Huyu aweza kuwa mrithi wa Yoweri Museveni

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
museveni.jpg


Habari zilizotufikia ni kwamba rais Yoweri Museveni anaweza kung'atuka atakapofikisha miaka 75. Hii ni kwa mujibu wa
maelezo yaliyotolewa na Museveni mwenyewe alipohojiwa na shirika la habari la Nation kupitia NTV Uganda. Alisema hana pingamizi kwa mke wake kugombea urais baada yake. Na kuna tetesi kuwa chama cha Museveni NRM kingependa Janet Museveni amrithi mumewe. Je hii ni janja ya Museveni kuendelea kutawala nyuma ya pazia? Je mwanae aliyemuandaa muda mrefu atakubaliana na hili au ameonyesha kutofaa? Je waganda watakubali kuendelea kuwekwa kinyumba na Museveni ambaye amewatawala kwa mabavu kwa miongo mingi. Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.
 
SHETANI azidi kukubariki ili hatimaye mwanao MUHOOZI awe makamu wa raisi wakati mama yake JANET ni Rais wa Uganda
 
Back
Top Bottom