Huyu mkaka mbona simuelewi??? nisaidieni mawazo wanajf

habari zenu wapendwa, kuna kaka mmoja alinipigia sim lakini akawa amekosea namba baada ya kujua kua kakosea akaniomba samahani nami nikaendelea na zangu, kilichonishangaza alinipigia tena na kunambia kuwa kavutiwa na sauti yangu hivyo kanipenda vyovyote nilivyo na lengo lake ni kuoana, sikumpa jibu rasmi ikawa tunaendelea kuwasiliana akaomba aongee na mama nikamkubalia sasa alipoongea nae akajitambulisha kuwa mimi ni mpenzi wake anataka kuja ili wajuwane, basi akafahamishwa mpaka nyumbani akaja akakaribishwa vizuri, sasa baada ya kuondoka akanitumia sms na kusema kuwa kazidi kuchanganyikiwa anaomba nisimtose nimkubalie tu ili aniowe, swali lipo hapa huyu jamaa hajawahi kunihuduia hata sent zaidi ya vocha nimaneno matupu hivi nikweli ana mapenzi yakweli? nisaidieni jamani nisijejuta kwa uamuzi nitakaotoa.
Kwa akili yako unafikiri mwenye mapenzi ya dhati mpaka akuhonge shopping au vogue?
Umeanza vizuri lakini mwishoni umeharibu na nimekuona wewe ni demu wa aina gani tayari, pole utaendelea kukaa nyumbani ukisubiri mapedeshee watoke kwenye kumbi za burudani labda watakuona.
 
Mpe zigo nae akupe visenti vya vocha.
Naunga mkono hoja asilimia mia, huwezi kuombwa uchumba ukamfanya kijana wa watu baba mzazi eti akuhudumie kwanza kwa kuwa huna mtu wa kukuhudumia, na yeye akiomba mzigo kwanza kwa kuwa hana mtu wa kumpa, atasemaje?
 
Dah.... Dada una spidi! Mie mbona huyu laaziz hajawahi kunipa hata senti lakini sina wasiwasi.. Maadam nina imani ananipenda wala sibabaiki.. Kinachokupa shaka ni hayo mazingira mliyofahamiana ndio maana unajiuliza kama anakupenda kweli au Lah!
 
kumbe hapa si pakuomba ushauri yani mtu anaona kakamilika anasahau kama anandugu au watoto kama mimi, mmmmmh!!! kaka zangu na dada zangu angalau tujifunze ustaarab, umri wangu ni miaka 21 tu sijakomaa vizuri msinipe maneno makali kiasi hicho
 
Pole sana! Kumbe una miaka 21, ok kwa sasa usiwaze ndoa sababu ujakomaa! Ila ushauri uliopewa si mbaya ukajua kuwa pesa si chochote kama hana mapenzi ya kweli na wewe! Mchunguze kwanza huyo jamaa usiwaze pesa!

kumbe hapa si pakuomba ushauri yani mtu anaona kakamilika anasahau kama anandugu au watoto kama mimi, mmmmmh!!! kaka zangu na dada zangu angalau tujifunze ustaarab, umri wangu ni miaka 21 tu sijakomaa vizuri msinipe maneno makali kiasi hicho
 
kumbe hapa si pakuomba ushauri yani mtu anaona kakamilika anasahau kama anandugu au watoto kama mimi, mmmmmh!!! kaka zangu na dada zangu angalau tujifunze ustaarab, umri wangu ni miaka 21 tu sijakomaa vizuri msinipe maneno makali kiasi hicho

Ushauri wangu ni kwamba usiombe ushauri wa jambo nyeti kwa watu usiowajua vizuri.

Wengine wachuuzi wa maneno na mabazazi.
 
Mh amina ali...jina lako linanikumbusha Amina Ally mmoja nilisoma naye O'level Kilimanjaro huko miaka hiyo..cjui ndo wewe!
eniwei, ushauri wa kukusaidia sina labda nikusaidie kuchagua gauni la harusi!!

ha ha ha ha yaani na harusi umeshapanga mwenzako anahisi hatapata vijisent vya kutosha wewe umeshakimbilia harusi, binti bado hajajielewa bado kinaweza kunuka wakati wowote, so hilo gauni lisubiri kwanza la sivyo anaweza kufunga na mgomba ili atoe mkosi ohooo shauri yako.
 
dada zetu pia waache unafiki kabisaaaaa huyo dada ameyatoa ya moyoni na amewakilisha kundi kubwa sana la wanawake wa siku hizi watu mnatoa ushauri ila najua kabisa moyoni mko tofauti ebu mjiangalie nyie wakati mnaolewa au mko kwenye mahusiano sasa hivi ukweli mnaangalia wapi zaidi ya mifukoni mwetu??? hili halina ubishi kabisa. hata mabinti wakienda kuongea na mama zao kuwa nimepata rafiki wa kiume swali la kwanza kwa mama anafanya kazi gani, akisema ni dereva daladala mama anaguna kidogo ila akisema ni finance manager or loan officer utasikia mama anasema wow hongera mwanangu halafu swali la pili ambalo ndilo lilitakiwa liwe la msingi anauliza ni wawapi na familia gani na mlikutana nae wapi? hapa anauliza baada ya kuridhika na swali la kwanza. wazazi nao wanachangia haya mambo kabisa. wanawake ukweli mnajua wenyewe hili msibishe ni wachache sana nahisi out of 10 ni only 2 wenye mapenzi ya kweli bila kuangalia pesa au kazi anayofanya. muosha maiti hata kama ni handsome vip na awe anakupenda vibaya wewe dada sidhani kama utamkubali na uzuri wako na hiyo kazi yako ya maana zaidi atamtafuta anaendana nae. wanaume kazi tunayo.
 
haya maisha ya nakupenda nyingiiii!!! nataka tuwepamoja mpaka kufa kwetu kila siku kubembeleza asitoswe, lakini hakuna msaada wowote wa kimaisha kutoka kwake

ulishatishia kumtosa nini, mbona anaogopa sana kutoswa? halafu hapo kwenye msaada wa kimaisha, uko tayari kuzingatia vigezo na masharti?
 
Back
Top Bottom