lifeofmshaba
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 867
- 219
Serikali izuie midahalo ya siasa shuleni, vyuoni'
TAASISI ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA) imeishauri Serikali kupiga marufuku midahalo inayochangia kukosekana nidhamu na kusababisha uvunjifu wa amani shuleni na vyuoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya aliliambia gazeti hili ofisini kwake kwamba vipo baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikiingiza siasa mashuleni, hali inayosababisha wanafunzi kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja na kuchangia kiwango cha elimu kushika.
Alisema midahalo ya siasa ambayo imekuwa ikifanyika vyuoni, demokrasia imekuwa ikitumika vibaya kutokana baadhi ya wachangiaji mada na wasikilizaji kutoa kauli zisizostahili kwa viongozi wa nchi.
"Wanafunzi wengi wamekuwa wakichanganywa na siasa ambayo imekuwa ikiingizwa mashuleni na baadhi ya vyama, mwanafunzi anatakiwa apate elimu na shule sio sehemu ya siasa, hali hii imechangia hata kiwango cha ufaulishaji kushuka," alisema Ngawaiya.
Ngawaiya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, alisema pia demokrasia imekuwa ikitumika vibaya, jambo alilodai kuwa nchi za Magharibi zimekuwa zikitumia fursa hiyo kuhakikisha nchi zenye amani zinaingia katika machafuko.
Kauli ya Ngawaiya ililenga kongamano la kujadili katiba lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) wiki iliyopita kujadili Katiba ambapo alisema baadhi ya wachangiaji walitumia vibaya demokrasia.
source habari leo
MY TAKE:huyo thomas ngawayi kalipwa kiasi gani kusema uongo wa wazi namna hii? nani kamwambie elimu ya juu inashushwa na siasa kama sio upungufu wa walimu na na vifaa vya mafunzo kwa vitendo? kwanza hakuna takwimu kwamba elimu ya juu imeshuka nadhani anaongelea shule za kata? na hao wamewai kushiriki midahalo kweli? au ni shule na kata za jk? thomas kama unamuogopa kikwete au wamekutuma basi unaishushia hadhi hiyo taasisi yanu nadhani wakufukuze kazi huna fikra, au kwa sababu ccm walizomewa wanataka midahalo ifanyike manzese