huyu ndiye mhe LEMA JE ANAFAA KUWA KIONGOZI?

Wabunge aina ya Lema hawaitofautishi CHADEMA na CCM. Anafanana kwa kila kitu na yule Mbunge wa Rorya, Lameck Airo.
 
Eti Mwana-CDM, siami kama wana CDM ni wanafiki kiasi hiki...Mmemkuja na janja ya kujifanya wana CDM na mkianzisha topic mnajidai mkoupande wa CDM lakini mwenye akili atakujua tu...na hii kampeni ya kumzima lema au kumugombanisha na ZItto mtachemka tu...hebu jiangalie hizi topic tano za karibuni utajijiua wewe siyo CDM na kama wewe ni CDM uko kikazi zaidi...
1. · huyu ndiye mhe LEMA JE ANAFAA KUWA KIONGOZI?

2. · Sifikirii kama lema huwa anashirikisha ubongo wake ktk maamuzi,

3. · Tetesi: Chadema kuwapokea Lowasa, RA na Chenge

4. · Unavyofikiri Tanzania itajengwa na CHADEMA peke yake?

5. · Unavyofikiri Tanzania itajengwa na CHADEMA peke
 
Tatizo JF ilitawaliwa na wanaCDM sasa ndio mjue maana ya upinzani. Tatizo lenu mnataka kila mnaloleta zuri la CDM lisifiwe na kila baya linyamaziwe. Jazba iko kuanzia CHAMA hadi wafuasi. Ndio maana kinaitwa chama cha wahuni. Huyo mzee muanzisha mada amutoa maoni na ushauri wake kama mkereketwa wa chama sasa kumjibu kwa shari inamaa gani?
 
Lema ni fighter jasiri na mwanaharakati huyu...labda unataka kuhakikisha hilo kupitia sisi; tayari ni kiongozi, kuzungumzia kuwa anafaa umechelewa, tupo nae kwenye mapambano. Sioni wa kumfananisha nae (mtazamo wangu)

Naona agenda yako ni swala la Lema kuwa Rais sio? Unakoelekea sio kama wewe kweli unajiita ni mfuasi wa chadema maana taswira unayoleta hapa ni kuwapambanisha Lema na Zitto; haijengi hio...ila subiri utaona mengi toka kwa Lema.
 
:israel:UNAWEZA KUWA KIONGOZI MZURI SANA LAKINI UKAWA NA MAPUNGUFU. HAYO NI SEHEMU YA MAPUNGUFU YA BWANA LEMA YANAYO ITAJI USHAURI, NA KUSHIRIKISHA WATU WENYE BUSARA KATIKA MAAMUZI YAKE. LAKINI SWALA LA ZITO KABWE KUTUMIWA LIMEKUWA LIKIONGELEWA CHICHINI NA WATU WENGI HUMU NDANI WANAONEKA KUMLAUMU, NADHANI HATA NDANI YA CHAMA KUNA WATU WALIKUWA WANASEMEA PEMBENI, SASA JE NIKOSA LEMA BAADA YA KUSEMA PEMBENI KAMUA KUSEMA NDANI YA KIKAO CHA CHAMA, KWA HILI NA MPA BIG UP LEMA NA HATA ZITO ATAJARIBU KUREKEBISHA BAAZI YA MAMBO AMBAYO UKIANGALIA UNASEMA ZITO ANATUMIWA.
 
Yuko wapi mzee wetu bob makani amfundishe lema ni vipi kiongozi anapaswa kuwa. Huyu kijana anapotea na sijui anatumiwa mbona kila siku yy migogoro na wenzake kujifanya mungu mtu. Kuwa kiongozi hakumaanishi saa zote uwashambulie wenzako au saa zote uongee au uonekane kwenye action,
 
Hakuna kiongozi au mtu yeyote aliye kamili duniani. Kila mtu ana udhaifu wake na huwezi kufanya kitu kwa kuogopa kwamba utakosea. Binafsi LEMA ni kati ya viongozi mahiri tunao wahitaji. Tanzania ya sasa lazima tufikie hapo ndo tutairejesha Demokrasia ya kujadili. LEMA hakopeshi na hakopesheki. LEMA songa mbele na usirudi nyuma. Nafiriki kama LEMA leo angekuwa Magufuli angejiuzulu kwa vile Mh RAIS kamwaibisha. Au la pangekuwa hapatoshi.

LEMA GO GO GO AND DONT BOW DOWN. PAMOJAH SANA. ACHANA NA MAJUNGU.
 
