Huyu mwanamke unaweza kuishi nae kweli?

fundiaminy

JF-Expert Member
Jun 4, 2009
355
51
Wanaume wenzangu..kweli kiasi kikubwa cha wachangiaji wanasema kuwa mke nyumbani huwa kisababishi kikubwa kwa wao kutoka nje ya ndoa.
Mke mwenye maneno mengi,mkali,ukifika hom toka dili mapokezi adimu..hakuulizi umeshindaje.usiombe boss akupe overtime.ujiandae kusema wapi umechelewa.
Sasa basi.huyu mama mwenye nyumba ana qualities zote.mapokezi utazani uko kwa small house.mnayajua mapokezi ya aina hio kwani wengi mmeyafagilia..mke kamfumania mumewe na mke wa jirani mara si moja.anachofanya ni kulia weee na kumwambia mumewe nimekusamehe ila usirudie mume wangu.
Mume akichelewa nje wala hatamkosa mkewe kwa nyumba.na wa wala hakuna dalili zozote kuwa mama huyu ana serengeti boy anaemfariji.
Sasa jamaa wasiwasi wake ni kuwa hajui hasira ya mkewe ikilipuka itakuwa vipi..ni sumu ataekewa kwa chakula? Atachomwa maji moto ama kuchomekwa kisu akiwa usingizini?...yani kwa kifupi,jamaa hajawahi kuona mkewe akimkaripia kwa makosa yote atendayo..nawasilisha.
 
anafumaniwa, anasamehewa, then anarudia tena na tena!?
kweli tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili........hata akimwagiwa maji ya moto ni halali yake!
 
kuna mawili

mama anaye anayempoonza machungu yake au hawa ni wale siku vikilipuka anatenganisha mapu****** na mwili
 
Inaonekana mama huyu anamjua mumewe tangu zamani kuwa ni kiwembe na anakubaliana na hali halisi,si jambo la kawaida kumfumania mwenza wako na kuishia kulia tu na mwisho wake kusamehe.
Pia inawezekana mama huyu mapenzi kwa mumewe hayapo tena hivyo hata kile kitu kinachoitwa wivu hakipo na limebaki suala la kutunza watoto tu kama wanao na anapolia analia kwa sababu ya watoto.Kama kutaka kumwadhibu mumewe angekuwa amefanya hivyo mara ya pili alipomfumania maana kama alisamehe mara ya kwanza si rahisi kusamehe tena hasa kwa mtu yule yule.
Mume anatakiwa atubu na kuachana na kumsaliti mkewe na aende kwa wazee akaombe msamaha mbele yao kwa yote aliyoyafanya na hii itampunguzia mashaka ya kuishi na mkewe.
 
Kuna wanawake wako hivyo wameumbwa na roho ya huruma na kusamehe,ila sasa tatizo kale kalugonjwa,mmhh!
 
:A S 13:atakufa usingizini we subiri,hakuna kama kitu anasamehe kila siku,anajipanga.......!!Mungu ambadilishe huyo mwanaume mapema na amrudishie imani kwa mkewe,la sivyo siku atakapomlipa utakuwa mwisho wa kati ya mmoja wao!
 
Huyo mwanamme hana adabu ndiyo maana akafanya takabari namna hiyo lakini iko siku Mungu atamlipa hata bila ya mwanamke kunyanyua mkono wake.

Off topic: by the way Dena Amsi hiyo picha ya mdogo wangu wa kitumbatu umeipata wapi?
 
Dah!
Mimi mwenyewe nikiolewa nitakuwa kama huyo mama.
Adhabu nzuri sana hiyo.
Mwanaume kashashindikana. Bora umpotezee kuliko kuendelea kupiga nae kelele.
 
Ila kweli kuna wanaume ambao wana roho za chuma,hata umbebe,he will never get satisfied!.hapo huyo mwanamke anaeza kua amepoteza matumaini ya kuwa na true happiness,anaishi ili tu siku ziende mbele..mi hii kwangu ni uuaji,kabisa,kwasababu sio lazima mtu akuue kwa risasi,thats internal death!..Mungu amsaidie atambue thamani yake mbele ya Mungu na sio wanadamu..ila kama yuko kwenye harakat ya kisasi then Mungu pia amsaidie asifanye hivyo.
 
hii nimeichukulia kama tafakari tu.wala tusimlaumu huyo mume tu.kwani kuna kisa nathibitisha kuwa mke kamfumania mumewe na wakapelekana kwa wazee wa kijiji..swala lilipotatuliwa wakarudia hali ya kawaida.mume kaamua kutulia kabisa kutokana na aibu aliopata kwa kikao cha wazee.miaka haikusonga mume nae kamfumania mke huyo huyo aliemshtaki kwa wazee.kwa busara mume kaamua kuuchuna kwa kuwa aibu tayari alishaipata..mkewe alisubiri apelelekwe kwa wazee kwa mashtaka ila siku zikawa wiki hadi mwezi wala mume hamgombanizi..alichofanya mkewe ni kutwika mizigo yake na kwenda kwao.sijui ni hofu ama ni guilty feeling wasemavyo wenzetu iliomkimbiza.
 
Aisifiye mvua imemnyea nahisi kama huu msemo unarelate na ishu yako ila usiwe na mawazo hasi kwa mkeo mungu kamuumba hivyo basi mshukuru mungu na wewe jaribu kubadilika kumuenzi mkeo kama ulivyosema amekuvumilia sana na mambo yako mabaya badilika ili na yeye ajisifiye kwamba kweli mvumilivu hula mbivu
 
hii nimeichukulia kama tafakari tu.wala tusimlaumu huyo mume tu.kwani kuna kisa nathibitisha kuwa mke kamfumania mumewe na wakapelekana kwa wazee wa kijiji..swala lilipotatuliwa wakarudia hali ya kawaida.mume kaamua kutulia kabisa kutokana na aibu aliopata kwa kikao cha wazee.miaka haikusonga mume nae kamfumania mke huyo huyo aliemshtaki kwa wazee.kwa busara mume kaamua kuuchuna kwa kuwa aibu tayari alishaipata..mkewe alisubiri apelelekwe kwa wazee kwa mashtaka ila siku zikawa wiki hadi mwezi wala mume hamgombanizi..alichofanya mkewe ni kutwika mizigo yake na kwenda kwao.sijui ni hofu ama ni guilty feeling wasemavyo wenzetu iliomkimbiza.

Mambo haya bora tuwafumaniage tu wanaume zetu linapokuja swala umefumaniwa mke sijui uso utauweka wapi hata kama ulimfumania mumeo mara tano.kaogopa maana wengine wanaua kabisa
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom