huyu mume amekuwa msalaba kwangu

Dada hakuna kitu kibaya kama kuvunja ndoa, inabidi uwe na uhakika asilimia mia kwamba wewe haukusababisha migogoro kwenye nyumba yako. Ningekuwa mimi ni wewe, maadam kutokuelewana kwenu hakujahusisha vipigo, ningekaa chini na mume wangu nimueleze nia yangu ya kutofanya nae mapenzi mpaka hapo atakapotulia na tukapima, ningeishi nae vizuri ila tu mambo ya unyumba ni mpaka atakapobadilika, Hata akirudi asubuhi we mwambie karibu mme wangu wala usigombane kwamwe ugomvi haujengi, ningeishi vizuri na hao watoto wake kwani hiyo ndio sababu ya kujivunia kuwa mama bora, hazina yako ya baadae, furaha yako na baraka zako zote zitapitia hapo. Bado unaweza fanya biashara zako ukiwa na huyo mumeo sasa hivi kwani atakukataza?? Sikushauri kuondoka, do something....
 
kipi bora urudi nyumbani kwenu?au ukupe Ngoma maana huyo ni Hatari kwa maelezo yako.Inatisha.nakuomba kuwa mwangalifu,wewe ni binti mdogo halaf hamwendani Au pesa yake..!!
 
that is for sure!
Kiukweli sie wadada mara nyingine tunajitakia haya mambo, mi nnachojua mara nyingi wewe kama mwanamke ukikubali kua na mume basi ujue ukubali haya yanayotoke. Maana kama aliweza kumuacha mkewe na kukufuta wewe na wewe ukaona ndo umepata basi itabidi ukubali tu zamu yako imepita waachie wengine. Hiyo ndio rule of the game. Maaana mke wa kwanza alikuachia wewe na wewe inabidi umuachie mwenzio wala usoine nyongo bi dada. what comes around goes around
 
nashukuruni kwa ushaur wenu me nlichofikiria nakaa mwaka mmja nijifanye napotezea mtaji wangu wa biashara utoshe niondoke nkaanze maisha yangu!vijana weng wananisumbua na wngne wasiojua nmeolewa nawakataa najiheshmu pamoja na uzur mungu alionipa naombeni muniombee niwe na ujasir wa kufanya maamuz haya magumu

wala usimuache, tumia njia hii: hakikisha kila siku mna-sex bao mbili au zaidi, hapo atakuwa hana hamu na nguvu zitampungua, pia kuwa mtundu kupita kiasi (wild) huenda kuna vitu anakosa kwako, kuna watu wengine wanaogopa kuwa wild ndani ya ndoa, usiogope fanya kila aina ya mauchafu ya mapenzi. Ukifanya hivyo ndani ya miezi 6 halafu akaendelea na tabia hiyo itakuwa ameshindikana.
 
ukisikia mwanaume analala mpaka na housegirl yaani ujue huyo ni proper shetani wa ngono achana nae kabisa atakuja kukuambukiza magonjwa..mkimbie na chukua nusu ya mali yake usepe...mwanaume hayuko mmoja hapa duniani
 
hivi jamani ndoa si inaweza kuvunjwa mahakamani kama kukiwa na evidence partner yuko unfaithful????
take his sorry ass to court,
huko utapewa talaka legally pamoja na nusu ya mali,
sasa hapo ndio uchakarike na hio nusu ya mali,hakikisha unaomba msaada wa wazazi wako na ndugu zako wengine wakusaidie kimawazo hio nusu ya mali izalishe kiasi cha kulisha wanao,
cha muhimu ni UJIAMINI,
 
pole sana binti ila ukiona umechoka kutumika na kuwa mtumwa wa ndoa yako hiyooo....utaamua nini cha kufanya!!!
 
habar wana jf!nawapenda sana kwa ushaur ambao mumekuwa mkiutoa hapa!
mimi ni mwanamke mwny miaka 24 nimeolewa miaka 6 iliyopita!
nina mtoto wa miaka 3
mume wngu ana miaka 48 aliponiowa alikuwa ana mke lakn sikugundua nligundua bda ya mwaka 1 kupita akawa amedanganya kwtu kuwa mkewe walishaachana kumbe ilikuwa uongo na vile alishatoa mahar na tulikuw tunapndana nkaona maisha yaendelee (hapa msipajadili sana nlishakosea)bda ya miaka 3 yule mkewe aliondoka akatelekeza watoto akaolewa na mt mwngne! ikabidi wale watoto wake niwachukue nikawa naish nao nymbani kwangu tulikojenga na huyu baba yao!

kiukwel huyu baba nlianza nae maisha akiwa na pesa m.1 tukawa tunalala chn na kabiashara kadg sa hv ana magar2 nyumba ambavyo amevpata tukiwa pamoja na ofcourse anajal familia na me mwnyewe

kinachnifanya niombe ushauri ni umalaya wa kupindukia alionao mwez wa tan nlisafir kma wki moja kurud nkakuta kamnunulia dada mmoja kitanda na vtu vya ndan ikiwa ni njia ya kumtaka kimapnz bda ya kununua yule dada akamtosa kwan alikuwa na boifrnd mume wangu akamzisha ugomv kudai hvy vit kwa jins nlivyoelezwa
hakuna sket inayompita awe housgirl au rafki yang nimevumilia nimechoka sasa naona imetosha lakini kikubwa sina pa kuanzia naogopa kuwaeleza wazaz wangu kwan wataniambia nirud nyumban hata leo nafikiri maisha ya hawa watoto wake bada ya mimi kuwaacha kwan nimekuwa kma mama yao na msaada kwao.
mume haambiliki na wala hawezbadilika nshaongea nae sana imeshndikana
wana jf naombeni ushaur wa kina nahs kuchanganykiwa
nb!

Hiyo ndiyo tabia yake halisi, kibaya ni kuwa hukuweza kumchunguza toka mwanzo. Inaonekana wazi hata mke mkubwa (wakubwa) alifanyiwa vituko hivyo wakati wewe ukitongozwa na kuolewa na huyo Bwana.

Hutaweza kumrekebisha tabia hiyo, chukuwa hatua kabla hujapata Ukimwi. Usiogope, piga hatua moja mbele ukimtegemea Mungu. Maisha yataendelea tu hata bila huyo Bwana, huishi kwa ajili yake bali unaishi kwa ajili yako mwenyewe. Hakuna cha ajabu wazazi na ndugu zako watakuelewa, vunja ukimya ongea nao utapata msaada utakaokuweka huru.
 
kuna mjumbe mmoja kagusa issue ya kusugua got nadhan ndo njia ya kufanya,jins ulvyojieleza hapa naonesha ua very gud woman na unaweza kubadlisha sura ya ndoa yako.wansema kwamba love has never failed anyone,i dont doubt upendo wako kwa mumeo but love hm more,mi naamin ndoa inapaswa ilindwe kwa gharama zozote,ingawa hili kupata magonjwa ni changamoto kwa hili nashauri hivi kaa na mumeo kwa heshima yote na upendo wote ni mwambia kama anaona humtoshelei basi mkumbushe kutumia mipira,hata hvyo hongera kwa kuwatunza vyema wanao wa kwama,dont leave your husband kwa sababu yeyote ile,tafuta namna yoyote ile ya kumfanya mumeo auno upendo wako and keep on praying inaweekana kabisa kwa hii ndoa kuwa njema kiasi ambacho huwe amin take ths from,kuania leo ana kufanya vitu ambavyo vitamsha upendo wa mumeo,just show more caring,love and respect i assure u i see bright future na ndoa yako dont give up atleast not yet!
 
The Boss hivi kumbe wanawake hua wanang'ang'ania ndoa zao ili wapate matunzo na sio kwa sababu ya mapenzi??na hayo maigizo mwisho wake sio virusi??kazi ipo!:flypig:

wewe hujanielewa kabisaa
hapa nampa option moja kulinganisha na zingine
sijasema hii ndo best option..
 
wewe hujanielewa kabisaa
hapa nampa option moja kulinganisha na zingine
sijasema hii ndo best option..

Mimi nakushauri tangu mwanzo huyu sio mumeo kabisa,kwanza baada ya wewe kugundua kwmba ana mke tena na watoto ulitakiwa kuvunja hiyo ndoa batili,hakuna sababu yeyote ya eti unawaonea huruma watoto wa huyo mumeo,kwa kuwa mke wake yupo hai wewe hauna tofauti na hawara tu,japo uliolewa kwa kwa mbwembwe zote,na nakwambia japo huyo mke wa kwanza yaani mke mwenzako unasema kaolewa kwingine bado tu ni mke kwa huyu ulienae sasa.
Vilevile huko alikoolewa hana tofauti na wewe kwani wote wazinzi,sasa shosti achana na huyu mwanaume sio mumeo,badilika ukimwi unautafuta chukua mwnao wanaume singo wapo,wazazi watasemaje onesha msimamo wako.
Na lingine hakikisha unapata matunzo hata mali kidogo kwa ajili ya maisha yako,shtuka atakuzeesha huyo.
 
wewe hujanielewa kabisaa
hapa nampa option moja kulinganisha na zingine
sijasema hii ndo best option..

Mimi nakushauri tangu mwanzo huyu sio mumeo kabisa,kwanza baada ya wewe kugundua kwmba ana mke tena na watoto ulitakiwa kuvunja hiyo ndoa batili,hakuna sababu yeyote ya eti unawaonea huruma watoto wa huyo mumeo,kwa kuwa mke wake yupo hai wewe hauna tofauti na hawara tu,japo uliolewa kwa kwa mbwembwe zote,na nakwambia japo huyo mke wa kwanza yaani mke mwenzako unasema kaolewa kwingine bado tu ni mke kwa huyu ulienae sasa.
Vilevile huko alikoolewa hana tofauti na wewe kwani wote wazinzi,sasa shosti achana na huyu mwanaume sio mumeo,badilika ukimwi unautafuta chukua mwnao wanaume singo wapo,wazazi watasemaje onesha msimamo wako.
Na lingine hakikisha unapata matunzo hata mali kidogo kwa ajili ya maisha yako,shtuka atakuzeesha huyo.
 
Kiukweli sie wadada mara nyingine tunajitakia haya mambo, mi nnachojua mara nyingi wewe kama mwanamke ukikubali kua na mume basi ujue ukubali haya yanayotoke. Maana kama aliweza kumuacha mkewe na kukufuta wewe na wewe ukaona ndo umepata basi itabidi ukubali tu zamu yako imepita waachie wengine. Hiyo ndio rule of the game. Maaana mke wa kwanza alikuachia wewe na wewe inabidi umuachie mwenzio wala usoine nyongo bi dada. what comes around goes around[/QUOTE
YEYE ALICHUKUA MUME WA MTU,ALITEGEMEA NINI?MALIPO YAKE NA YEYE ANACHUKULIWA!WAKATI MWANAUME ANAACHA MKE YEYE AKAWAPROMOTED KUTOKA HAWARA KUWA MKE,LAZIMA ANA MAHAWARA WENGINE AMBAO SASA YEYE KAMCHOKA ANATAKA MKE MWINGINE!MALIPO NI DUNIANI AKHERA KUHESABIWA!TUBU KWA MUNGU WAKO AKUSAMEHE!
 
Mwenye kuijua atakuwa milionea for sure..lol
iko in demand kwa kweli...lol
mimi nasikia tu

Haaahaaaa! Nimeisikia sikia kwa waganga wa jadi...wanainadi kwa kusema kwamba ukitaka kumvuta unayempenda. Nisichojua hiyo dawa kama inaweza pia kumfanya zezeta.
 
Hakuna utakachopata tofauti na hicho cha huo mume wako. Mweke sawa na wewe ujujali unaonyesha una hamu ya umalaya tuu take care.
 
Utakuwa si wa kwanza kumkimbia mme we achana nae kamata mgumu
 
Haaahaaaa! Nimeisikia sikia kwa waganga wa jadi...wanainadi kwa kusema kwamba ukitaka kumvuta unayempenda. Nisichojua hiyo dawa kama inaweza pia kumfanya zezeta.

mi nishaona wake za waganga wa jadi 'micharuko'
sasa hapo go figure lol
 
Back
Top Bottom