Huwa mnamsoma Ulimwengu?

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Jenerali Ulimwengu

TUMEONA katika makala ya wiki jana jinsi kitoto kilichozaliwa katika familia ya mafisadi kinavyolelewa kifisadi, kinavyosomeshwa kifisadi, kinavyofanywa 'kifaulu' kifisadi, kinavyoajiriwa kifisadi, kinavyoozeshwa kifisadi na kinavyokuwa kitu kingine cha ufisadi katika mwendelezo wa utamaduni wa ufisadi kilimozaliwa.

Sidhani kwamba tunaweza kuwa na matumaini ya kupata lo lote la maana kutoka kitoto hicho kwa maana ya kuiendeleza nchi na kuwaendeleza watu wake. Watu wa aina ya kitoto hicho hawawezi kuijenga wala kuiongoza nchi, kwa sababu wao hawajajengwa wala kuongozwa katika misingi ya kujenga lo lote la maana isipokuwa kuendeleza utamaduni uliowazaa na kuwalea.

Kwa bahati mbaya, katika mazingira yetu, na katika mazingira ya nchi nyingi za Kiafrika, hawa ndio watu wanaoelekea kuchukua mikoba ya utawala kutoka kwa wazazi wao, katika mazingira ambamo mifumo ya utawala haiwaachii wananchi nafasi ya kuchagua viongozi wao.

Haya ni mazingira ambamo, kama nilivyoeleza katika makala zangu za nyuma, watawala wanaendesha nchi bila itikadi ya kimsingi inayowaelekeza na wanachofanya ni kila siku kuzuka na jipya lisilokuwa sehemu ya mwendelezo wa jambo jingine lo lote walilosimamia huko nyuma wala wanalotaraji kulisimamia siku za usoni.

Unakuwa ni uongozi wa kubabaisha, wa kila siku kuokoteza 'sound bite' za kauli-mbiu zisizodumu hata mwaka mmoja. Baada ya muda ukiwaangalia wanaonekana kama vile wamekwisha kusahau kauli-mbiu ya mwaka jana na sasa wanazindua nyingine.

Ni hali hii ndiyo inayojenga utegemezi wa kila aliye ndani ya utawala kwa 'busara' za Bwana Mkubwa, kwa maana ya kiongozi wa juu kabisa wa wakati huo, ambaye atakuwa na 'busara' kubwa sana ambazo hakuwahi kuwa nazo kabla hajaingia madarakani, na ambazo akiondoka madarakani anaziacha ofisini; anarudia kuwa mtu wa kawaida, wa akili kama zako na zangu.

Bila shaka hapa kuna tatizo: Waliomzunguka Bwana Mkubwa, kwa kukosa itikadi au mfumo wa fikra unaowaunganisha, na kwa kuhofia kupoteza 'kibarua' chao, wanajenga ukimya mkubwa na hatimaye hata uwezo wa kufikiri na kutamka kile wanachoamini unavia. Baada ya miongo michache katika hali hiyo hata yule aliyewahi kuwa mwalimu mzuri wa shule ya msingi hawezi tena kazi hiyo kwa kuwa kapoteza mazoea ya kufikiri, hata kwa kiwango hicho.

Papo hapo tunajua kwamba 'busara' za Bwana Mkubwa nazo hazina uhalisi wo wote kwa sababu zimetokana na sifa anazomwagiwa na waajiriwa wake na wapambe wengime. Sasa tukiunganisha 'busara' hizi feki na mazoea hafifu ya kutumia akili ya wasaidizi na wapambe wake, kinachozalishwa ni ombwe (vacuum) katika uongozi hata kama utawala unaweza kuwa na ufanisi wa kufanya menejimenti ya kilipo bila maendeleo.

Kwa kuwa maumbile hayapendi ombwe, Bwana Mkubwa na wapambe wake watajikuta wanafunikwa na itikadi kutoka kwingineko, kutoka nchi na asasi ambazo maslahi yake siyo lazima yasadifu na maslahi ya watu wetu. Mara nyingi haya maslahi ya pande mbili yanakuwa yanakinzana moja kwa moja, na vikali.

Yote hii ni kusema kwamba mazingira ambamo watawala wanaendesha utawala wao bila mfumo wa fikra, bila mtazamo wa kimkakati kuhusu mustakabali wa nchi yao na watu wao, katika mazingira hayo kitakachowaunganisha watawala hao ni ufisadi.. ufisadi wa ndani ya nchi ukisaidiana na kuelekezwa na ufisadi wa nje ya nchi.

Lile ombwe nililolitaja hapo juu linadhihirika hadi nje ya nchi, na wenye maslahi yao hawashindwi kulitambua hilo na kulifanyia kazi. Wanachofanya ni kuwapata mawakala wao katika nchi zetu watakaowatumikia. Malipo yao ni madaraka ya kisiasa, ambayo watawasaidia kuyapata katika gulio la kura pamoja na mapesa ya kuwapa ukwasi wa kuazima.

Hali ikiisha kuwa hivyo, hakuna linaloweza kufanyika kubadilisha fikra za watawala wa aina hii, kwa sababu ufinyu wao wa kufikiri na maslahi ya mabwana zao kutoka nje vinakuwa vimejenga ubia imara usiomsikia mtu wala jini. Mambo yao 'yanajipa' katika utaratibu tuliokuwa tukiujua kama Ubeberu lakini hivi sasa unatambulishwa kwa jina laini la Utandawazi.

Hii siyo hali ya kuruhusu, achilia mbali kuchochea, maendeleo. Maendeleo hayapatikani kutokana na mchakato unaoendeshwa na mawakala wa ndani wanaofanya kazi kwa kusimamiwa na kuelekezwa na maslahi ya kiuchumi ya Ubeberu. Hii ni hali ya kudumisha na kuimarisha uduni, udhaifu na umasikini wetu ndani ya kila aina ya neema tuliyopewa na maumbile na Mwenyezi Mungu.

Msomaji atakuwa amenielewa ni nini nataka kusema: kila kiongozi mwenye nia njema na watu wake na aliyedhamiria kuwaongoza ili waweze kujiletea (siyo kuwaletea) maendeleo ya kweli, hana budi kuwa na ubia katika uongozi wake. Kwanza atakuwa ameingia ubia na wananchi anaowaongoza; pili ataingia ubia na asasi anazozitumia katika malengo yake (tuseme chama, kwa mfano); tatu ndani ya asasi hizo ataunga ubia, atakula yamini, na viongozi wenzake wenye malengo kama yake.

Asipofanya hivyo, na akizidi kung'ang'ania kwamba uongozi wake hauna ubia, mtawala huyo anajidanganya, na wanaomwangalia na kumsikiliza watagundua baada ya muda si mrefu kwamba anao wabia ambao inamuwia vigumu kuwatangaza.

Hii si hali ya kuridhisha hata kidogo, na ni hali hiyo inayoifanya Afrika iendelee kumenyeka na umasikini wakati inao kila aina ya utajiri. Mojawapo ya mambo yanayoweza kuchochea maendeleo ni utawala bora, na utawala bora lazima uwe ni utawala wa pamoja, angalau kwa watu waliokula yamini ya pamoja ya kufanya mambo fulani ili kufanikisha malengo maalumu.

Kinyume cha hilo ni nini? Iko mifano lukuki, lakini mmoja ni wa hivi karibuni na unahusu maneno yaliyojaa masikioni hata wakati nikiandika makala hii. Imezinduliwa kampeni kubwa, na yenye kelele nyingi, inayoitwa 'Kilimo Kwanza.' Lengo lake la jumla ni kutoa kipaumbele kwa kilimo, ambalo ni jambo jema na sahihi.

Hata hivyo, wakuu wa Serikali wanajua kwamba ilikuwapo sera iliyoitwa 'Siasa ni Kilimo' iliyotangazwa mwaka 1972 kisha ikawekwa kabatini. Alipoondoka Mwalimu madarakani na sera hiyo ikaondoka, kwa sababu, kama ninavyosema, alijizungushia ukuta wa matarishi badala ya kujijengea wigo wa viongozi wenzake.

Baadaye sana, mmoja wa warithi wake, ambaye kwa hakika zamani alikuwa ni mmoja wa hao matarishi wake, aliulizwa ni jambo gani alidhani alikuwa amesahau kulishughulikia katika utawala wake wa miaka kumi. Jibu lake? Kilimo .

Tunashangaa nini? Katika 'uongozi' usiokuwa na ubia, ni nani katika watu waliokuwa wamemzunguka angethubutu kumwambia, Mzee, samahani sana kwa usumbufu wangu, lakini naona kama vile tumesahau kilimo? Tena, hata kwa kusema "tumesahau" ili aonekane naye anahusika katika uzembe huo.

Tunajua tayari kwamba watawala wa Kiafrika hawana washauri. Ofisi za 'washauri' ni vituo vya kuwazawadia wapambe waliotoa huduma kwa Bwana Mkubwa (aghalabu huduma chafu) wakati akisaka madaraka. Hakuna ushauri wo wote wanaotoa mbali na kumshangilia Bwana Mkubwa na kumwambia, Mzee ile hotuba yako ya leo, haijapata kutokea! na upuuzi mwingine kama huo. Hakuna washauri bali wamejaa wapiga debe, mashabiki, wapambe na washikaji, wote wakigharimu fedha nyingi mno za walipa kodi.

Sasa mawaziri ndio hao, na washauri ndio hao. Ni kwa nini hasa tunataraji kupata maendeleo? Nakumbushia tena: Kufanya jambo lile lile kila siku kwa njia ile ile, na kutaraji kupata matokeo tofauti, ni ishara mojawapo ya taahira ya akili.

Itaendelea

Source: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1596

Nashauri isomwe pamoja na hii:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/35474-ikulu-watakubali-kunipa-kibarua-nilichoomba.html

Nashauri pia baadaye hii yangu Mods waiunganishe kule kwa MM
 
Hii makala nzuri.

Inanikumbusha thesis ya historian Arnold Toynbee,katika kitabu cha world history,anasema zile civilization Duniani zilizodumu muda mrefu,ni zile ambazo viongozi walikuwa wanajaribu kuwafanya watu wafikiri.

Zile ambazo hazikudumu muda mrefu,ni zile viongozi walikuwa wanataka to lead by example,'mimesis',ameiita,mimic the leader.

Pia siku hizi tunasikia sana kuhusu so called ''cospiracy theory'',kwamba asasi 2000,elfu mbili zilizo juu[prominent] Duniani,zinatafuta kurubuni watu talented from all over the world. The agenda is to dominate the World. Au kuwarubuni ,au kutazama method yao ya kufanya kazi.

Get the man or get the method.
 
jenerali2.jpg

Huyu ni mwanafalsafa ambaye hadi tusubiri atuage ndipo tumuenzi? Mengi anayoandika anayafahamu kwa kina then kuyatengenezea lugha ya mzunguko ili ujumbe ufike bila ya maumivu sana au purukushani. Namfahamu kwa hoja zake tu na si vingine. labda makala hii itwaamsha.

TUMEONA katika makala ya wiki jana jinsi kitoto kilichozaliwa katika familia ya mafisadi kinavyolelewa kifisadi, kinavyosomeshwa kifisadi, kinavyofanywa 'kifaulu' kifisadi, kinavyoajiriwa kifisadi, kinavyoozeshwa kifisadi na kinavyokuwa kitu kingine cha ufisadi katika mwendelezo wa utamaduni wa ufisadi kilimozaliwa.
Sidhani kwamba tunaweza kuwa na matumaini ya kupata lo lote la maana kutoka kitoto hicho kwa maana ya kuiendeleza nchi na kuwaendeleza watu wake. Watu wa aina ya kitoto hicho hawawezi kuijenga wala kuiongoza nchi, kwa sababu wao hawajajengwa wala kuongozwa katika misingi ya kujenga lo lote la maana isipokuwa kuendeleza utamaduni uliowazaa na kuwalea.
Kwa bahati mbaya, katika mazingira yetu, na katika mazingira ya nchi nyingi za Kiafrika, hawa ndio watu wanaoelekea kuchukua mikoba ya utawala kutoka kwa wazazi wao, katika mazingira ambamo mifumo ya utawala haiwaachii wananchi nafasi ya kuchagua viongozi wao.
Haya ni mazingira ambamo, kama nilivyoeleza katika makala zangu za nyuma, watawala wanaendesha nchi bila itikadi ya kimsingi inayowaelekeza na wanachofanya ni kila siku kuzuka na jipya lisilokuwa sehemu ya mwendelezo wa jambo jingine lo lote walilosimamia huko nyuma wala wanalotaraji kulisimamia siku za usoni.
Unakuwa ni uongozi wa kubabaisha, wa kila siku kuokoteza 'sound bite' za kauli-mbiu zisizodumu hata mwaka mmoja. Baada ya muda ukiwaangalia wanaonekana kama vile wamekwisha kusahau kauli-mbiu ya mwaka jana na sasa wanazindua nyingine.
Ni hali hii ndiyo inayojenga utegemezi wa kila aliye ndani ya utawala kwa 'busara' za Bwana Mkubwa, kwa maana ya kiongozi wa juu kabisa wa wakati huo, ambaye atakuwa na 'busara' kubwa sana ambazo hakuwahi kuwa nazo kabla hajaingia madarakani, na ambazo akiondoka madarakani anaziacha ofisini; anarudia kuwa mtu wa kawaida, wa akili kama zako na zangu.
Bila shaka hapa kuna tatizo: Waliomzunguka Bwana Mkubwa, kwa kukosa itikadi au mfumo wa fikra unaowaunganisha, na kwa kuhofia kupoteza 'kibarua' chao, wanajenga ukimya mkubwa na hatimaye hata uwezo wa kufikiri na kutamka kile wanachoamini unavia. Baada ya miongo michache katika hali hiyo hata yule aliyewahi kuwa mwalimu mzuri wa shule ya msingi hawezi tena kazi hiyo kwa kuwa kapoteza mazoea ya kufikiri, hata kwa kiwango hicho.
Papo hapo tunajua kwamba 'busara' za Bwana Mkubwa nazo hazina uhalisi wo wote kwa sababu zimetokana na sifa anazomwagiwa na waajiriwa wake na wapambe wengime. Sasa tukiunganisha 'busara' hizi feki na mazoea hafifu ya kutumia akili ya wasaidizi na wapambe wake, kinachozalishwa ni ombwe (vacuum) katika uongozi hata kama utawala unaweza kuwa na ufanisi wa kufanya menejimenti ya kilipo bila maendeleo.
Kwa kuwa maumbile hayapendi ombwe, Bwana Mkubwa na wapambe wake watajikuta wanafunikwa na itikadi kutoka kwingineko, kutoka nchi na asasi ambazo maslahi yake siyo lazima yasadifu na maslahi ya watu wetu. Mara nyingi haya maslahi ya pande mbili yanakuwa yanakinzana moja kwa moja, na vikali.
Yote hii ni kusema kwamba mazingira ambamo watawala wanaendesha utawala wao bila mfumo wa fikra, bila mtazamo wa kimkakati kuhusu mustakabali wa nchi yao na watu wao, katika mazingira hayo kitakachowaunganisha watawala hao ni ufisadi.. ufisadi wa ndani ya nchi ukisaidiana na kuelekezwa na ufisadi wa nje ya nchi.
Lile ombwe nililolitaja hapo juu linadhihirika hadi nje ya nchi, na wenye maslahi yao hawashindwi kulitambua hilo na kulifanyia kazi. Wanachofanya ni kuwapata mawakala wao katika nchi zetu watakaowatumikia. Malipo yao ni madaraka ya kisiasa, ambayo watawasaidia kuyapata katika gulio la kura pamoja na mapesa ya kuwapa ukwasi wa kuazima.
Hali ikiisha kuwa hivyo, hakuna linaloweza kufanyika kubadilisha fikra za watawala wa aina hii, kwa sababu ufinyu wao wa kufikiri na maslahi ya mabwana zao kutoka nje vinakuwa vimejenga ubia imara usiomsikia mtu wala jini. Mambo yao 'yanajipa' katika utaratibu tuliokuwa tukiujua kama Ubeberu lakini hivi sasa unatambulishwa kwa jina laini la Utandawazi.
Hii siyo hali ya kuruhusu, achilia mbali kuchochea, maendeleo. Maendeleo hayapatikani kutokana na mchakato unaoendeshwa na mawakala wa ndani wanaofanya kazi kwa kusimamiwa na kuelekezwa na maslahi ya kiuchumi ya Ubeberu. Hii ni hali ya kudumisha na kuimarisha uduni, udhaifu na umasikini wetu ndani ya kila aina ya neema tuliyopewa na maumbile na Mwenyezi Mungu.
Msomaji atakuwa amenielewa ni nini nataka kusema: kila kiongozi mwenye nia njema na watu wake na aliyedhamiria kuwaongoza ili waweze kujiletea (siyo kuwaletea) maendeleo ya kweli, hana budi kuwa na ubia katika uongozi wake. Kwanza atakuwa ameingia ubia na wananchi anaowaongoza; pili ataingia ubia na asasi anazozitumia katika malengo yake (tuseme chama, kwa mfano); tatu ndani ya asasi hizo ataunga ubia, atakula yamini, na viongozi wenzake wenye malengo kama yake.
Asipofanya hivyo, na akizidi kung'ang'ania kwamba uongozi wake hauna ubia, mtawala huyo anajidanganya, na wanaomwangalia na kumsikiliza watagundua baada ya muda si mrefu kwamba anao wabia ambao inamuwia vigumu kuwatangaza.
Hii si hali ya kuridhisha hata kidogo, na ni hali hiyo inayoifanya Afrika iendelee kumenyeka na umasikini wakati inao kila aina ya utajiri. Mojawapo ya mambo yanayoweza kuchochea maendeleo ni utawala bora, na utawala bora lazima uwe ni utawala wa pamoja, angalau kwa watu waliokula yamini ya pamoja ya kufanya mambo fulani ili kufanikisha malengo maalumu.
Kinyume cha hilo ni nini? Iko mifano lukuki, lakini mmoja ni wa hivi karibuni na unahusu maneno yaliyojaa masikioni hata wakati nikiandika makala hii. Imezinduliwa kampeni kubwa, na yenye kelele nyingi, inayoitwa 'Kilimo Kwanza.' Lengo lake la jumla ni kutoa kipaumbele kwa kilimo, ambalo ni jambo jema na sahihi.
Hata hivyo, wakuu wa Serikali wanajua kwamba ilikuwapo sera iliyoitwa 'Siasa ni Kilimo' iliyotangazwa mwaka 1972 kisha ikawekwa kabatini. Alipoondoka Mwalimu madarakani na sera hiyo ikaondoka, kwa sababu, kama ninavyosema, alijizungushia ukuta wa matarishi badala ya kujijengea wigo wa viongozi wenzake.
Baadaye sana, mmoja wa warithi wake, ambaye kwa hakika zamani alikuwa ni mmoja wa hao matarishi wake, aliulizwa ni jambo gani alidhani alikuwa amesahau kulishughulikia katika utawala wake wa miaka kumi. Jibu lake? Kilimo .
Tunashangaa nini? Katika 'uongozi' usiokuwa na ubia, ni nani katika watu waliokuwa wamemzunguka angethubutu kumwambia, Mzee, samahani sana kwa usumbufu wangu, lakini naona kama vile tumesahau kilimo? Tena, hata kwa kusema "tumesahau" ili aonekane naye anahusika katika uzembe huo.
Tunajua tayari kwamba watawala wa Kiafrika hawana washauri. Ofisi za 'washauri' ni vituo vya kuwazawadia wapambe waliotoa huduma kwa Bwana Mkubwa (aghalabu huduma chafu) wakati akisaka madaraka. Hakuna ushauri wo wote wanaotoa mbali na kumshangilia Bwana Mkubwa na kumwambia, Mzee ile hotuba yako ya leo, haijapata kutokea! na upuuzi mwingine kama huo. Hakuna washauri bali wamejaa wapiga debe, mashabiki, wapambe na washikaji, wote wakigharimu fedha nyingi mno za walipa kodi.
Sasa mawaziri ndio hao, na washauri ndio hao. Ni kwa nini hasa tunataraji kupata maendeleo? Nakumbushia tena: Kufanya jambo lile lile kila siku kwa njia ile ile, na kutaraji kupata matokeo tofauti, ni ishara mojawapo ya taahira ya akili.
Itaendelea
 
