Huyu mbunge, mh!

Mmh, mi nilipita tu, naogopa kuchangia maana wenyewe wakikusikia kesho asubuhi wanakuja kuangusha kipigo mtaani kwenu.

Hii kali kwelikweli!
 
Mzee usogope kiingilio itakuwa bure mradi utafute pa kuiweka roho yako na ukienda kwenye mechi ugawe urithhi kabisa. Safi sana nimecheka
 
Me ninaona ni jambo la msingi kwa sababu siku ikitokea vita hawataweza kupigana,
vita vya kirafiki vinaongeza mazoez
 
Dah, wakuu mnahatarisha hali ya nchi!! Kuna mtu ana note User I'd zenu, soon mtajaopolewa mlipo.
Ni hayo tu
 
Huyu mbunge amechoshwa....ajaribu pia kupendekeza kuuzwa kwa nchi kila raia apewe chake atafute sehemu ya kukimbilia au aishi hapa kama mkimbizi...hiyo nayo imekaage?
 
Kwani kuwakodisha lazima iwe kupigana??Twaweza kuwakodisha hata kutishia kwenye shughuli za kumzuia BESIGYE asitembee kwa miguu kwenda kazini!! Au kuwa walinzi wa makampuni nyakati za night....Hivi kwanini pia wasilinde nyumba za viongozi wakawapa nafasi wenzao FFU nao wakapumua kidogo??
 
Huyu mbunge hatari sana! Kumbuka kuwa na jeshi lenye zana nzuri ni sawa na bima. Ukipata shida unanufaika, usipopata shida ni ahueni!
 
ebwana nimependa wazo lako nakushauri tuwasiliane ili tuandae hiyo proposal tuiwasilishe kwa mkuu wa nchi
 
[Mh. Madam speaker, kwa kuwa serikali yetu inaajiri wanajeshi kila mwaka, na kwa kuwa hakuna kitu wafanyacho zaidi ya kula na kukimbizana na raia. Na kwa kuwa serikali yetu inanunua silaha kila mwaka na silaha hizo hazitumiki ipasavyo na kwa wakati na hatimaye kuharibika na kudhuru raia kama ilivyotokea Mbagala na G'mboto. Je serikali haioni umuhimu wa kukodisha wanajesh wetu ili tupate nyongeza ya pato la kigeni? Na je, serikali haioni umuhimu wa kuomba vita vya kirafiki na jirani zetu ili kuchangamsha wanajeshi wetu na kutumia silaha ili zisilipuke ovyo]

Mhe Mbunge hapo penye kula na kukimbizana na raia, ongeza kulewa na kucheza gwaride! Hofu yangu ni kwamaba mabomu yenyewe na wao wanayasikia yakilipuka G'Mboto na Mbagala ukiwapeleka vitani unategemea nini kama sio kuchanja mbuga na kulala mbele?
 
Mbunge huyu atakuwa alilala kama kawaida yao, alipokurupuka ndo akaja na kioja hiki.
 
Back
Top Bottom