Huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM

yaani inaboa sana Police kuua Raia mwenzake( mzawa) kisa kumnufaisha mkaburu ,Hivi ukiwa police na akili huwa inaharibika ?
CCM inaboa sana
 
Wafundisheni watoto wenu kuepuka udokozi kwenye mali za wawekezaji, acheni mawazo ya kimasikini la sivyo nyie na vizazi vyenu mtakufa vifo vya aibu.
yaani inaboa sana Police kuua Raia mwenzake( mzawa) kisa kumnufaisha mkaburu ,Hivi ukiwa police na akili huwa inaharibika ?
CCM inaboa sana
 
Endelea kupiga kampeni na kushawishi vijana wakakwapue dhahabu kwenye migodi: ama kwa hakika musipoacha mawazo yenu finyu yaviteketeza vizazi vyenu kwa vifo vya aibu.
Kila mara huwa nawakumbusha watanzania wenzangu kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia kile CCM na serikali yake wanafanya. Ukiachilia mabali yaliyotokea Tarime ya kuua wananchi wanaoenda kudai mali yao inayo dhulumiwa na wezi wa kizungu na vibaraka wao ndani ya nchi.

Angalia wanavyo shughulikia suala la umeme. Kikwete mwaka 2006 alitamka kwa mdomo wake kwamba ndani ya miaka 3 chini ya utawala wake mgao wa umeme utakuwa historia, sasa na asimame na athibitishe usemi wake huo!!

Kiinimacho kingine ni upumbavu wanaoufanya juu ya mitambo ya Dowans. Wanapitia mlango wa nyuma kununua mitambo hiyo wakidhani hatujui, wadadisi wa mambo mkitafuta info kidogo mtajua hiyo kampuni ya Symbion imefikiaje uamuzi wa kujitwika Dowans na hapo mtagundua tu kwamba ni jamaa wanazunguka mbuyu.

Niseme tu kwamba kwa CCM na serikali zake walipo tufikisha, si tegemei kwamba kuna mtu ana akili timamu anaweza kujiunga na chama hiki ambacho ni cha kuangamiza wananchi na mali zao.
 
Kwa ushabiki huu watanzania wengi watakufa vifo vya kujitakia.
attachment.php
 
Wafundisheni watoto wenu kuepuka udokozi kwenye mali za wawekezaji, acheni mawazo ya kimasikini la sivyo nyie na vizazi vyenu mtakufa vifo vya aibu.

wafundisheni au tuwafundishe kwani wewe sio mtanzania?nani kakwambia wemedokoa ni vile hauko katika eneo hilo
 
Ukimuona kijana anashabikia CCM ujue alinyonya ***** ya baba yake akiwa mdogo
 
Yaani nimeona hii heading Nimecheka kicheko kisicho na nusu.
Hivi majuzi nilikaa katika kilinge fulani na jamii moja ya wakulima, katika maongezi nilijaribu kujiweka katika support ya Chama Tawala.

One of the very old men told me and I quote ''yaani kijana na ujana wako wote huo unaiunga cccm mkono? Lazima utakua na matatizo'' End of quote.

Mie naliita JANGA
 
Mimi si Mshabiki wa siasa lakini bado sijaona chama chenye kuckuwa nafasi ya ccm na hicho kinanifanya niwe mshabiki wa CCM, ... CCM hii ingekuwa wakiritimba msingoena kwamba kuna makosa ya kina dowans, mafisadi wangefichwa.. mfano mzuri ni chama kinachotawala burundi na jinsi kinacvyowazima wapinzani... ukomavu wa domkrasia wa CCM ndiyo unawapa uhuru wa kupiga domo humu Jf, mzee slaa kusimama juu ya mimbari na list yake ya mafisadi bila kuletewa chokochoko kama anavyofanyiwa yule mpinzani Uganda, ukomavu wa kisiasa wa serikali unawaachia chadema kuandamana mpaka miguu iingie ndani.. inshort nina akili timamu 100% kuliko unavyofikiria wewe na bado nashabikia ukomavu wa kisiasa wa CCM
 
Hili la Dowans ni kichekesho kitupu
Kampuni inatoka marekani kuja kununua mitambo mitumba tanzania
kama walikuw ana mpango wa kuzalisha kumeme kwa nini wasingekuja na mitambo mipya ya kuzalisha umeme badala yake wanakuja kununua mitambo mtumba tanzania

Kama kama wametoka marekani na wamenunua mitambo mtumba hapa tanzania nikwa kujua potential ya mitumba yeyenyewe ambayo cc kwa umbumbumbu wetu na chuki za kimaskini hatuoni umuhimu wake. Kama wamenunua kwa pesa yao wewe kelele za nini. Funga bakuli lako watu wazalishe umeme wapate mpunga.
 
Ukimuona kijana anashabikia CCM ujue alinyonya ***** ya baba yake akiwa mdogo

umemaliza kutukana, lete hoja, but ujue CCm ni jiwe kuu la pembeni lililokataliwa na waashi.................................................
 
Mimi si Mshabiki wa siasa lakini bado sijaona chama chenye kuckuwa nafasi ya ccm na hicho kinanifanya niwe mshabiki wa CCM, ... CCM hii ingekuwa wakiritimba msingoena kwamba kuna makosa ya kina dowans, mafisadi wangefichwa.. mfano mzuri ni chama kinachotawala burundi na jinsi kinacvyowazima wapinzani... ukomavu wa domkrasia wa CCM ndiyo unawapa uhuru wa kupiga domo humu Jf, mzee slaa kusimama juu ya mimbari na list yake ya mafisadi bila kuletewa chokochoko kama anavyofanyiwa yule mpinzani Uganda, ukomavu wa kisiasa wa serikali unawaachia chadema kuandamana mpaka miguu iingie ndani.. inshort nina akili timamu 100% kuliko unavyofikiria wewe na bado nashabikia ukomavu wa kisiasa wa CCM

Hoya yako kwamba chama kinacho tawala Burundi kinawaminya wapinzani haina mashiko kwa sababu hali hiyo tulikuwa na yo miaka ya 1995. Jiografia ya Burundi na Tanzania inatosha sana kubadilisha hali na mbinu za utawala. ukijaribu kuitawala Tanzania kama Burundi mapinduzi ya kijeshi yanakuja kesho yake tu.

hoja yako ya Uganda bado narudia pale pale kwamba ukujaribu kuleta utawala kama wa mseveni hapa TZ haita chukua muda bila kushuudia jeshi likimeguka na hapo kuwa na Tanzania 3, moja ya kaskazini, nyingine ya ziwa magharibi na nyingine ya nyanda za juu kusini.

Wito wangu kwako ni kwamba badilika na ukemee uozo unaofanywa na CCM kwa kulinda wezi wa mali ya wananchi maskini. Huwezi kuniambia una akili timamu ili hali sukari kutoka malawi ni Tshs. 1200 ambao wao ni maskini kuliko sisi alafu sukari inayozalishwa hapo mtibwa na kagera unauziwa Tshs. 2000 na unasema unayo akili!!
 
nafikiri punguza makali ya lugha yako.

Kwani wote hao ni wana siasa lao moja hakuna hata wa afadhali. wamejaa tu maneno matamu lakini utekelezaji zero
 
umemaliza kutukana, lete hoja, but ujue CCm ni jiwe kuu la pembeni lililokataliwa na waashi.................................................

CCM ni jiwe kuu kwa ajili ya kusagia mifupa ya watanzania wanaokufa kwa kukosa tiba, chakula, na dawa.
 
Mleta mada yuko right kabisa, huwezi kuwa na akili timamau 'ukashabikia' CCM. Chama hiki ambacho mwenyekiti wake ndiye aliyetengeneza serikali ya CCM alimpeleka mahakamani waziri wake ambapo aliamini kabisa kuwa alitumia ofisi vibaya.
Kwa mshangao wa mwenye akili yeyote akaruhusu chama chake kimteue 'mtuhumiwa huyu' kuwa mgombea wa ubunge. Hakuishia hapo, alikwenda jimboni kwake na kumnadi kwa wapiga kura, ambao wengi wao ni 'mashabiki' wa CCM. Mashabiki hao (wasio na akili timamu-kwa mujibu wa mada yetu) wakamshangilia mwenyekiti wao pamoja na mtuhumiwa huyo badala ya kumhoji kulikoni?
Conclution yangu siku zote huwa ni kwamba, ukimwona mtanzania yeyote ambaye ni mwanachama wa CCM- basi ujue
a) Ana maslahi ya moja kwa moja na system. eg mshahara, biashara, ufisadi (rushwa) nk
b)Ni dependant wa mnufaika wa system hapo juu (a)
c) Ana matatizo ya akili ktk utambuzi na uchambuzi- bahati mbaya sana kundi hili kwa mtazamo wangu ndio kubwa sana ktk chama chetu hiki.
 
Miezi kadhaa nilisema "huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM" lakini waosha vinywa wakanikalia kooni. Sasa nalirudia tena kwani imejidhihirisha katika suala la kupunguza matumizi kwa kutowalipa wabunge posho za vikao kwani vikao ni sehemu ya kazi zao za kawaida.

Wabunge wa CCM wakiongozwa na spika wamegoma kata kata kuachia posho na mpaka wanamtishia Mh. Zitto Kabwe kuwa watamfukuza bungeni. Hii inadhihirisha kwamba CCM ipo kwa masilahi ya mifukoni mwao na si kwa maslahi ya wananchi na hivyo yeyote anayeishabikia pamoja na vitendo vyao naye hana akili timamu ya katambua mema na mabaya.

Miaka 50 ya uhuru na CCM madarakani lakini bado tuna shule za msingi zilizo ezekwa kwa nyasi, madawati hakuna ili hali tuna miti ya kutosha, umeme hakuna ili hali tuna makaa ya mawe hadi tunawauzia wageni, gesi ipo ya kutosha, geo-thermal ipo lukuki..... je, tuna haja gani kuwa na CCM??
 
Back
Top Bottom