Huyo mbunge wa CHADEMA Mwanza, aliyetaka kuhongwa ni nani?

CHADEMA SENGEREMA; TAARIFA KWA UMMA


WILLIAM NGELEJA NA HAMIS MGENJA WANAPONGEZANA KWA KUTAPELIWA! HILA HAZITAINUSURU CCM INAYOUMWA NAMBULILA!


KWA siku mbili mfululizo kumekuwepo na propaganda na uzushi mkubwa unaonezwa kupitia njia mbalimbali kuwa Waziri William Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema, amehamisha uongozi wote wa juu wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema.

Kupitia taarifa hii kwa umma, CHADEMA Wilaya ya Sengerema tunapinga uzushi huo, ambao watu wazima na akili zao wameamua kukaa chini na kuupika, wakiwa na madhumuni yao ambayo kwa bahati mbaya sana yanajulikana siku nyingi sana, kwa sababu CHADEMA ni chama imara kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya chini kabisa inayoitwa msingi.


Tunajua kuwa uzushi huo ni sehemu tu ya mpango mkakati ambao CCM inafikiri itaweza kujinusuru, kuwasahaulisha na hatimaye kuirejesha Kanda ya Ziwa katika nchi ya Misri, baada ya watu Kanda ya Ziwa kuonesha kasi ya ajabu kuikimbia nchi hiyo ya mateso kwenda nchi ya ahadi, CHADEMA.


Tumelazimika kutozipuuza na kuamua kuzungumzia uzushi na propaganda hizi kwa sababu moja mkubwa, moja ya malengo yake makuu ni kutaka kuwavunja nguvu wananchi, Watanzania wema ambao wameamua kwa dhati kabisa kuunga mkono upinzani wa kweli unaongozwa na CHADEMA, kwa ajili ya kufikia mageuzi ya kweli ya uongozi na kupata mfumo mpya wa utawala.

Ni mwendelezo ule ule wa CCM na serikali yake kuwarubuni na kununua makapi ya uongozi ambayo yamejificha katika mwavuli wa upinzani. Mbinu hii haijaanza jana wala leo, na kwa namna ambavyo siasa za nchi hii sasa zinavyokwenda, huku CCM ikiendelea kuwadanganya……….

Lakini pia propaganda na uzushi huo ulioanzishwa na Mbunge Ngeleja na viongozi wake wa wilaya na sasa umedakwa juu kwa juu bila hata tafakuri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgenja, pia hauwezi kuachwa hivi hivi kwani ndani yake umedhihirisha kwa kiwango cha hali ya juu namna CCM na viongozi waandamizi wa serikali yake, wanaweza kudiriki kuudanganya umma wa Watanzania mchana kweupe kwa nia ya kutimiza mchezo mchafu kwa ajili ya manufaa ya watu binafsi na chama chao. Hawaangalii taifa, wala wananchi.

Uongo na upotoshaji mkubwa katika mpango wa Ngeleja na wenzake Sengerema

Kwanza imepotoshwa kuwa mmoja wa wanaotajwa kuwa wanachama wa CHADEMA ambao wamehamia CCM, Bw. Ayub Thomas Malima, alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema, huu ni uongo na upotoshaji mkubwa, lakini ni aibu kubwa kwa CCM na serikali yake kwa sababu umefanywa kwa maelekezo na chini ya Waziri Ngeleja.

Ukweli ni kwamba, Bw. Malima alivuliwa uongozi na uanachama tangu Julai 20, 2010, katika Mkutano Mkuu ulioitishwa kujadili utovu wa nidhamu wa bwana huyo. Moja ya tuhuma zilizowasilishwa kwenye mkutano wa maamuzi ni kubainika kwa mipango yake ya kujipatia fedha kutoka kwa mgombea ubunge wa CCM, William Ngeleja ili amfanyie hujuma na kumwangusha mgombea ambaye angesimamishwa na CHADEMA.

Kila mtu anayefuatilia siasa za Sengerema tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, mpaka sasa anafahamu hali ya Ngeleja ilivyokuwa ya hati hati kuweza kurudi bungeni, kutokana na chama chake na yeye mwenyewe kuchokwa na wananchi.

Kwa hiyo moja ya mbinu kabambe ilikuwa ni kuhakikisha kila njia inatumika, kuhakikisha anapita bila kupingwa, akiogopa kubwagwa.

Kwa umakini wa CHADEMA kama tulivyosema hapo juu, chama kiliweza kujua hata mipango ya hujuma hizo ilipokuwa inafanyika. Ilikuwa ikifanyika katika moja ya hoteli mjini hapa iliyopo Barabara ya Kamanga. CHADEMA kilikuwa na ushahidi mkubwa juu ya njama hizo, ikiwemo sauti zilizorekodiwa na hata wajumbe aliowaita ili wamsaidie kufanikisha suala hilo, bahati nzuri walikuwa waaminifu na wapambanaji wa kweli, hivyo walileta taarifa zote.

Baada ya wajumbe kumvua uanachama, Kamati Tendaji ya Jimbo la Sengerema ilimteua Ndugu Said Shabaan kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema ambaye anaendelea kukaimu hadi leo.

Sarah Mathayo, siyo Katibu wa BAWACHA kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari kadhaa, bali ni mke wa Katibu wa Wilaya (Kesy Misalaba) ambaye yeye pamoja na mmewe wana tuhuma ndani ya chama kuhusika kugawa fedha, tisheti na chumvi, vitu vilivyotolewa na CCM ili kuwapatia wapiga kura. Kiongozi pekee wa Wilaya wa BAWACHA ni Bi. Agnes F, ambaye ni Mratibu. CHADEMA hatuna cheo cha katibu wala mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya kwa mujibu wa katiba yetu. Hii yote inathibitisha namna uongo huo ulivyo mkubwa!

Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Sengerema ni Deus Juma, ambaye mpaka tamko hili linapotolewa yuko kazini, akitekeleza majukumu yake kama ilivyo kawaida ya CHADEMA, hivyo aliyetajwa katika vyombo vya habari, Stanslaus Pastory kuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA ni uongo mkubwa.


Baadhi ya watu hao waliokimbia majukumu ya kutumikia umma, kwa sababu ya uroho wao na kuwasaidia wananchi kuijua rangi yao halisi, walishafukuzwa siku nyingi kwa sababu walikiuka taratibu za chama kwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Diwani wa Viti Maalum, Bi. Sarah P. Nyanda.

Kiuhalisia, waliowahi kuwa wanachama wa CHADEMA Sengerema waliovutana na akina Ngeleja kwenda safari moja ya kifo cha CCM, ni Ayub Malima na mke wake, Bi. Luci Mussa na Kesi Misalaba na mke wake, Bi. Sarah Mathayo, wengine waliotajwa katika vyombo vya habari kuwa ni wanachama wa CHADEMA wala hata hatujui uanachama wao unafanana vipi, maana hawakuwahi kuwa wanachama wa chama hiki makini.

Chama kinapanga kufanya mikutano ya hadhara wilaya nzima ili kuwafikishia ukweli wanachama na Watanzania wote wenye moyo wa dhati katika mapambano ya kweli ya awamu ya pili, kuipigania nchi yao inayomalizwa na chama kilichofikia mwisho wa kufikiri na kuongoza.

Tuwaambie Ngeleja, Mgenja na wenzao wote katika mpango huo na CCM kwa ujumla, kuwa chama chao kinaumwa ugonjwa wa Nambulila ambao watu wa Iringa wanajua. Mtu anakuwa ni mzima, lakini hajiwezi kabisa kuzungumza. Yeye anajiona kuwa ni mzima, lakini wenzake wanaona tayari ni mfu. Hivyo wanambeba kwenda kumzika akingali mzima lakini hawezi kutamka kuwa yeye ni mzima, mpaka anazikwa akingali hai.

CCM waulize ugonjwa huo huwapata watu wenye makosa gani. CCM inaugua ugonjwa huo kwa makosa hayo hayo ambayo imefanya kwa Watanzania. Isubiri kuzikwa ikijiona!

Imetolewa leo, Januari 7, 2012

Said Shaaban

Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, Sengerema
 
Mkuu hebu soma kwa makini hapo kwenye rangi nyekundu. Wasalimieni huko Kanda ya Ziwa, waambieni wawe makini. Mkakati huo! Bahati mbaya ndo hivyo ulishajulikana siku nyingi sana, lakini pia umeanza kwa kuambulia makapi sana. Hata hao wa Magu na Kwimba wengi ni makapi yaliyokwisha kutemwa na CHADEMA kitambo. CCM wanachukua wanasema wameteka chadema, If God wants to destroy u, he first makes u blind, what u c is just the reflections of ure thinking and ideas, halafu unafikiri uko sahihi kweli! CCM should go back to draw board, wakiwa tayari wameshakabidhi madaraka
 
Mkuu hebu soma kwa makini hapo kwenye rangi nyekundu. Wasalimieni huko Kanda ya Ziwa, waambieni wawe makini. Mkakati huo! Bahati mbaya ndo hivyo ulishajulikana siku nyingi sana, lakini pia umeanza kwa kuambulia makapi sana. Hata hao wa Magu na Kwimba wengi ni makapi yaliyokwisha kutemwa na CHADEMA kitambo. CCM wanachukua wanasema wameteka chadema, If God wants to destroy u, he first makes u blind, what u c is just the reflections of ure thinking and ideas, halafu unafikiri uko sahihi kweli! CCM should go back to draw board, wakiwa tayari wameshakabidhi madaraka

Mkuu Makene Tumaini,,karibu sana jamvi hili bana! hivi kweli miaka yote haukuwemo humu?
 
Ile fani ya kumperesheni kichwa mgonjwa wa mguu inakamata nafasi ya ngapi kama ya uandishi ndo imebeba bendera?
Well, kwa ujumla Tanzania hakuna wataalam, wowote wale, hao madaktari unaozungumzia nao ni wale wale, wamepeleka waziri India kutibiwa upele na magamba ya ngozi. Lakini angalau wao wana kisingizio, hawana magodoro na sakafu za kulaza watu, hawana madawa, pia hizo medical malpractice hutokea duniani kote.

Lakini waandishi wa habari yani ndio uhoro wa kwanza na wa mwisho, na readership ya Watanzania nayo imelishwa putrid news mpaka imezoea uhoro kwenye media outlets kiasi kwamba hawasikii tena harufu.

Eti Kuficha jina la Mbunge aliyekataa rushwa ni "kulinda maadili ya taalum ya uandishi wa habari."! Jamani, kama sio vichwa vya panzi vilivyosindikwa mirungi mibichi ni kitu gani hicho? Waandishi wa habari wa Tanzania mmesoma chini ya miembe ya wapi nyinyi wazembe wa kutupwa nyinyi?
 
Hakusema mbunge wa mwanza ila amesema mbunge toka kanda ya ziwa
Wadau,
Gazeti la leo la Tanzania Daima,8/1/2012,limemkariri Dr.Slaa akisema kwamba chama cha Magamba kilitaka kumuhonga mmoja ya wabunge wa CDM mkoa wa Mwanza milion 323/=Tsh ili akihame chama hicho,..bahati mbaya gazeti wamelifadhi jina la Mbunge huyo(nadhani kwa ajili ya kulinda maadili ya taaluma ya uandishi)..Sasa kwa kuwa motto wetu ni ,''Where we dare to talk openly'',naomba atajwe kwa faida yake,chama,wanachama na nchi kwa ujumla..maana akitajwa anaweza kuja ulezea umma issue ilivyokuwa
Nawasilisha.
 
Magamba wameona hizi ndizo mbinu zao za mwisho kwa sasa,Mungu anaendela kuwalaani vibaka wakubwa nyie wa Resource zetu
 
Kila kiongozi ndani ya Chadema ananunulika tatizo bei tu.
 
Leticia Mageni(nyerere)mbunge wa viti maalum(Kwimba)alianza na kujiuzuru Uwaziri kivuli na kuahidiwa na Lukuvi kuwa angeteuliwa viti vya Uteuzi na Rais
 
Hawa jamaa wanapaswa kuwa makini hivi ndiyo wanajimbia kaburi kubwa Mbalizi walitanga wanachama 720 hewa the same Mby mjini 320 wakawaonyesha si zaidi ya 33 leo Sengerema tunaambiwa walio hamishwa si viongozi wa CDM kikatiba wakuu hii imekaaje

Naombeni ukweli kusu wale 32 wa NYANZA
 
Hakusema mbunge wa mwanza ila amesema mbunge toka kanda ya ziwa

Nashukuru mkuu kwa kuweka rekodi sawa,..nilioverlook baada ya huyo M/kiti wa Magamba mkoa wa Mwanza kumjibu Dr.Slaa,nikahisi labda ni mbunge toka Mwanza,nashukuru..
 
Kama ni kweli imeripotiwa hivyo basi Dr. Slaa mzushi, gazeti jongo na wewe mdaku.

Toka lini kuficha jina la mtu anaedaiwa kutaka kuhongwa ikawa ni "kulinda maadili ya taaluma ya uandishi"?

Toka lini Dr. Slaa ambae amejipambanua kwa kufichua mafisadi papa akashindwa kutaja jina la mbunge wao aliyekataa hongo?

Toka lini vigazeti feki feki hivi vya kibongo vikaandika kitu cha maana?

Hakuna taaluma mbovu nchini kama uandishi wa habari.

Taarifa ya gazeti inasema Dr.Slaa alimtaja huyo mbunge ila gazeti jina wamelihifadhi, Dr hana wa kumwogopa,kama aliweza kumlipua Mkulu atamshindwa nani?,..ni kweli baadhi ya magazeti na waandishi wanapotoka,..lakini kwa hili nadhani hili gazeti wako sahihi,ma be walikuwa hawajamuhoji huyo Mbunge nae atoe maoni yake, or hawajathibisha kikamilifu,kumbuka hii ni media,ujumbe wake huenda mbali.
 
Acheni kudanganyana ccm ni zaidi ya chama huyo wenje sisi wana mwanza tulimtumia kutuma msg kwa mwenyekiti wetu taifa, na kama anadai alitaka kuongwa it was from a personal level yeye na huyo aliyetaka kumpa hizo hela siyo chama, mwambie atafute pa kwenda wazawa wanadai jimbo lao 2015, m.i. S daima.
Nani kakudanganya wazawa hawako CDM?
 
Hili swala mbona ni la siku nyingi.

Kwenye Uchaguzi mkuu wa 2010 MB wa Nyamagana Mh.Wenje alitaka kuhongwa pesa na Lawrence Masha aliyekuwa MB wa Jimbo hilo kupitia CCM. Wenje alikataa nandiyo maana baadaye Masha akamwekea pingamizi kuwa hakuwa Raia na hivyo hapaswikugombea Ubunge. Hata hivyo pingamizi hilo lilitupwa.
 
Ile fani ya kumperesheni kichwa mgonjwa wa mguu inakamata nafasi ya ngapi kama ya uandishi ndo imebeba bendera?


kuwa na staha kijana!!!!kati ya fani inayoeshimika duniani ndio hiyo lait ungeipitia ungejua thamani!!!!
 
hey ngoja kwanza! Kwahvyo ile stori ya ngeleja kuzoa viongozi wa cdm ni uongo: teh teh teh
 
..............................................Loading.....................................
 
Meshack Opulukwa mbunge wa Meatu. Beleave or not

Mbona Kijana Sana Milioni 323 ndio zimtowe kwenye ubunge wake na heshima ambao hana uhakika kama atapata ,kama ni kweli basi mjinga sana Kweli anaweza kukubali kuchezewa ndevu zake na huyu Jambazi wa Madini ,chokoraa wa umeme Ngeleja mmh, anaweza akamshusha Makende Meshack Opulukwa Kama akawa si riziki ,si amini jamani duuh
 
Acheni kudanganyana ccm ni zaidi ya chama huyo wenje sisi wana mwanza tulimtumia kutuma msg kwa mwenyekiti wetu taifa, na kama anadai alitaka kuongwa it was from a personal level yeye na huyo aliyetaka kumpa hizo hela siyo chama, mwambie atafute pa kwenda wazawa wanadai jimbo lao 2015, m.i. S daima.

fikra masaburi mgando
 
Back
Top Bottom