Huyu jamaa anaakili sawa kweli?

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Huyu Kijana ni fundi ujenzi, anasimamia project yangu moja ya nyumba, sasa jana nimefika home nikakuta yuko nyumbani na mke wake, eti kaja kuniaga amepata safari ya ghafla anakwenda Mwanza kuna tatizo la kifamilia kwa hiyo anaomba niwe napita nyumbani kumjulia hali mkewe hasa ukizingatia hajaacha pesa ya kutosha nyumbani.

Nikamuambia kwa nini asiende na mke wake nitamuadvance hata pesa, akanambia kinachompeleka huko ni issue ya mke wake wa kwanza (ndo najua sasa kama alikuwa na mke mwingine huko Mwanza), nikamuambia basi nampa pesa aache nyumbani sababu siwezi kuguarantee kwamba ntafika nyumbani kwake sababu niko busy sana, akang'ang'ania oooh ndugu yangu nisaidie bwana uwe unapita nyumbani si unajua mambo ya wanawake.

mke wake mwenyewe utata kweli kweli, sasa mi najiuliza kwani yeye hajui mambo ya wanaume au anataka tukosabe bure sababu namdai bado??
 
Hajali kama utamsaliti anachotaka mkewe mdogo apate mahitaji yake...dah! Maisha magumu jamani. Mpaka watu wako radhi kukodishia wake zao!
 
unajua ktk hii dunia mitihani ipo mingi sana sasa huo ni mmoja wapo swala hapo kinachotakiwa ni ubinadamu na si vinginevyo msaidie kwani waswahili wanasema akufasadiae kwenye shida ndiyo rafiki wa kweli.
 
Ukute jamaa genuinely anakuamini umwangalizie kaya yake,halafu wewe unaingiza mawazo ya ukware.
 
Hajali kama utamsaliti anachotaka mkewe mdogo apate mahitaji yake...dah! Maisha magumu jamani. Mpaka watu wako radhi kukodishia wake zao!

Nasikia nannhii anakodishwa,ni kweli? Bei gani kwa siku?
 
Huyo kakuamini sasa wewe umekosa imani tukusaidieje?/ndugu.. Sangarara..wewe inamaana ujiamini nazaidi ulishamtamani mke wa fundi wako!!kweli mbinguni wanakokutaja tutafika??sijui ngoja tuone mwisho wa movie!
 
Last edited by a moderator:
Huyo jamaa ana akili sana na anajua kuua sooo kwa taarifa yako wewe ndo unaliwa............na wewe siku hiyo jamaa akirudi atakukuta umekaa na mkewe kama ulivyomkuta wewe na mkeo
 
ukiona hivyo ujue yamemfika...lakini bado najiuliza kwani mna undugu wowote mpaka akuachie familia yake?...au ndio mambo ya ukikipata kitumie, hivyo kakupata bhana lazima utumike.
 
Kwa nini usingemwambia na wewe unataka kusafiri?Angalia mkuu dunia siyo kabisa hii
 
Huyo kakuamini sasa wewe umekosa imani tukusaidieje?/ndugu.. Sangarara..wewe inamaana ujiamini nazaidi ulishamtamani mke wa fundi wako!!kweli mbinguni wanakokutaja tutafika??sijui ngoja tuone mwisho wa movie!

Kakakiiza, tuwe wakweli, Mwanamke na Mwanamme ni kama Moto na Fuel, si busara hata kidogo kuruhusu mazingira ya faragha/hatarishi na mwanamke ambaye si ndugu yako,si mtoto wako, sio busara hata kidogo, mimi nalitambua hilo na kwa sababu namuogopa Mungu sintokwenda kumsalimia huyo mwanamke.

Kinanchonishangaza ni kwamba, huyu jamaa haelewi madhara ya maamuzi yake? I wish awe ameniambia habari hizi mwenyewe ama sivyo lazima aaribiwe.
 
Back
Top Bottom