Huyu mpenzi wangu simuelewi

Mungu akishakupa akili kamaliza,mnataka kumuhusisha na ukuadi.tumia akili alizokupa kupembua.
 
Polee Sana bidada hata huyo wa pili hamna kitu hapo. Hizo Gia tu za kutaka hapo kweny mti wa katikati.
 
Naomba msaada wa ushauri hasa wanaume.

Nilianza kuwasiliana boyfriend huyu kwa njia ya simu mwaka 2014 mwanzoni ambapo wote tulikuwa hatujuani tukawa tunapendana sana tumeendelea na mapenzi yetu ya simu hadi kufikia mwaka jana 2015 Decemba ambapo nilifanikiwa kusafiri hadi hapo alipo na tukajuana tukakumbatiana sana na kukakutanisha na miili yetu ambapo nililala kwake siku mbili.

Cha kushangaza nilidhani tulivyoonana ndo ingekuwa muda mzuri kwa mimi na yeye kupanga mikakati ya mahusiano yetu lakini haikuwa kama nilivyodhania. Alikaa kimya na kunisindikiza kwenda kupanda gari kurudi kwetu Njombe yeye akiwa Dar es Salaam.

Nilipata safari ya pili kwenda Dar nilifikia kwake na nikalal siku moja na kurudi kwetu bila mipango yoyote juu ya mahusiano yetu.Sasa nikwamba tunawasiliana kama mtu na mpenzi wake kwa miaka miwili sasa lakini haoneshi mwelekeo wowote wa kuwa ananihitaji in future na wala hasemi chochote na kila nikisema nataka kumuacha huwa hakubali.

Siku za karibuni nimepata mwanaume yuko serious kabisaaa anataka kunioasasa naogopa kumkubalia wakati sijajua hatima ya yule wa Dar ambaye hasemi chochote.Naomba kwa mlionielewa mnisaidie mawazo hapo nimpige chini huyo wa zamani nimkubali mpya mwenye nia na mimi au niwe mwaminifu hadi aniache huyo wa Dar?

Nawaza nakosa majibu tafadhali msaada

Wanaume wa Dar huwa hawaoi wanakula tu. Utasubiri sana dada yangu nani amuoe mtu kutoka Njombe? Olewa tu na huyo aliye serious
 
kuna possibilities zifuatazo;
i) huyo mpenzio anaweza kuwa na asili ya ukimya uliopitiliza hivyo hata hajui cha kuongea au anaona kawaida tu..cha kufanya we jiongeze muulize una mpango gani na mimi
ii) huenda ana mtu mwingine hivyo kwako anakutumia kama starehe tu anashindwa kutoa kauli ya moja kwa moja kuhusu future yenu aidha anampenda alienae hivyo anakutumia tu.. cha kufanya mpeleleze jaribu kuwajua rafiki zake wa karibu na pata ukweli toka kwao, mchunguze ujue kama kwake unaenda wewe tu au usipokuwapo anaenda na mwingine.
iii) kuhusu huyo mkaka anaetaka kukuoa usimpe jibu la moja kwa moja kama YES au NO ila kuwa nae karibu ili asitoweke mazima msubirishe mda unakuwa unazidi kumbana zaidi huyo mpenzi wako juu ya mpango wake kwako...cha kufanya mpe mda hata miezi miwili huyo mpenzi wako mbane akutambukishe kwao ukiona anajiumauma ndani ya miezi miwili hamna dalili yote ya matumaini mkimbie mara moja mkubalie huyo mwenye malengo ya kukuoa.
 
Wewe unapenda Dar sio mwanaume. Kama unapenda kweli na umekutananae na amepiga kimya basi ujue huyo ni machinga, kariakoo wamefukuzwa kaishiwa na swaga, olewa hukohuko Njombe.
 
kimya kingi kina mshindo!!
huwezi jua anakuwazia nini ,waweza mjudge vibaya kumbe hana nia mbaya pia si msemaji, au pia wewe huonyeshi kuhitaji zaidi ndoa wala kusema/ wanaume wengine mpaka wasukumwe ndo watoe la moyoni!
au pengine hana nia na wewe pia
.
ushauri ni kwamba huyo muoaji mwambie aje na mahari ,akitoa piga chini wa Dar
maana usije kuacha mbachao kwa msala upitao

labda mshikaji nae sound tu....
 
Miaka 2 bado hakuna jipya dada unatumika,
Fimbo ya mbali haiui nyoka huyo wa karibu alieonyesha nia mpe nafasi japo kwa kuanzia usiingie mzima mzima Anza kwa kumchunguza.


Ila mkuu Njombe mpaka dar unafuata dyudyu tu
watu wanatoka kigoma itakuwa njombe chezea ukuni wewe
 
Tatizo ulicheza mechi chini ya kiwango, naona anazidi kukupa muda kama kiwango kitapanda akupandishe kwenye kikosi cha kwanza, jitahidi uboreshe kiwango chako cha uchezaji.
asisahau kulamba dyudyu au
mkuu muelekeze hivyo viwango afudhu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom