Huyu Mzee ni bora astaafu tu, maana sasa anachemsha

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Kingunge ajitapa kumuenzi Nyerere

na Prisca Nsemwa na Scola Athanas
Tanzania daima

MWANASIASA mkongwe nchini Kingunge Ngombale -Mwiru amewataka wananchi kujihadhari na wanasiasa wa upinzani wanaotumia jina la Mwalimu Nyerere kukichafua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani ni wanafiki.
Aliyasema hayo jana kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, yaliyoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kilichopo Kivukoni, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

"Wanaotumia jina hilo, sera na mipango wanayoitumia ipo kinyume na misingi na kanuni alizoziweka Mwalimu enzi za uhai wake, wakitaka kuichafua CCM ndiyo wanalitumia jina la Mwalimu, hao ni wanafiki, mjihadhari," alisema Kingunge.

Akizungumzia suala la ubinafsi, alieleza kuwa Mwalimu alikuwa mfano wa kutosha kwa kuweza kuishi na wananchi wake bila kuwa mbinafsi, hakutawaliwa na tamaa na wala hakutafuta faida binafsi.

Kingunge alisema Nyerere aliwathamini watu aliokuwa akiwaongoza na ambao alikuwa akiwatumikia, ili kuiletea nchi maendeleo na kulazimika kujitoa kwa kila hali ili kuitoa mikononi mwa wakoloni na alifanikiwa.

Akitoa mfano wa kuonyesha kuwa Mwalimu hakuwa mbinafsi, alisema kuwa alipochangiwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kwenda Umoja wa Mataifa kuwasilisha hoja ya kutaja Tanganyika ijitawale, alirudisha fedha zote zilizobaki ambazo walimchangia, kiasi cha sh 2,000, hatua ambayo iliwashangaza wengi.

"Mwalimu hakuwa mtu wa tamaa alizirudisha hizo fedha kwenye kikao huku akiwaacha watu wakimshangaa na yeye kudai kuwa zile zilibaki kwa hiyo zihifadhiwe kweye mfuko wa chama, hii inadhihirisha kuwa hakuwa na tamaa na angeweza kuzitumia," alisema Kingunge.

Alisema lakini viongozi wachache wanaoyafanya hayo leo, ambapo wananchi wanashuhudia viongozi wakijikusanyia utajiri na kuwaacha wananchi wanaowaongoza katika lindi la umasikini.

"Tunayo mifano ya wakubwa wanaozunguka na mabunda ya mapesa mifukoni na tunao hapa hapa nchini, huu ni ubinafsi," alisisitiza Kingunge.

Alisema kuwa suala la ubinafsi ni tatizo kubwa katika Bara la Afrika ambapo watu wanataka madaraka ili kuweza kuwaongoza watu maskini lakini wanapopata hujinufaisha wao wenyewe zaidi.

Wakati huo huo, wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TNGP) jana walifanya maandamano ya amani maalumu kama sherehe za uzinduiz wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kumuenzi hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Maandamano hayo yaliyoanzia njia panda ya Mabibo jijini Dar es Saalam na kuishia katika viwanja vya ofisi za TGNP, yaliwahusisha wanaharakati waliokuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na ujumbe wa nukuu za kauli zilizowahi kutolewa na Mwalimu Nyerere.

Maandamano hayo yalipokewa na wanaharakati kutoka katika asasi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na TANGO, FORDIA na Haki Ardhi, na walifanya mdahalo ambao ulikuwa ukikumbusha yale ambayo yalikuwa wakisisitizwa na Baba wa Taifa.

Akizungumza katika mdhalo huo, Mkurugenzi wa TGNP, Usu Mallya, alisema kuwa wanaharakati wana kila sababu ya kumuenzi Baba wa Taifa kwani alikuwa ni mwanaharakati mkubwa na alitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa anatetea haki za wananchi wote bila kujali wala kubagua.

Mary Mwingira amabaye ni mwanaharakati kutoka TANGO, alisema wanamkumbuka Mwalimu kwa kuwa katika uongozi wake alisisitiza kuwa ili maendeleo yapatikane, kunahitajika watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

"Tukiangalia sasa katika nchi yetu viongozi wameshindwa kumuenzi Mwalimu kwa kuendeleza kaulimbiu hiyo, kwani watu wapo, ardhi hakuna, wanamiliki wachache wenye fedha na mabepari na nina mashaka kama siasa safi ipo na uongozi bora hakuna, ila kuna bora uongozi," alisema Mwingira.
 
suala sio kingunge kustaafu suala ni huyo/hao waandishi wanaotumia kalamu zao vibaya kuwaremba viongozi ! mtu unaweza ukafall in love na kiongozi hivi hivi literali kwa sababu ya maandishi ya hao wajinga !
 
Hivi walipomfuata kumuomba arudi FISIEM akawagomea hawakuwa wakiyajua hayo? Muulizeni mbiyombiyo mzee alimjibu nini "....hamna adabu"
La kuvunda halina ubani...
Fukueni makaburi yote tuwaoneshe wafu wenu... :D:D:D
 
Jf never bored,haha Jamaa nahisi atakuwa anatamani aifutilie mbali thread hii
 
huu unaitwa unafiki wa kiwango cha standard gauge, kweli tuwe na akiba ya maneno ni muhimu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom