Huyu ndio mbunge aliemtaja polisi Kweka kushirikina na wahalifu.

THE CHOICE

Member
Jul 11, 2012
19
1
[h=3][/h]
Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola

Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola kupitia CCM bungeni july 17 2012 amesema polisi wamtafute Fadhili Kweka mwenye mtandao wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi.
Amesema “kuna mtandao mkubwa wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi na ushahidi ninao, wanatoa kwa wahalifu taarifa za wananchi wanaomiliki silaha ili wahalifu wajue wananchi wana uwezo kiasi gani wa kujihami ili waende kufanya uhalifu, IGP unaenisikiliza naomba anza na mtumishi wenu anaitwa Fadhili Kweka anaomtandao wa uhalifu ndani ya jeshi la polisi, hainiingii akilini anapata wapi taarifa za wananchi wanaomiliki silaha alafu anawapa wahalifu, anzeni na huyo na nitawapa ushahidi wa kutosha”
Hiyo ndio kauli ya Mbunge Kangi Lugola ambae alikua akitoa hiyo mistari wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi…. unaweza kumsikiliza zaidi hapo
chini ufahamu yote aliyosema….

 
Mi nilitegemea umwonyeshe Polisi aliyetajwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu!...it could sound much more attractive!
 
Watu kama hawa ndio wanatakiwa hapa Tanzania sio watu wanao ficha ukweli kuhusu yanayotokea.
Tokea ameanza kuchangia alikuwa anaongea kwa uchungu sana
 
Kangi Lugola atakuwa na ushahidi dhidi ya Kweka I believe that.

Kangi Lugola baada ya kumaliza UDSM 1990(?) alijiunga na JESHI LA POLISI. Amefanya kwenye Jeshi la Polisi hadi alipoacha na kuingia SIASA 2010.

Kangi Lugola ni dizaini ya Filikunjombe, sio mbunge mnafiki.
 
Fadhili Kweka ..?

Wakuu, aliye na Photo ya hili gaid aitupie humu ndani basi. Usikute tunalifahamu
 
Hili lina ukweli kabisa hata maeneo yetu ukimilikishwa silaha asubuhi jioni hawa hapa wanaitaka kama sio police hao ni nani?hili jeshi la vipolic ni baya sana sana sijui tufanyaje tukamkamata askari nakuumuua wanakuja kutuambia mtatutambua sie kwetu huishiwi kelele za mwizi
 
Ni kweli kabisa polisi ndiyo waizi number1 ktk matukio yote ya ujambazi yanayotokea. Wao ndiyo wanaotoa taarifa za mtu/mahali patakapovamiwa na wanashirikiana na watu wa nje ya polisi kufanikisha ujambazi huo.
 
Pamoja na umuhimu wa kumtambua huyu ni vyema mtuhumiwa akafahamika. Kumwonyesha aliyetoa taarifa kunahatarisha usalama kwa njia moja au nyingine hasa ukizingatia wimbi lililojitokeza la kuwateka watu na kuwatesa. Mbunge huyu ni makini na anastahili sifa kwa vile anatuonyesha uzalendo alio nao. Hii inadhihirisha uzalendo hauna chama ila ni uungwana wa kuzaliwa nao.
 
Back
Top Bottom