Mkuu Mwanaone pole sana kwa machungu yako ya kisiasa.
Inaelekea unapitia ile hatua ya kuchanganyikiwa inayopelekea mtu kuwa na kiwewe na kuona maluweluwe, yaani hallucinations.
Ukitaka kufa , kufa kwa utaratubu tu na haitafikia anguko la CCM kama unavyomuomba Mungu maana Yeye anasikia hata wengine na si peke yako.
Hivyo basi kufa kwa utaratibu tukuzike kwa heshima.

Sijui, tena nasema sijui wazo lako la kumfikiria Mh. Lema na Urais umelitoa wapi , yarabi!!!
Na hapo ndo naona unaota ndoto za mchana na kuona maluweluwe.
Lema na Urais ? wapi na wapi?Ni kama mbingu na ardhi zikaishi zizi moja!
Observations zako kwa huyu Mh Lema zinaweza kuwa sahihi kabisa, lakini la kumpa dhamana ya aina yoyote nji hii, hilo wazo ONDOA.
Sababu zilizofanya wananchi kumpa JK awamu ya pili wakati alishasema hajui ni kwa nini sisi ni maskini na kitaaluma ni mchumi, sababu hizo hizo ndio zinaweza kumfanya Lema kuwa rais.
 
Msikilizi kamanda Godbless Lema kwa Wana Arusha na Watanzania kwa ujumla..


kesho njoo na kisa kingine
 
Last edited by a moderator:
Eti Mwana-CDM, siami kama wana CDM ni wanafiki kiasi hiki...Mmemkuja na janja ya kujifanya wana CDM na mkianzisha topic mnajidai mkoupande wa CDM lakini mwenye akili atakujua tu...na hii kampeni ya kumzima lema au kumugombanisha na ZItto mtachemka tu...hebu jiangalie hizi topic tano za karibuni utajijiua wewe siyo CDM na kama wewe ni CDM uko kikazi zaidi...
1. · huyu ndiye mhe LEMA JE ANAFAA KUWA KIONGOZI?

2. · Sifikirii kama lema huwa anashirikisha ubongo wake ktk maamuzi,

3. · Tetesi: Chadema kuwapokea Lowasa, RA na Chenge

4. · Unavyofikiri Tanzania itajengwa na CHADEMA peke yake?

5. · Unavyofikiri Tanzania itajengwa na CHADEMA peke

Hivi? Chadema inaongozwa na malaika? kama ni kweli tupe jibu.
Na katika orodha yako mbona huonyeshi zinazoikandia CCM kwa hivi karibuni, naambazo ni nyingi zaidi ya hizo!!
 
mwanaone asante kwa kujenga hoja,,,,sijaona hata mchangiaji mmoja aliyetoa hoja ya kupinga/kusafisha Mh Lema. wadau toeni hoja si kutukana na kutafuta wapi mtoa mada kakosea,,,ndo mana hapa JF ni pahala pa GREAT THINKERS,, km wewe unamahaba na Lema mwite ukanywe nae chai,,lkn alichokileta mtoa mada ni kitu cha ukweli.
 
Sababu zilizofanya wananchi kumpa JK awamu ya pili wakati alishasema hajui ni kwa nini sisi ni maskini na kitaaluma ni mchumi, sababu hizo hizo ndio zinaweza kumfanya Lema kuwa rais.
Mkuu babu katika maajabu ya dunia ni Lema kukarbia Magogoni achilia mbali kuingia pale ndani.
Yeye ataishia kuandamana pale getini na nyie mkimsindikiza.
 
ukifuatilia historia yake utakuta alikuwa jambazi, matajiri wa arusha sina hamu nao!

Sorry to say this but small minds talk about people... Jamii forums tujitahidi kuongelea issues na sio mtu. Ndugu yangu Ndumbayeye, remember this, you are not what you, you are what you make.

Lema anaweza asiwe your cup of tea lakini anamchango kwenye mambo yanayosibu taifa hili leo. Mfano keshatoa warning/somo tosha kwa viongozi wetu wakuu kwamba kuanzia sasa wananchi hawatavumulia funika funika kwenye mambo ya msingi kama aliyojaribu Mh Pinda & Arusha saga.
 
Sifikirii kama Lema huwa anashirikisha ubongo wake ktk maamuzi.

