Huyu bibie wa ki Hispania, nimwambie aje?

Bellerina kumpenda nampenda, inapokuja kwenye tamaduni za mahusiano wenzetu hawa tuko tofauti nao ktk at least vitu viliwi, kwenye uhusiano wako straight na ni waaminifu zaidi yetu, kwenye swala la ndoa huwaga naona kama wanaweza kutoka muda wowote wakiboreka, divorce si ishu kwao. Katika hili la divorce I'm still old fashined, mimi naamini ndoa ni kufa na kuzikana. Kuwa na mke mzungu sijawahi fikiria huko nyuma ila nimeanza kulifikiria. Huyu bibie nadhani anafikiria ndoa ila si unajua kwao haiendagi fasta kivile, anaweza kutaka mkae pamoja hata five years kabla ya kuingia kwenye ndoa!
New generation ya Wahispania, ndoa kwa maana ya "kufunga ndoa", sio issue kwani sheria zao zinawapa haki ya kukubalika kama wana ndoa kwa kuishi pamoja miaka miwili. Labda utafautishe baina ya divorce na separation. Kwao, divorce ni suala gumu sana kiasi kwamba "wanahofu ya kuoana kwa kuogopa urasimu na gharama kubwa za divorce". Kwa hiyo upo right unaposema wanaweza kukaa pamoja kwa miaka mingi kabla ya kuamua kufunga ndoa, lakini hata ikifikia hatua hiyo, kunakuwa na uhakika wa kuwa ndoa hiyo itadumu. Kwa hili sioni ubaya wowote kwani "sababu kubwa ya divorce katika jamii zetu ni kukimbilia kuoana", baada ya hiyo miaka 5 uliyosema au kasoro, mnagundua kuwa picha haziendi na mnaachana. Na kwa kuwa "at first instance" unaogopa commitment, hii ni faida kwako. Hata hivyo ninakushauri uwe na uamuzi thabiti kwani kukataa kwako commitment kunaweza kupelekea "kumsaliti huyu binti", na kwa kuwa umeshaonja uchungu wa kusalitiwa, usije ukawa msaliti wewe.
Kuhusu tafauti za kiutamaduni, ni suala la kila mmoja kujifunza mema ya utamaduni wa mwenzake, kuvumilia unayoyahisi ni mabaya kwako, na zaidi kulegeza kamba katika misimamo yetu.
Ikiwa huyu msichana kakubali kurudi Bongo, ni ishara tosha ya kuwa nakupenda kweli kwani tatizo au kikwazo kikubwa kwa Wahispania (hasa wasichana) ni kuhama kwao.
Mkuu, ikiwa unampenda, usisubiri sana na chukua uamuzi haraka.
 
mapenzi ya kizungu??? Babaaaangu utasalitiwa vibaya mno hutaamini macho yako, kama yeye hajali mahusiano ya mpenzi wako ulienae siku akiamua kutema atashindwa nini? Hapo ndipo pabaya usipaguse, labda kama unataka kulitandika tunda.
 
Nashukuru Dr, ushauri mzito huu, ila swali jingine nimekuwa najiuliza, uhusiono wa awali ulikuwa casual, huu wa sasa utakuwaje? utakuwa kama awali au she will be more demanding? Sijaweza tengeneza picha bado
toe-in-water_thumb[10].jpg

...kila mtu na hisia zake, pima mwenyewe hilo 'zali la mentali!'

Bellerina kumpenda nampenda, inapokuja kwenye tamaduni za mahusiano wenzetu hawa tuko tofauti nao ktk at least vitu viliwi, kwenye uhusiano wako straight na ni waaminifu zaidi yetu, kwenye swala la ndoa huwaga naona kama wanaweza kutoka muda wowote wakiboreka, divorce si ishu kwao. Katika hili la divorce I'm still old fashined, mimi naamini ndoa ni kufa na kuzikana. Kuwa na mke mzungu sijawahi fikiria huko nyuma ila nimeanza kulifikiria. Huyu bibie nadhani anafikiria ndoa ila si unajua kwao haiendagi fasta kivile, anaweza kutaka mkae pamoja hata five years kabla ya kuingia kwenye ndoa!
 
Kaka unasubiri nini sasa?tuletee shemeji bana,kama mapenzi yapo why unaupa dhuluma moyo?
 
ukiwa umechoshwa na kazi, ukipita humu...unakuta maandishi mazuri. Ila Mbu na Mwanakili90 mmeniacha hoi the way mlivyo-present majibu. Jf ni ntamu!
 
...wewe unampenda, yeye anakupenda. Tatizo ni nini ilhali mlishaishi pamoja?
Unaung'ang'ania mlango ulokwishajifunga, (ex-gfriend wako) wakati dirisha la
kutokea li wazi?

Ushauri wa bure. Acha kuomboleza msiba uliokwisha, move on with you life,
Open your heart...! fungua moyo wako kwa mrembo wa kihispania, achana na huyo
'marehemu'

Mbu yani acha tu, hya wee! subiri tufungue mioyo:))) ha ha

Mleta mada!..Take a chance if you can, inaonesha mko in love!..Hivyo basi live the present life not the past!!
 
Acha kujidanganya wewe. Mbona moyo wako umeshaufungua? Hebu vuta huyo mrembo wa kispaniola maisha yaendelee bwana.
 
Turudi kwa huyu bibie wa Kihispania, so we had a relationship kwa mwaka moja plus, apart from being my mpenzi she was a friend, hakuwa kama wazungu wengine (wanawake) niliowafahamu kwa maana kutaka kuwa juu ya mwanaume and being too demanding emotionally, but on the other hand she used to challenge me the way no other woman did, alinieleza mapungufu yangu niliyoyajua na ambayo sikuyajua kabla, alinibadilisha namna yangu ya kufikiri kimfumo dume kwa kiasi kikubwa. She made me a better man, lazima nikubali.
Nadhani ni moja ya watu wachache walionisoma na kunifahamu sana
, bila kujua na mimi nikajikuta nimemfahamu sana japo tulikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi kifupi. Hadi leo J5 sijamjibu!

Hapo nilipobold ndio nilikuwa napatafuta hasa hapo pekundu. Kama unaamini kwa dhati kabisa kuwa wewe umebadilika - yaani unafikiri kimfumo jike kwa sasa - na upo tofauti na ulivyokuwa kabla ya kukutana na huyu mzungu basi endelea. Ila usije kuanza kulalamika kuwa umepangiwa zamu ya kupika, kufua nguo, kuogesha watoto na mambo mengine yanayofanana na hayo. Kuhusu kuwa demanding asingeweza kuwa demanding kwa sababu mlikuwa marafiki tu na hamkutamkiana hata mara moja kuwa mnapendana. Sasa awe demanding ili iweje. Yeye alikuwa anakusoma tu na kukurekebisha hapa na pale ili ufanane fanane na tabia za kwao.
 
Don't worry brother, mwambie kuwa unampenda na usimfiche chochote! Lakini naoomba uelewe kitu kimoja ndugu yangu: Wanawake wachache sana wanaoweza kuwa katika mahusiano na mwanaume mmoja. Kwa hiyo kama unaamua kukubali kuingia kwenye deep love, jitahidi usiingie kwenye details zake sana wala kufuatilia maisha yake kwa undani sana. Anaweza akawa anakupenda, lakini inawezekana naye akawa alishawahi kuwa na mtu ambaye anampenda sana. Hivyo ukiamua kumkaribisha kwenye maisha yako, uwe tayari kwa lolote ili usije kuumia tena!
 
Hapo nilipobold ndio nilikuwa napatafuta hasa hapo pekundu. Kama unaamini kwa dhati kabisa kuwa wewe umebadilika - yaani unafikiri kimfumo jike kwa sasa - na upo tofauti na ulivyokuwa kabla ya kukutana na huyu mzungu basi endelea. Ila usije kuanza kulalamika kuwa umepangiwa zamu ya kupika, kufua nguo, kuogesha watoto na mambo mengine yanayofanana na hayo. Kuhusu kuwa demanding asingeweza kuwa demanding kwa sababu mlikuwa marafiki tu na hamkutamkiana hata mara moja kuwa mnapendana. Sasa awe demanding ili iweje. Yeye alikuwa anakusoma tu na kukurekebisha hapa na pale ili ufanane fanane na tabia za kwao.

Tata unanitisha kidogo, so tukianza upya there will be different rules, kwamba atakuwa more demanding! Sijabadilika completely, kupika hapo parefu, bado
 
Wewe acha kupoteza muda maisha mafupi furahisha moyo wako maisha bila ya furaha ya dhati sio maisha. wa2 wanatafuta furaha za kweli na hawapat if u feel de way she feel usingojee mara mbili try ur luck
 
Bellerina kumpenda nampenda, inapokuja kwenye tamaduni za mahusiano wenzetu hawa tuko tofauti nao ktk at least vitu viliwi, kwenye uhusiano wako straight na ni waaminifu zaidi yetu, kwenye swala la ndoa huwaga naona kama wanaweza kutoka muda wowote wakiboreka, divorce si ishu kwao. Katika hili la divorce I'm still old fashined, mimi naamini ndoa ni kufa na kuzikana. Kuwa na mke mzungu sijawahi fikiria huko nyuma ila nimeanza kulifikiria. Huyu bibie nadhani anafikiria ndoa ila si unajua kwao haiendagi fasta kivile, anaweza kutaka mkae pamoja hata five years kabla ya kuingia kwenye ndoa!

Naona kama unajaribu ku generalise wazungu. Mediterranean countries kama Italy, Spain, Portugal and Greece ni family oriented. Tofautisha na nchi kama Uingereza whose people desire modernity, meaning like career outside the home, luxuries, freedom preferred over virtue, etc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom