Huyu Mpumbavu anaweza akasababisha maafa makubwa sana

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
<TABLE cellSpacing=0 cellPadding=0 width="100%" border=0><TBODY><TR><TD vAlign=top align=middle>
06_10_w9h4u7.jpg
</TD></TR><TR><TD class=kaziBody vAlign=top align=left>Kijana huyu akihatarisha maisha yake kwa kukinga mafuta kutoka kwenye tenki la gari hili likiwa linatembea katika barabara ya Nyerere Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).</TD></TR></TBODY></TABLE>
 
hayo ni mabaki ya mafuta, hilo tank limetoka mkoani/congo/zambia/malawi etc na linakuja Dar kujaza mafuta, hivyo kwenye tank huwa kuna mafuta mabaki kidogo sana NDIO MAANA HATA MADEREVA huwa wanawaruhusu tu na wanawaacha tu wafanya wanachofanya kwasababu hapo wanakuwa wako safarini kwenda kujaza mafuta. ukisimama pale ubungoubungo ni kitu cha kawaida,madereva wanawaona, wanawaacha tu etc.

HOWEVER, ni hatari sana na inatakiwa kukemewa kwasababu mafuta kidogo tu yakilipuka kama ndo mko pale kwenye foleni mataa ya ubungoubungo walioko kwenye foleni wote inakuwa mshikemshike. hii kitu inafanyika sana pale mataa ya ubungoubungo.
 
Huu mchezo hawa vijana wameshauzoea na wakati mwingine wananyonya mafuta askari wa barabarani wapo wanawaangalia tu. madereva na makondakta wao pia wanawaona hawakemei. barabara ya mandela ndio hasa kunakofanyika mchezo huu maeneo ya buguruni. siku ikitokea maafa (mungu aepushe) sijui itakuwaje na msongamano wetu huu wa barabarani.
 
Huu mchezo hawa vijana wameshauzoea na wakati mwingine wananyonya mafuta askari wa barabarani wapo wanawaangalia tu. madereva na makondakta wao pia wanawaona hawakemei. barabara ya mandela ndio hasa kunakofanyika mchezo huu maeneo ya buguruni. siku ikitokea maafa (mungu aepushe) sijui itakuwaje na msongamano wetu huu wa barabarani.

mwenye jukumu la kuwazuia si dereva wala konda, aidha hata uwezo wa kuwazuia hawana. jiulize ni wewe ukiwa barabarani kwenye foleni hawa watu wanaparamia gari lako na mifuko ya rambo utafanya nini??, hata ukisimama na kuwafukuza , ikiwa upo kwenye foleni uingiapo ndani ya gari bado watasogelea na kuendelea na wanachokifanya. chaajabu wanapofanya hivyo wanakuwa hata hawana ukahika na aina ya mafuta yaliyomo ndani. ni jambo la hatari sana ki usalama , pia hata kwa ubora wa mafuta kwani mwisho hayo mafuta wanayokusanya kwa rambo huishia kuchanganywa na na kutumiwa kwenye vyombo vya watu

dola ndiyo yenye jukumu la mwisho la kuwalinda wazalishaji , walipa kodi na wananchi kwa ujumla. hivyo kwa lugha ya kawaida , jiji wanatakiwa walione hili tatizo, kwa kushirikia na na vyombo vingine kama polisi na hatimaye kuweka utaratibu wa kuzuia haya mambo.
 
pia hata kwa ubora wa mafuta kwani mwisho hayo mafuta wanayokusanya kwa rambo huishia kuchanganywa na na kutumiwa kwenye vyombo vya watu

washangae wanaonunua mafuta ya kwenye rambo!!!!
nafahamu wanunuaji wa mafuta hayo ni wenye pikapu za kubeba mizigo, zile zilochoka mbaya!!
Na bongo kukishakuwa na mnunuaji, basi biashara haiwezi kwisha hiyo!!
 
washangae wanaonunua mafuta ya kwenye rambo!!!!
nafahamu wanunuaji wa mafuta hayo ni wenye pikapu za kubeba mizigo, zile zilochoka mbaya!!
Na bongo kukishakuwa na mnunuaji, basi biashara haiwezi kwisha hiyo!!
...Unanikumbusha biashara ya machangu doa kinondoni enzi za Yusufu Makamba akiwa Mkuu wa mkoa walimwambia mzee nenda ukalae tu hii biashara haiwezi kufa maana wateja wapo wengi tena wengine ni vibosile kabisa...!! Maisha bora kwa kila Mtanzania.:hail::hail::hail::hungry:

 
Kaaazi kwelikweli, maana hata kule Arabuni wapo hawa, ngoja tuone Lukuwi aah Lukuvi baada ya Ardhi Kinondoni atahamia huku labda!!!
 
Hawa wasinge hatarisha maisha yao namna hii kama wasingekuwa na wateja (wapenda dezo) tayari tayari
 
Ubungoubungo:picha iyo uwa naipenda sana (ambayo ni avatar yako)

ila maisha ndo yanafanya mtu ufanye vitu kama ivi ili uishi,kuliko kuwa jambazi!!
ss wafenyeje?maisha ni kasheshe jamani
 
Mungu wangu!
Wengine tunasema safety is our number one value wenzetu .....:embarrassed:
 
Watu washasahau yaliotokea Mbeya(njia ya kwenda Tukuu) miaka ile

Kama sijakosea eneo lenyewe lilikuwa linaitwa Kijiji cha Edweli, na mwaka jana tukio kama hilo lilijirudia Kenya...utafutaji riziki wa namna hii ni hatari si wa kuchekewa hata kidogo.
 
Ni hatari sana lakini hapa bongo ni kama imehalalishwa vile, kuna siku nilishuhudia jamaa akijichukulia mafuta kwa staili hiyo hiyo huku nyuma ya hilo lori kuna gari ya polisi ambao walikuwa wakimwangalia na kucheka tu.
 
Tusiwalaumu sana wapo katika kutafuta riziki zao.

Mkuu X-PASTER lakini kutafuta riziki yake kunaweza kabisa kusababisha maafa makubwa kwa mamia kama siyo maelfu ya Watanzania. Fikiria jinsi Dar kulivyo na foleni kubwa za magari halafu hili gari lilipuke na huku lina mzigo mkubwa wa mafuta si kitakuwa kilio cha kusaga meno? Si vibaya kutafuta riziki lakini tufanye hivyo katika njia ambazo hazihatarishi maisha ya Watanzania wenzetu.
 
Back
Top Bottom