Ndugu zangu ktk jambo ninaloshukuru ktk maisha yangu ni kutokuwahi kuwa CCM, siku zote ktk kipindi hiki kifupi nichobakisha ktk maisha yangu namuomba Mungu anipe umri nitakaoweza kushuhudia anguko la CCM.

Tangu zilipoanza siasa za vyama vingi nilikuwa natamani WATANGANYIKA tuwe kama WAZANZIBAR ndugu zetu wa visiwani walinifurahisha sana zilipoanza SIASA ZA VYAMA VINGI walifunguka mapema na kuona ni wakati muafaka wa KUIANGUSHA CCM japo mpaka leo wameshindwa kutokana na WIZI WA CCM.

JAPO HIVI SASA NAFURAHI WATANGANYIKA TUMEAMKA ZAIDI YA WAZANZIBAR NA NAAMINI 2015 CCM WATAKUWA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI. NA CHADEMA KITAKUWA CHAMA TAWALA.

Lakini ndugu nimekuwa nikiwafuatilia kwa karibu sana MAWAZIRI wetu watarajiwa kwenye SERIKALI MPYA ya CHADEMA hapo 2015. Huyu waziri wetu mtarajiwa wa MAMBO YA NDANI mheshimiwa LEMA nahisi ana walakini.

Kwangu kiongozi shupavu ni yule;

1: mwenye hekima
2:mwenye busara
3:mwenye kufikiria kabla ya kuzungumza au kutenda
4: na jasiri

Nina posema kiongozi jasiri simaanishi yule ambaye yuko tayari kupigana wakati wowote au kutukana wakati wowote kwangu mimi kiongozi JASIRI ni yule ambaye ana uwezo wa kudhibiti HASIRA ZAKE.

5: mwenye kuona mbali
6:mwenye kuwaheshimu viongozi wenzake
7:asiye na majivuno ya kuona yy pekee ndio mwenye uchungu wa nchi hii

Ktk sifa zote nilizoorozesha hapo kwangu mimi nahisi na naamini ndio kiongozi bora anatakiwa kuwa nazo lkn nina hofu itakuwaje siku mhe LEMA AKIWA NDIO RAIS WA NCHI HII AU WAZIRI MKUU WA NCHI, AU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI HII AU WAZIRI WA ULINZI WA NCHI ETC

Ndugu zangu nina mashaka nae na ikiwa kama raia mwema na mpiganaji wa jeshi la wanyonge wa nchi wenye kutaka maendeleo kwa njia ya AMANI nahisi mhe LEMA inabidi apunguze HASIRA, JAZBA, KUJIFANYA YEYE PEKEE MWENYE UCHUNGU, PIA AWE MWENYE KUFIKIRIA KABLA HAJAONGEA AU AJITAHIDI KUUSHIRIKISHA UBONGO WAKE KTK MAAMUZI YAKE IKIWA HASWA YY
NI KIONGOZI PIA NI KIOO CHA JAMII.

Mheshimiwa LEMA amekuwa mara kwa mara akitaka kutumia MABAVU au amekuwa akiwashutumu au kutumia lugha mbovu dhidi ya viongozi wenzake especially kwa MHE ZITTO.

NA HIVI KARIBUNI AMEKARIRIWA AKISEMA MILANGO IFUNGWE ILI WABUNGE WAPIGANE HII NI KUONYESHA LEMA SIO JASIRI, HANA HEKIMA, HANA UVUMILIVU. N

AOGOPA SANA AKIWA YY NI RAISI ANAWEZA KUTUUINGIZA KTK MIGOGORO MINGI DUNIANI.

Mheshimiwa ajue siasa si uwanja wa FUJO siasa tunaka hoja na kuvumilana, na sio saa zote kuwashutumu wenzake kuwa ni wanatumiwa na kama ana ushahidi autoe ili wachukuliwe hatua stahiki sio kuleta shutuma zisizokuwa na msingi na umaarufu anaotaka wa fujo utamtokea puani.

Nadhani mhe LEMA utaisoma habari na utanielewa, mimi ni mfuasi mahiri wa CHADEMA NA NIMESHINDWA UVUMILIVU WA HIZI KAULI ZAKO.

IKIWA KUNA POPOTE NIMEKOSEA UTANISAMEHE USIJE UKASEMA UTANITAFUTA ILI UNIPIGE KAMA ULIVYOTAKA KUWAPIGA WABUNGE WA CCM BUNGENI.

hapo kwenye red ndo unatakiwa na wewe uwe hivyo ili tuwe wengi tunaopigania nchi yetu. vinginevyo una wivu na nyota ya dogo.
 
Sifurahii wabunge wetu kutaka kuzichapa mjengoni! Ila pia hakuna kifungu cha sheria zozote Kubwa wala ndogo wala kanuni za bunge zinazoruhusu kuzomea bungeni(kama zipo nielimishwe).Sasa pale inapokuwa kuna mbunge anatoa hoja ambazo ni za msingi kabisa na kuna mwingine anazomea,hii ni dharau.Nasikitika ni tabia ya wazi iliyoasisiwa na CCM na inaendelezwa.Inakera. Mie syo mwanaCDM wala siko CCM! Ila naamini kila binadamu hata awe na hekima kama za Suleimani,awe mvumilivu kama punda kihongwe,awe jasiri kama simba, bado ana mwisho wa kubeba kero! Simlaumu Lema kwa hilo namlaumu spika anayejisikia kuwa mwalimu wa chekechea fulani! (Nadhani hii ndiyo wanawake wanaweza yenyewe) na wakiendelea kuweza hivi iko siku hii nchi italala makorongoni.

Hebu tusiangalie hapa tunapoangukia kwani hapa hakuna tatizo haswa.Tulitakiwa kushangaa tangu ilipolazimishwa Mh.Makinda kuwa spika.Ukiacha uzoefu na elimu bado wanaomjua walitakiwa waelewe ni mtu mwenye jazba za haraka na mwenye maamuzi yasiyofikiriwa kwa kina,kitu ambacho ni hatari kwenye sehemu nyeti kama bunge.

Tulitakiwa tupinge kwa nguvu zote hii tabia ya kuzomea tangu ilipoanza.Kila mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa Tanzania wenye haki sawa na wengine wowote.Kwa hiyo under no circumtances kuna mbunge;regardless ametoka wapi anapata haki ya kumzomea mwakilishi wa wananchi wengine.Ni utovu wa adabu kwa mwakilishi huyo na wananchi wake waliomwona anafaa wakamchagua.

SO pale ambapo sheria,kanuni na taratibu hazifuatwi,huwa heshima haipo.Na heshima inatoweka kwa sababu tu kuna wabunge wanaojidanganya kuwa wao ni superiors,kitu ambacho kikatiba kwa dhana ya haki na usawa hakipo. Sasa pale usawa unapotishiwa kutoweka ni lazima kifanyike kitu kitakachourejesha. Kutokana na misingi kuwa USAWA HAUOMBWI mi nafikiri mtu anapoamua kufanya "what it takes" kurejesha usawa siyo mbaya sana kwani ilianza kuwa mbaya pale usawa ulipoondoshwa bila kuzingatia haki za wote.

Nimalizie kwa kunukuu maneno ya jaji fulani hapa majuzi kuwa "PALE AMBAPO HAKI NA USAWA VIMEKUWA HAVISIKIKI;VIMESIKIKA RISASI NA MABOMU"

Sheria ziwe za wote ili iwe kweli ni kama msumeno!

Mkuu sitasita kumshangilia mtu mwenye hoja. Nakupa tano. Umenena kwa hoja. Umeonyesha kilichomfanya Lema atake milango ifungwe ili wapigane!! Pamoja na hayo ni vyema Mh. Lema akapunguza jazba. Sijui kama kwenye mkutano wa CHADEMA Lema alizomewa na Zitto hado kutake kutokea tafrani!!
 
ndugu zangu viongozi wetu wa chadema sio waungu watu ni binadamu kama sisi so pale wanapokesea au wanapoenda kinyume na vile ambavyo kiongozi anapaswa kuwa ni wajibu wetu sisi kuwakosoa na kuwakumbusha. kakutakiae mema hukwambia ukweli na sio saa zote kukusifu. jamani hao mitume walikosea sembuse viongozi wetu wa chadema. imekuwa tabu humu ndani ukimkosoa kiongozi inaonekana wewe ni msaliti. tusiwe ka CCM ulipoanza mfumo wa vymama vingi na walipoanza kukoselewa na vyama vya UPINZANI WALISEMA SIO KWELI . LKN HIVI SASA WANFANYAJE WANASEMA WANAJIVUA GAMBA KWAHIYO WAMEKUBALI. CHA MSINGI HAPA NI MHE LEMA NA VIONGOZI WENGINE WA CHAMA CHETU KUJIREKEBISHA NA SIO VINGINEVYO.
 
Back
Top Bottom