Huyu George Maratu wa ITV style yake ya utangazaji ikoje?

Si mwisho tu, ni kila anapomalizia sentensi anakuwa kama "gramophone" linalotaka kuwa "rewound" na kubadilishwa sindano. Ukiyajuwa haya utajuwa nasema nini.
Duh...inawezekana huwa simfuatilizii vizuri labda! Au pengine ni tofauti yetu ya 'taste' tu! Maana hata nikisema nimlinganishe na maripota wengine bado 'sioni' ubaya wake!(frankly, hanikeri!)

Btw, kumbe mada hii kumuhusu Marato imewahi kujadiliwa humu hapo kabla: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/132896-huyu-george-maratu-wa-itv.html

Kuna blogger mmoja yeye amemuelezea hivi kwa ufupi:

[h=3]George Marato wa ITV[/h]

George Marato ni mwandishi mashuhuri wa kituo cha televisheni cha ITV ambaye hurusha habari kutoka mkoa wa Mara.

Kwa muda niliyomfahamu ni mtu ambaye ni mtafutaji mzuri wa habari. Iwapo habari haijamfikia Marato, hiyo siyo habari. Itakuwa ni uzushi. Pamoja na kazi anayofanya ITV huwa anaandika makala kwa magazeti mbalimbali ya hapa nchini.

Kwenye picha anaonekana akiandaa habari kwa ajili ya kurusha hewani.
 
watu wengine wakikataaliwa mapenzi hasira zao wanaziondoa kwa kuwaanzishia thread walio wakataa. Na miongoni mwa mifano michache ni hii thread.
Nikiripoti kutoka Musomaaaaaaa, mimi ni Geooooooooooorge Maratu wa aiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii tiiiiiiiiiiiiiiiiiii viiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Jamaa anaboa kinoma, mimi nikimsikiliza huwa nahisi kizunguzungu. nadhani aliambiwa akitaka kuwa maarufu lazima awe unique.
 
Namna ya utangazaji wako kwenye luninga unakera sana , hivi ni kwanini lazima uvute hayo maneno unapomalizia sentensi? ni mbwembwe au nini? hivi hujuwi kuwa Kiswahili kikiongewa au kutumika kutangaza kama kilivyo kina ladha yake zaidi yakukigeuza na kuvuta maneno bila sababu yoyote?

Awali nilikuwa nikifikiri labda una lafdhi (accent) ya lugha fulani ya Tanzania na huna budi na kila unapoendelea kutangaza kwa Kiswahili utabadilika kwa ku "improve" lakini baada ya kukusikiliza kwa muda mrefu sasa, naona unazidi. Sijui ni nani alikusifia kuwa kwa kuongezea kuvuta sauti ya matamshi ya kila neno la mwisho la sentensi ni utangazaji mzuri? aliyekusifia anakudanganya, tangaza kwa kutamka maneno kiufasaha na kama kawaida ya Kiswahili utafanya vizuri zaidi. Tafadhali badilika.
avoid the ignorant." (Qur'an 7:199)
 
Kumbe mkuki kwa kitimoto.....
Just imagine unavyokera watu hapa JF dada yangu FF; kumbe nawe uwaga unakerwa! Sina tatizo sana na G.Maratu, lakini kumbuka: One man's meat is another man's poison.
 
Basi hapa Mbeya kati ya watangazaji wanaopendwa sana si tu na wazee bali wamama,vijana na watoto ni hawa hapa;
G.Marratu
Hamad maulid hamad
Maulid wa kitenge
Pendael omari
Rainfred Masako
Mareen Hassan
Zakaria wa Tbc one
Juma nkamia japo hayupo.
N.k
@kila mwandishi ana talent yake kuwasilisha habari
ktk kuwasilisha lazima ujue kuna watu watampenda wengine hawatampenda
HILO LA KAWAIDA SANA.

~tHe aLpHA~Nimechangia!
 
Namna ya utangazaji wako kwenye luninga unakera sana , hivi ni kwanini lazima uvute hayo maneno unapomalizia sentensi? ni mbwembwe au nini? hivi hujuwi kuwa Kiswahili kikiongewa au kutumika kutangaza kama kilivyo kina ladha yake zaidi yakukigeuza na kuvuta maneno bila sababu yoyote?

