Huyu kaka jamani~~~ Nimjibuje mie!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Leo naomba kueleza lililo moyoni mwangu, wallahi sitanii, maana najua hapa watu watakuja na vijineno vya kukatisha tamaa~~~~Mabibi na Mabwana naomba saaana jambo hili msilifanyie dhihaka.

Ni hivi, kuna kijana mmoja kahamia huku visiwani Zenji mwaka jana mwishoni. Huyu kijana anaishi mtaa wa pili kutoka hapa nyumbani. Mara nyingi akienda kupunga upepo ufukweni huwa anapita hapa kwetu na hapiti bila kutusalimu, kwani kijana mwenyewe ana heshima kweli na aonekana kuwa amefunzwa huko kwao. Hivi karibuni nilipokuwa huko Dar, kula mwaka mpya alikumpa rafiki yangu kadi aniletee ya kunitakia heri ya mwaka mpya na niporudi na kupewa kadi hiyo nilimpa ahsante wakati anapita hapa kwetu. alifurahi sana.

Sasa juzi nimekutana naye Hoteli moja ya ufukweni nikiwa na dada yangu na tulipata wasaa wa kuzungumza kidogo na hapo ndipo aliposema yaliyo moyoni mwake kuwa ananipenda na angependa tuwe wapenzi. Nimemwahidi nitamjibu. Kusema ukweli ni kijana mzuri kwa sura na nimtanashati hasa na mwenye heshma kwa wakubwa na wadogo. Lakini kuna tatizo. Tatizo lenyewe ni kwamba, huyu bwana ni mfupi mno, yaani tukisimama ananifika kiunoni (Mie ni mwembamba na mrefu kiasi)~~~~~ Mwenzenu mie na wanaume wafupi~~~ akha! Hilo kwa kweli limeniwia gumu kukubali ombi lake, maana hata kutembea naye barabarani mwenzenu sitaweza.....

Sasa naomba msaada mwenzenu, nitumie msamiati gani kumkatalia, maana sipendi nimuumize moyo wake.
 
Zinduna weye Zinduna we..
 
Mpe laivu...hauko interested na yeye. mchezo umeisha. ataumia na siku chache baadae ataona mdada mwingine na kukusahau.
 
Kwanı kwa sasa hıvı upo sıngle? Maana kama una mtu mwıngıne ınakuwa rahısı kutoa jıbu kwamba una mtu tayarı.
 
acha kumpotezea muda. Ulitakiwa umjibu palepale but unampa hope ili hali ukijua humtaki. Come on act like a lady.
 
Acha nyodo mtoto wa kike kulikua na wenzako kama wewe hoo nataka mwanamme handsome oh awe mrefu at the end wameolewa na vibabu na mvi tii,usimkatae kwa kua mfupi sema wewe bado mtoto ukishafikisha 29 au 30 utawatafuta hata kina mwala na utawakosa mwishowe utakuja kuishia kwa kina emoro,grow up acha utoto,kama haumtaki sema tu simtaki usije ukasema kisa mfupi au ni promo tujue kwamba wewe ni mwembamba na mrefu?
 
mdanganye una mtu,akija kuja huna atajua tu humtaki,afu hivyo visalam vyake visikuzingue...inawezekana kwa vile ana 'interest' kwako ndio ana play hivyo....ukute ni lilevi kupindukia lol
 
ila wanamme wafupi wanapenda kama wana kichaa, hata uwafanye bushoke wapo tu.
Wana raha yao nao.

Ila kwa wewe umeshasema 'Khah' mwambie ivo ivo.
 
Kama unapenda wanaume warefu nikupe kakaangu.. Tena ukizingatia twatoka pamoja ati.. And kuhusu huyo kaka mwambie ukweli usijeku mpotezea muda!
 
Ila akidoda na kufikia desperate age atapata muda wa kuomba ushauri na sala zetu hadi tutakoma! Wakati huo hata wafupi-decent hakuna, na wala unga na wala urojo tena serengeti boy wanaotaka kulelewa!
achana nae, hakufai

ukipenda kweli, hata muda wa kuomba ushauri unakua haupo :nerd:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom