Huyu ndiye anafaa kuvaa kiatu cha Mwl Nyerere

MUGOLOZI

Member
Jun 22, 2011
28
7
Ndugu wanajamii forum, ni nafasi nyingine tena ya pekee kuweza kuongea nanyi kuhusu maswala ya taifa letu ambalo tuseme ndiyo maisha yatakayoongoza vizazi vyote.

Nchi yetu tangu Mwalimu atoke madarakani ndiyo mwanzo wa kuparaganyika kwa maadili ya taifa kwani yeye aliyajenga kupitia mawazo yake ya Ujamaa na kujitegemea, huyu ndiye aliyemlea mtanzania kimwili na kiakili (kiroho). Watu kwa kuheshimu misingi ya Ujamaa walijikuta wanaenenda na vitabu vitakatifu kama kuruani na biblia. Lakini maadili haya nchi haina tena na mbegu chafu zinazidi kuoteshwa katika taifa la Nyerere. Hebu tuone matukio yafuatayo:
Baada ya Mwalimu alifuatia Mzee Mwinyi (ruksa), mzee huyu aliweza kubadilisha taifa kutoka mfumo wa Ujamaa hadi Ubepari ambao ulianza kuonekana kwa hali mbalimbali, binafsi nasema Mwinyi alijitahidi kwani alitoa taifa katika mfumo mmoja hadi mwingine japo athari zake zimekuwa kubwa kama ilivyo kawaida ya Ubepari naweza kusema alifanya hivyo bila kujua au alijua lakini alishindwa kuepusha. Tatu, aliingia Mzee Mkapa (Mr. Clean), hapa ndipo kasi ya kukua kwa Ubepari kulishamili kwani aliongeza kasi ambazo ni mbolea ya Ubepari, kwa nafasi yake namwona alipiga hatua fulani katika Utawala wake kwani mbali na kuzikuza sela za magharibi aliweza kufuatilia mambo muhimu sana kwa ustawi wa jamii kama vile Elimu na kujikita katika kuboresha miundo mbinu kwa hili namsifia. Nne ameingia Mr.Kikwete (........), hapa sasa watanzania ndipo tulipo, naweza sema mzee huyu aliingia kwa mapenzi ya wananchi wengi lakini kashindwa kuleta matumaini ya wengi kama walivyo tarajia. Tatizo ni nini?. Jibu ni dogo tu kwani ni kwamba ameshindwa kutengeneza sela zinazoweza kujenga mfumo maalum wa kiutendaji, amevaa viatu vikubwa vya Maraisi wawili nyuma yake ambavyo ni vikubwa sana na awezi kutembea. Kwasasa hakuna dira ya maendeleo ya taifa ndiyo maana leo hili kesho lile.
Ndugu wanajamii forum tunahitaji viongozi wanaodhubutu kuonesha taifa dira maalum si leo Mkukuta kesho Mkurabita kesho kutwa Kilimo kwanza bila mpango madhubuti wenye nia endelevu. Mnaweza kuwa shaidi wangu kwamba Inchi nyingi zimeendelea kwa sababu ya kutengeneza mifumo, Nyerere alijua nini maana ya mifumo ndiyo maana uongozi wake ulipata mwelekeo zaidi.
Jibu la swali langu nafikiri limefikiwa, anayeweza kumrithi Nyerere ni yule atakaye tengeneza sera hatimaye mfumo wa maisha (kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni) na siyo kuleta kauli mbiyu ili kuvutia kundi fulani kwa manufaa ya Chama fulani. Leo hii vijana wengi vyuo vikuu wamejipaga lini wamalize waende nao wakaibe, tatizo si wenyewe ila ni mfumo unaowatengeneza. Mwalimu aliamini kuwa hatua mbele haiwezekani kama hakuna elimu na hiyo elimu iwe na lengo fulani, (EDUCATION FOR SELF RELIANCE), leo wanafunzi wa vyuo vikuu waishi katika mazingira magumu (vulnerable environment) najua wote mnajua na wataalamu wenye nia njema fanya utafiti (research) mtajibu hoja zangu. Baadhi ya vyuo miundombinu ni ya Mwalimu na ukizingatia imechakaa, wanafunzi wanaishi mitaani hakuna hostel za kutosha lakini vyuo vinaongezeka, wanafunzi wanalipa ada ambayo kuipata ni lazima watumie fedha yao ya kujikimu na hatimaye wanashindwa kutulia na kufikiria kama yanavyopaswa kuwa masomo ya chuo kikuu lakini tunashuhudia bungeni wabunge wanagombania posho,mambo mengine ntayaongeza katika nafas nyingine, Je, hawa ndiyo wasomi tunao waandaa? . Kiongozi tunayemhitaji asijivunie namba ya wanafunzi bali ubora wa elimu husika, ni sawa na mzazi anayezaa watoto wengi lakini anafurahi wingi wao huku wakidhoofika na utapia mlo. Viongozi wenye kupenda maendeleo ya wengi ndio kilio chetu si wale wanaolala bungeni na hatimaye kuamshwa ili waweze kukubali mswada hata kama alikuwa amalala aseme NDIYOOOOOOOOOOO ili mradi hoja za chama chake zipite na huku akidhani anamkomoa zito na Mnyika. Atakaye mrithi Nyerere ni yule atakaye tumia maneno yake kuwa (He who pays the piper should call the tune) yaani kila amlipaye mwimbaji lazima amchagulie wimbo, viongozi wanaokubali kuyumbishwa na mabepari ndiyo hao wasioweza kutengeneza sera kwani hawana sauti, leo wataambiwa fanya hili kesho lile na watakubali tu. Hawa viongozi tumewaona wanaweza kusafiri hadi Marikani kuomba mradi wa billioni 1 huku wakitumia bilioni 5 bila kufikilia ilimradi waonekane kwenye picha na wazungu.
Naona nisiwachoshe tafakari ni lini Tunampata mrithi wa MWALIMU. kwani sifa nimewapa.
 
labda huyu
267416_141918939216775_100001960098301_286787_3622046_n.jpg
 
Maneno mengi ya kuchosha lakini point yenyewe kumbe ni debe kwa Slaa!
 
Mjadala huu hauna tija. Nyerere aliondoka madaraka miaka 26 ilitopita na kufariki karibu miaka 12 iliyopita. Toka wakati huo, tayari nchi yetu imeshuhudia marais watatu. Sijui kama mwenzetu anaamka usingizini leo na kuliona ombwe la Nyerere? Au wakati huo ulikuwa hujazaliwa mzee. Kama ni hivyo tunaweza kukusamehe. Otherwise, hii hoja iko time barred.
 
wapi slaa ametajwa???? kumbe mnamkubali kiana eeeeeh... sifa njema zote zinamgusa dr

Tukubali kwa rhetoric za jukwaani tu? Tungeliona hili kupitia uwakilishi wake bungeni na management ya resources za jimbo. In any case mrengo wa Chadema na ule wa Mwalimu Nyerere ni miwili tofauti.
 
Kwa kufuata ubora:
1:Dr. Slaa
2: Babu wa vikombe Samunge!

Life is a bitch, and death her sister! (i like this signature, sijui ni ya nani vile, nimemsahau!)
 
Mjadala huu hauna tija. Nyerere aliondoka madaraka miaka 26 ilitopita na kufariki karibu miaka 12 iliyopita. Toka wakati huo, tayari nchi yetu imeshuhudia marais watatu. Sijui kama mwenzetu anaamka usingizini leo na kuliona ombwe la Nyerere? Au wakati huo ulikuwa hujazaliwa mzee. Kama ni hivyo tunaweza kukusamehe. Otherwise, hii hoja iko time barred.

Mkuu umesoma masomo gani? Unafahamu kitu kinaitwa Historia??? Kwanini tunawakumbuka akina Nkrumah, Abraham Lincoln, Mahatma Gandhi, Chief Mkwawa, Mao Titse na wengine wengi????????????

Mkuu umeteleza kuikwepa historia ya Mwl Nyerere kwa ajili ya kusahihisha kizazi cha leo? Kama ndivyo tukusamehe!!
 
Kiatu cha baba wa Taifa kitamfaa yule
  1. Mzalendo wa kweli - Mtanzania halisi anayejua tunataka nini watanzania
  2. mwenye kujua kuwa binadamu wote ni sawa
  3. asiyehubiri masuala ya udini
  4. aneejua kuwa maendeleo yanatoka ndani(sio kwa kutegemea misaada)
  5. msikivu
  6. mwenye kutunza na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kuneemesha watanzania tu
  7. ....
 
Kiatu cha baba wa Taifa kitamfaa yule
  1. Mzalendo wa kweli - Mtanzania halisi anayejua tunataka nini watanzania
  2. mwenye kujua kuwa binadamu wote ni sawa
  3. asiyehubiri masuala ya udini
  4. aneejua kuwa maendeleo yanatoka ndani(sio kwa kutegemea misaada)
  5. msikivu
  6. mwenye kutunza na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kuneemesha watanzania tu
  7. ....

7. Asie fisadi
8........................

IS NOT YET BORN!
 
Back
Top Bottom