Awali nilikuwa nikifikiri labda una lafdhi (accent) ya lugha fulani ya Tanzania na huna budi na kila unapoendelea kutangaza kwa Kiswahili utabadilika kwa ku "improve" lakini baada ya kukusikiliza kwa muda mrefu sasa, naona unazidi. Sijui ni nani alikusifia kuwa kwa kuongezea kuvuta sauti ya matamshi ya kila neno la mwisho la sentensi ni utangazaji mzuri? aliyekusifia anakudanganya, tangaza kwa kutamka maneno kiufasaha na kama kawaida ya Kiswahili utafanya vizuri zaidi. Tafadhali badilika.

Hizo ni swaga zake.
 
:juggle::juggle::juggle:huyo jamaa alipata mke kwa ajili ya hicho kisauti chake, mnataka aache ili aachane na mke wake?nyie vp pateni ushauli kwa mke wake kwanza.
 
Kuwa mvumilivu FF huwezi kupendezwa na kila mtu....by the way George Maratu huwa ana news moja tu katika habari tena si kila siku.
 
Namna ya utangazaji wako kwenye luninga unakera sana , hivi ni kwanini lazima uvute hayo maneno unapomalizia sentensi? ni mbwembwe au nini? hivi hujuwi kuwa Kiswahili kikiongewa au kutumika kutangaza kama kilivyo kina ladha yake zaidi yakukigeuza na kuvuta maneno bila sababu yoyote?

Awali nilikuwa nikifikiri labda una lafdhi (accent) ya lugha fulani ya Tanzania na huna budi na kila unapoendelea kutangaza kwa Kiswahili utabadilika kwa ku "improve" lakini baada ya kukusikiliza kwa muda mrefu sasa, naona unazidi. Sijui ni nani alikusifia kuwa kwa kuongezea kuvuta sauti ya matamshi ya kila neno la mwisho la sentensi ni utangazaji mzuri? aliyekusifia anakudanganya, tangaza kwa kutamka maneno kiufasaha na kama kawaida ya Kiswahili utafanya vizuri zaidi. Tafadhali badilika.
umewahiwa kumsikia Ummul Kheri wa Dutch Welle au Jocob Tesha wa Rtd(Tbc)? au Ngayona nkondola wa Radio Free ! Hiyo ID yake hivyo acha nongwa !
 
Waambie haooo!! Chuki binafs zawatesa dahh!! CNN or BBC what for kwetu ? Lazima tuige kila kitu shindwa wee!! BIG UP MARATU :A S embarassed::spy:
 
Masako alivyo tangaza kifo cha baba wa taifa ni ulivutiwa haujavutiwa? au kipindi kile alipokuwa anatangaza nia ulionaje?. Zile ndo swagga zao. mia
 
Jamani acheni unafiki Huyu jAmaa anatia kinyaa hakuna MTu serious anaweza kusikiliZa upupu wake watu wa mara wameliwa huweZi huweZi sema ni creativity ni ushamba uliochanganyika na shule nd ogo take na mabosi wake ni kweli huweZi kuwakuta wasomi kermis best practice za serious media wakiruhusu hip ushuzi media zetu haZiko serious

Mkuu hata wewe hauko serious; unachanganya herufi kubwa na ndogo alafu udai kuwa 'a great thinker'!
Nadhani facebook inakufaa mkubwa.
 
Mitanzania Ndivyo Tulivyo, angekuwa anatangaza radio za ughaibuni kila mtu ange-admire lakini kwa sababu ni wa hapahapa lazima mponde, Big up George Marato
 
Mshindwe na mlegee kawaboa nini mtoto wa watu? Hiyo ndo ishara yake ni sawasawa kabisa na masako nawapenda mno kwa style zao acheni chuki binafsi bana kha?!

"Nikiripotiiiii kutokaaaa kyabakariii mkoaaaaani Maaaaaara, huyu ni Joooooooooooooooji maratoo, waaaa aitiviiiiiiiiiii". Naipenda chorus hii, yaani basi tu.
 
Back
Top Bottom