Full clip, do you wanna mess with this?
Gangstarr, one of the best yet!
 
TUMEONA katika makala ya wiki jana jinsi kitoto kilichozaliwa katika familia ya mafisadi kinavyolelewa kifisadi, kinavyosomeshwa kifisadi, kinavyofanywa 'kifaulu' kifisadi, kinavyoajiriwa kifisadi, kinavyoozeshwa kifisadi na kinavyokuwa kitu kingine cha ufisadi katika mwendelezo wa utamaduni wa ufisadi kilimozaliwa.

Sasa "kulelewa kifisadi" na "kuozeshwa kifisadi" ndiyo kupi huko"?
 
I salute to Jenerali Ulimwengu.

hakika huyu ni ngwiji sana katika fani hii na mjuzi wa mengi na anajua mengi ya Tanzania kwani naye aliwahi kuwa ndani.
 
Sasa "kulelewa kifisadi" na "kuozeshwa kifisadi" ndiyo kupi huko"?

kaka, watoto wa wakubwa kwa maana nyingine wanapata mahitaji ambayo katika hali ya kawaida ni kufuru tupu! sasa hao ndio wanaoandaliwa kuwa viongozi wetu wa kesho
 
Huna akili wewe huwezi elewa, hivi una ID ngapi hapa JF hahahaha

Kama mtu unaweza "kujibiwa kiufisadi" kama ulivyofanya hapo juu, basi vyote "kulelewa kiufisadi" na "kuozeshwa kiufisadi" ni rahisi kuelewa! Hahaaahaa...ama kweli akili sina!
 
waweza kutoa ufafanuzi zaidi mkuu?

Jenerali is
Full clip - fully loaded gun, or fully equipped machine, well read, someone who can stand their own turf, well read, a bona fide intellectual.

Do you wanna mess with this? Self explanatory, who would?

Gangstarr- His flow has got that confidence that is rare among Tanzanian professionals, especially journalist- and characteristic ofthose who are on the other side of the law, such as do or die Gangstars

One of the best yet- simply stated.

That's a chorus to the song "Full Clip" by Gangstarr. For some reason when I was reading that song resonated with Jenerali's confident, intellectual and informed flow.
 
sijajua watz huwa wanataka unabii wa aina gani tena ili kufumbika macho kw ayale yanayosemwa na watu kama hawa. au kwa vile akina mkuchika walishasema kuwa 'hata mkiandika watu wenyewe hawana umeme wa kideo, hawasomi magazeti yenu...'
 
Kusema ukweli jamaa ni muwazi na ana makala nzuri sana hebu soma makala ambazo aliandika baada tu ya JK kuapishwa ndani ya RAI. Alitoa maoni mengi kuhusu hali ya nchi ilivyo na yeye JK km Prdnt nn afanye ili aondokane na ombwe la uongozi liloanza kujitokeza. JK hakuzingatia japo robo ya makala ya 'Salam zangu kwa JK' na matokeo yake tunayaona. Huyu jamaa ni mkali wa kuonya kwa maandishi yuko juu
 
I salute you Mziwanda.
Tunahitajia chakula kama hiki kiwe cha kawaida hapa jamvini. Siyo kwamba inaelimisha tu bali inaamsha chachu ya tafakuri ambazo zinaweza kuzaa mawazo mapya ambayo yanaweza wote kutupeleka direction inayotakiwa.
 
Mkuu ulimwengu anasomeka ila bado anaendelea na kaugomvi kak na mkapa na kidogo sasa anadiriki kupingana na utakatifu wa kambarage ktk maono yake ya kitawala, maana haishi kuwahukumu hawa wakuu wawili ktk kila makala zake, ni vizuri tunamsoma na kumtafakari maana mzee wetu ulimwengu kwakweli ana nyanga za mbivu kwelikweli.

Taratibu namuona anajiandaa kuanza kuishughulikia awamu ya nne baada ya kuiomba radhi awamu ya pili ambayo kwake yeye sasa anathubutu kutuaminisha kuwa ilikuwa bora zaidi kwa nchi yetu.
 
Mkulu Frank Delano Roosevelt,Jr,
Wakati mwingine inakuwa vyema kama unasinzia kupata usingizi kwanza ndipo unarudi barazani. Awamu ya pili ni lini aliiomba radhi na kwa kosa gani? Halafu pamoja una "ubovu" wa awamu zingine tatu according to you ni kipindi gani kibovu kuliko cha huyu Mkwere? Kulinganisha hakuna tatizo kwani hata wewe unalinganisha ndio maana umsema uanataka kuaminishwa
 
i like this guy,he walk the talk,he call a spade a spade,hana unafiki.waandishi vijana fanyeni mahojiano na ulimwengu,mpate kilicho ndani ya mtizamo wake,msisubiri tu kuandika wasifu wake akisha ondoka.

hii ni mashine inayoishi,jamaa anajua mambo mengi sana ya nchi hii,hawa ni watu ambao baadae wataitwa wanafilosofia na kuwekwa katika kumbu kumbu zetu,naamini haya tunayoyafanya leo(ujambazi wa mchana) vizazi vijavyo vitatuuliza tutajidai hatukujua lakini watatuambia mbona jenerali alikua anawaambia(someni kitabu chake cha rai ya jenerali-kipo pale E&D publishers jirani na kona bar-sinza).

hivi vichwa ni adimu sana vinazidi kutoweka mfano chachage,haroub jamani huyu mzee ametuambia mengi sijawahi kuona hata akiitwa na kuhojiwa specifically kuhusu maisha yake kama mwandishi,ametokea wapi amepitia yapi hadi kufikia hapo alipo sasa
 
Mkuu Mziwanda,

Huwa sikosi gazeti la Raia Mwema kila alhamisi, lengo kuu ni kumsoma huyu bwana. Kwa kweli ni mmoja kati ya watu wachache ambao nawapa heshima kuu nchini kwetu. Tumuombe mungu ampe maisha marefu kwani anachokifanya ni faida kubwa kwa wengi wengi
 
Huyu mzee ni fisadi tu hana jipya. Kwanza ni mdini. Pili yupo bitter baada ya kuwekwa benchi na kuondolewa kwenye lineage ya wala nchi..thats the motives msiwe naive mazee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom