Huyu Ndio Ngeleja Mnaetegemea Atatue Tatizo la Umeme

Ukienda siku za wkend club 84 iliyoko Dodoma kipindi cha bunge ni nadra sana kumkosa waziri ngeleja. Lkn kibaya zaidi ni kipindi hiki ambacho nchi iko kwenye crisis ya umeme waziri huyu bado ana muda wa kwenda kukata viono na wanafunzi wa UDOM 84. Hivi mtu kama huyu tuliyemakabidhi wizara nyeti kama hii atakaa saa ngapi na kufikri namna ya kutatua tatizo hili? Inasikitisha kumuona waziri wa wizara nyeti kama hii akiwa dancing floor anashindana na watoto wadogo kucheza kwaito na bolingo saa 8 usiku wakati nchi iko gizani. Watanzania kwa serikali hii ya akina ngeleja matatizo yetu hayatakuja kuisha.
angekesha kanisani ingekuaje?
 
Mi ni mwanafunzi wa UDOM, nasema ukweli kutokana naogopa dhambi, nimewahi kukutana na Ngeleja disco clab84 na nikashangaa sana, nikajaribu kumuuliza mwenzangu ambaye anamazoe ya kwenda sana hapo clab84 akaniambia huwa yeye ameshakutananae karibia kila anapokwenda clab84, hivyo alichosema hapo ndugu yangu ni kweli kabisa!
 
<br />
<br />
Kwenye hii picha Vasco da Gama II anaonekana anafatilia mambo. Huyo Ngeleja kalala. Kwanza ni fedheha unalala mbele ya bosi wako wakati wa kazi. Hilo peke yake lingemtosha Vasco kumtimua kazi. Tatizo Vasco naye kilaza tu.

Wee vipi, hebu angalia hiyo picha kwa umakini-hao wote wamelala yeye na boss wake hiyo ni geresha tu kuacha kijitabu wazi
 
Mi nashanga sana Tanzania ina watu wengi wasomi na walio-serious sijui kwanini Kikwete aliunda Baraza la Mawaziri lilijaa wapumbavu na wasiojuwa hata la kufanya, au CCM inataka kusema wabunge wake wote ni vyote! Najuwa mawaziri wapuuzi kama huyu walikuwa wanapewa wizara kama za jinsia, michezo, mwisho kabisa vijana.

Ndio maana namlaum sana Pinda maana kama siyo Mnafki alipaswa kumsaidia Rais jinsi ya kuunda Baraza imara kulingana na uwezo wa mawaziri kama rais hamsikilizi kama alivyofanya kwa swala la Jairo basi ajitoe ili amwachie serikali yake.
 
1. Unaingilia maisha binafsi ya Ngeleja, wewe ukicheza na watoto wa shule nani anakumulika? Hili sio tatizo kwani wako wengi. Acha
2. Wewe umeshiriki kumkabidhi Ngeleja wizara, maana unasema "tuliyemkabidhi wizara nyeti". Hiyo hujui hata kapewa vipi, acha.
3. Unasema nchi iko gizani na muheshimiwa anaruka majoka! Inawezekanaje kucheza muziki katika kiza totoro?

Jipange upya na uje umshambulie vizuri waziri Ngeleja

Ana siku 21 tu za kuleta hoja mbadala kutatua tatizo la umeme, sisi tunaona chache sana ila yeye badala ya kutumia na muda wa usiku kusoma na kupumzika yeye anaruka ruka mabarabarani - ukipewa madaraka ya umma lazima ujitoe na ujiheshimu ili hata watu wakuamini kwamba upo nao katika wakati huu wa shida. Baba wa taifa alituonya watanzania kuhusu hili sasa majibu yake ndiyo haya.

Hii hoja ya maisha binafsi tunaitafasiri vibaya ndugu zangu.
 
Hata yeye ni binadamu....ili mradi muda wake wa kujirusha usiathiri utendaji kazi wake.Hukumbuki hata shule kulikuwa na watu walikuwa wanabukua usiku kucha lakini kwenye pepa wanataga? Kila kitu ni discipline ya kile unachofanya.Nakumbuka tukiwa form six kwenye pepa 2 ya chemistry ambayo ilikuwa ya mwisho kulikuwa na Disco kwenye shule ya disco-partner wa shule yetu,pepa ilikuwa jumatatu na Disco lilikuwa usiku jumamosi....hapo ilikuwa mtego kwa wale wapenda mziki.Headmaster wetu akatutisha kwamba hatakataza watu kwenda lakini mtakaoenda mtashangaa matokeo yatakapotoka jinsi mtakavyofeli hii paper.Cha kushangaza watu walienda,waliokomaa class nao walikomaa lakini baada ya matokeo ilikuwa aibu.Walioenda hakuna hata mmoja aliyefeli ile pepa...so kila kitu ni discipline tu.

Kama mtu ni bogus basi atakuwa bogus tu sio shuleni,hata ofisini au kwenye uongozi...DISCIPLINE ! ! !
 
Huyu bwana hana uwezo wa kusaidia lolote kwenye kero ya umeme msameheni bure. Generations and generations will always read and remember the time we have wasted to develop our nation during fourth phase government
 
Narudia kuwakumbusha wanaJF, serikali ya CCM imejiapia na kurudia kuwa mgao huu utakuwa historia, maana yake eleweni hatutakaa tuusahau maishani maana haijawahi kutokea.
Wengi tunaelewa kuwa wanalenga kuondoa, kumbe wanlenga kuuzidisha mpaka tuseme tuiiiiiiiiiii
Tutakoma kulinga hakuna lisilowezekana chini ya jua, zamu yetu kulala gizani na kuzima computer zote kazi zizifanyike.
tayari malipo ya mishahara yanaanza kuletwa kwa utata kupishanisha payroll za vituo na pesa itokayo hazina, sijui nayo computer ya hazina ilizima wakati wa kuprint cheque
Ku><>>((**& zao
 
[
images
183940_199410123421651_100000579932347_667244_995926_n.jpg


......kweli.... si mnaona hapo katoka dancing..... halafu anaenda kulala mbele ya bosi wake..... .j.k mpige kibao huyo aamke alaa
 
Mwacheni Ngellejjah acheze disco sasa kwani kwenye umri wa uvulana hivi vitu alivikosa kwa hiyo lazima a compensate sasa
 
Kuweka contacts za mtu kwenye mtandao bila ridhaa yake ni dalili ya ujinga na upumbavu pia.Nawashangaa mlivyo na akili kama za bata(kusahau),mbona mmewasahau akina Lowassa na Karamagi ambao walihusika ktk richmond scandal?Maisha binafsi ya Ngeleja yaachwe!!Kama ni utendaji Magufuli angepewa wizara zote na cha ajabu anaingiliwaingiliwa kiutendaji,mawaziri wengine ubunifu hawana!
 
Ndio uwezo wao ulipofikia hawawezi tena! Tuwatimue wote, serikali yao imekuwa pango la wanyang'anyi, matapeli, wavivu, walevi ambao hawana kiasi.
 
Back
Top Bottom