouraged me from taking the part,? Deacon admits, reflecting about his role. ?He said I?d be type cast, as had happened with other actors.?

Many people advised Deacon how to play his part. He felt pressure from people who wanted a voice for their ideas. ?The character of Jesus belongs to everyone, and I had to find my voice and emotion for the role,? Deacon recalls.

Three weeks before the filming began, Deacon read the Gospel of Luke more than 20 times. ?It comforted me,? he said.

From the Bible reading, Deacon viewed Jesus as a man with great compassion and understanding. He decided to emphasize this role of Christ. During the seven months of filming in Israel, Deacon and others in the crew worked long hours, often starting at 4 a.m. for six days a week. Sometimes Deacon had a vast amount of dialogue on a particular day. He felt exhausted from the hours of work.

?I turned to the others and said, ?You have to help me today. I?m not sure how it will turn out.?? He then felt an unusual sense of strength.

Discussing his own faith, Deacon says, ?I?m a lapsed Catholic who hasn?t practiced his faith. I?ve had many doubts about Jesus? teaching. I?ve always found it difficult to know how truth can be proclaimed to others?the very ministry of Jesus. To me it?s more of a private matter.?

Yet during the filming, Deacon recalls some odd occurrences. One day as Jesus, Deacon stood on a rock and laid his hands on people. Suddenly an old woman clasped his arm.

?I had been expelling demons,? he says. ?Something happened to this woman, and it took her about five minutes to calm down.? For the rest of the day, the woman stared at Deacon in a bizarre way.

Other times, the filming had light moments. The 12 disciples traveled together on a bus. One day among themselves, these men discovered a wide variance of pay and decided to go on strike. The director came to Deacon and asked, ?Would you talk with these guys??

?Hey, I?m Brian Deacon, not Jesus Christ,? Deacon said. But, he discussed the problem with the men. After 36 hours, they resolved the disagreement and returned to work.

Another evening in Tel Aviv, Deacon woke up at 3 a.m. in his hotel room. The 15th floor of the hotel was on fire. From the balcony of his 18th floor, Deacon looked out on a towering inferno. Later, he learned that a British crewmember on the 15th floor had fallen asleep with a cigarette, and it had caught the ceiling on fire. No one was hurt, but the next day, they worked a full day, despite the lost sleep.

That next day, Deacon?s stand-in actor Tom Pannella said, ?That fire was the work of Satan.? The conversation frightened Deacon. Satanic influence wasn?t an idea that he wanted to consider. Throughout the filming, Deacon was aware of various problems or a spiritual dimension to the work. The production changed cameramen three times and used two different directors in the project.

?It wasn?t an easy film and at times not a happy experience,? he recalls.

For almost 18 months, Deacon worked on the film, then its promotion. To show his agent, friends, and members of the film community his acting role in Jesus, Deacon rented a small cinema on Water Street in London. The 80 guests drank wine and watched the completed film. Firsthand, Deacon saw the special impact of his role on the screen.

He said, ?I was struck with the genuine belief in the movie, not something manufactured. The film seemed to have a truth about it, and it touched those in the audience.?

After the showing, Deacon turned to other roles in the theater, film, and television. Recently, he played a villain on an English television program. It was a high-tech adventure called Bugs.

In the last 21 years, over 3 billion people in 233 countries have seen the Jesus film. Over 117 million people indicated a decision to follow Christ after watching the film, according to the recent statistics from the Jesus Film Project, a division of Campus Crusade for Christ. Also through more than 400 mission agencies and organizations, the Jesus film is available in 582 translations and 237 language versions are in progress.

Today when he looks back, it almost frightens Deacon. ?I?m just an actor,? he says. ?I was the medium. It wasn?t me that impacted those people, but it?s difficult for people to make that distinction.?

Deacon continues to receive letters of appreciation from all over the world. Part of him feels proud for this acting experience, but ?on the other hand, I don?t want the responsibility of being Jesus Christ,? he says.

He has the completed film on his shelf in his home in England. ?It?s like looking at an old school picture from your youth,? Deacon says. ?I?m pleased as an actor, but don?t put anything else into my role.?

Every day Deacon?s work from over 20 years ago is viewed by thousands of people in their own language. It continues to change lives and impact the world for Christ.
 

huyo ni BRIAN DECON mzaliwa wa uingereza mwenye asili ya uyadi.
Aliweza kupita ktk mchujo wa watu elfu moja waliopita ktk mchujo wa nani atakae kuwa nyota ktk filamu hiyo.
Aliweza kuisoma Biblia mara nyingi zaidi ili kumjua yesu kiundani.
Mwisho wa siku bwana huyu alikuja kuokoka.
Ukumbukwe kwamba filamu ya yesu ndio filamu ilietafsiriwa ktk lugha nyingi zaidi duniani na ni filamu iliyotazamwa kwa muda mrefu.
Ni filamu yenye mafunzo mengi na isiyobagua umri wa mtazamaji.
 
Aliyecheza "Passion of Christ" si Mel Gibson, huyo ni muongozaji. Kamanda mwenyewe ni Jim Caviezel. Unaweza kumpata tena katika "movie" yake matata inaitwa "Transit"...Namkubali sana huyu jamaa.


Kama unaangalia movie inayoitwa the passion of Jesus ilichezwa na mmarekani Mel Gibson. Lakini kama unaangalia Jesus of Nazareth hata mimi simfahamu aliyeicheza let us-hope wadau wengine wanakuja kutujuza.kejeli mwiko hii issue ni serious.
 
mbona zile picha za brian deacon mmetundika makanisani mwenu, na kundi kubwa la wakristo wanaamini kuwa huyo ndo yesu mwenyewe, hata wanaodai wametokewa na yesu ktk njozi huwa wanadai kwa taswira ya brian deacon, hata akina yakhe wazee wa dinu li haku tulivokuwa tukihoji tunabishiwa mpaka basi, hata picha ya bikira maria ni ya kufoj na cha ajabu sanamu lake linasujudiwa wakati ni dhahir shahir kuwa sio picha halisi. kuna haja ya wakristo sasa kuchambua yanayofaa na yasiyo faa
 
mbona zile picha za brian deacon mmetundika makanisani mwenu, na kundi kubwa la wakristo wanaamini kuwa huyo ndo yesu mwenyewe, hata wanaodai wametokewa na yesu ktk njozi huwa wanadai kwa taswira ya brian deacon, hata akina yakhe wazee wa dinu li haku tulivokuwa tukihoji tunabishiwa mpaka basi, hata picha ya bikira maria ni ya kufoj na cha ajabu sanamu lake linasujudiwa wakati ni dhahir shahir kuwa sio picha halisi. kuna haja ya wakristo sasa kuchambua yanayofaa na yasiyo faa

Tuwekee hapa picha halisi ya Yesu.
 
Heee ujue mm some tme hua naona ka sio movie? Me niljua ni yesu mwenyewe! Make hata pcha yake msalaban ktk makanisa yetu ni sawa na yeye
 
mbona zile picha za brian deacon mmetundika makanisani mwenu, na kundi kubwa la wakristo wanaamini kuwa huyo ndo yesu mwenyewe, hata wanaodai wametokewa na yesu ktk njozi huwa wanadai kwa taswira ya brian deacon, hata akina yakhe wazee wa dinu li haku tulivokuwa tukihoji tunabishiwa mpaka basi, hata picha ya bikira maria ni ya kufoj na cha ajabu sanamu lake linasujudiwa wakati ni dhahir shahir kuwa sio picha halisi. kuna haja ya wakristo sasa kuchambua yanayofaa na yasiyo faa

Hazisujudiwi ila uwepo wake unakumbusha tu uwepo tu wa kitu cha namna hiyo. Ni kama unavyoweza kuchora picha yako its not real ila ukiiona unajikumbuka. Lakini cha zaidi ni kuna hata wapagani ambao wanaabudu miti na mawe na hawana shida na mtu yoyote. Pa kuanzia kuna dini ambazo ni kitovu cha fujo na ughaidi hizi ndizo zinahitaji kufanyiwa overhaul.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom