Huyu Mdada Anateseka!...Kuna Namna Ya Kumsaidia...

KAMA NI KWELI................
1.Mme na mke kuvumiliana ni muhimu.Swala la ngono nje ya ndoa ufumbuzi wake ni talaka,Kama ana uthibitisho kuwa mmewe ana mtu nje,hana haja ya kuendelea kuvumilia.
2.Mwambie arudi kwao kama hana ndugu aende kwa marafiki au schoolmate,office mate wanaosali pamoja nk
3.Njaa haivumiliki,mwambie aachane nae.Akili yangu inaniambia kuwa asipoangalia atauawa aidha na mmewe au na hawara ya mumewe.
4.Kama amekosa kabisa cha kufanya,basi amtafute kijana,ampe pesa kidogo tu,halafu ampe kazi ya kumfuatilia mumewe,akijua yupo wapi,mchezo unakuwa rahisi awachukue watoto wote kama saa 3 hivi usiku aende akamkabidhi wanawe,ikiwezekana apitie kwa mjumbe wa nyumba kumi.
5.Aaache kabisa hasira na kulia,hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu.atulie,amwombe Mungu atampa suluhisho sahihi.
6.Aaanze biashara yoyote,kwa jinsi ilivyo,akimwelezea mtu yoyote,anaweza pata pesa japo kidogo za kuanzia kabiashara.
7.Mwambie kuna kitu kinandelea nje ya ndoa yake,lakini haya mambo ni temporary,kuna wakati atastuka na kurudi kwake.
8.Kwa sasa afute kabisa kichwani kama ana mme,hii itamsaidia kuendesha maisha.
9.Mweleze pia asisahau kuvaa zile condomu za kike,akizivaa kama zinavyotakiwa mumewe hatajua kuwa kamvalia condom
10.Anaweza kwenda pia ustawi wa jamii akaeleze kuwa,mumewe hampatii yeye na wanawe haki zao za msingi.
11.Mmewe huyo keshapaikana lakini bado anaakili yake,ndio maana alikumbuka kuja kumtoa hospitali japo baada ya siku tano.
12.Nadhani bado anampenda mkewe asingempenda angeshamfukuza siku nyingi tu,ngoja aibiweibiwe huko nje atarudi tu pesa zikiisha.
13.Asiende kwa mganga, ANAWEZA akajikuta yupo kwa mganga yuleyule mganga wa mwizi wake?yaani mganga wa adui yake ni hapo sasa atakapogeuzwa nyau.Elewa kuwa mwizi wake kama yupo anammonitor yeye kila siku anafanya nini,hakuna mwanamke anaetembea na mme wa mtu asijue data za mke wa huyo jamaa,hivyo huyo mama mfano akienda kwa mganga akatoa sh 30,000 hivi mfano,yule mwizi/mke mwenzie anaweza kwenda pale pale akatoa sh 60,000/ unasemaje hapo?kwa nini kibao kisigeuzwe
14.Baada ya kukupa dawa utasikia mganga akisena'' nenda salama mganga ni mungu,au tuombe Mungu''hii inaonyesha kuwa hata yeye mganga anategemea Mungu.....kwanini usimwombe wewe Mungu wako moja kwa moja?.Au hujui kuomba?...Jifundishe..
15.Binafsi nilishaomba mambo mengi tu na hapo hapo napata nikitakacho...pasipo kukosa. wakati mwingine kabla hata ya kusema AMINA.NAJIBIWA NA KUPATA NITAKACHO.
Mwisho kwa wanaume na wanawake wote wa hapa JF TUWENI NA HURUMA jamani, unakaa/kumzuia mpenzio hata chakula asipeleke kwake? oooooh NO. hata mambo yenu hayawezi kufanikiwa kabisa.

VERY COMPREHENSIVE!
Sheria, ustawi wa jamii na ushauri nasaha, Kalumanzila, Mungu mHH ... MRADI NI MSETO WA AINA YAKE.
Tall uko Juu kwa kweli ...
 
Mhh Fidel!
Kulishwa limbwata siyo hoja..kwani alishikwa pua afungue mdomo alishwe kwa nguvu?
Huu ni ulimbukeni haswa ... Iweje wewe mwanaume mwenye akili timamu... unajua una familia ukaamua kuwa na mpenzi wa pembeni ujisahau namna hii? Kwani jamani mkiwa na hao wapenzi wenu wa nje akili inahama? Si bado mnakuwa na akili zenu? Ingekuwa akili zinahama basi mngekuwa mnasahau hata kuvaa nguo na hapo tungejua kweli kuwa love can make u go crazy.Ni wazi kwamba akili bado zinakuwepo.Kwanini ushindwe kutanabahi kuwa hilo penzi la nje ni kitu cha muda cha kupita kama ulivyomzuzukia mkeo hadi ukamuoa, hata huyu kimada wako utakuja kumuona wa kawaida tu.Kabla hujajiingiza kwa nyumba ndogo jipige interview wewe na roho yako ujue kama una ubavu wa kubakiza akili zako intact.

Kwa mdada unayewakiliswha na boflo, elewa kuwa waume wengi wana roho ndogo sana ya kushinda majaribu.The good thing is wengi hata kama wana vimada, hustahi na kuheshimu familia zao kwa kuzijali kwa kila hali ikiwa ni pamoja na mahitaji - shule, chakula, mavazi, ugonjwa nk.Huyu wa kwako inaelekea alikuwa mbaya tangia akikuchumbia na ulidhani utambadili uingiapo ndani ya nyumba ya ndoa.Hilo lilikuwa kosa. Maadam ulishakosea toka mwanzo, ujue hilo ni zigo lako utalibeba na kuhangaika nalo labda ulitue. Sasa ni wewe tu uamue unataka kulitua lini na kwa style gani.
Pole sana mpenzi!
Na akishalitua wengine walipokee kwa furaha
 
Libwata siku hizi dili mama,
Mtu anamlisha mwanaume kwa matakwa yake binafsi na akili za mwanaume zinahamia kwa huyo kimada.
Nina jamaa zangu kadhaa walilishwa hii kitu ikabidi tufanye kazi ya ziada kwenda kwenye kamati za ufundi sasa hivi wanafrahia maisha yao.
We noma mkuu .... big up sana kwa info hizo
 
Back
Top Bottom