Huu wizi wa vifaa vya magari bandari ya dar utakwisha lini?

Ufunguo

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
330
231
Hivi karibuni niliagiza gari ndogo (980 CC) kutoka Japan kutokana na unafuu wake (mafuta na bei) ili kukidhi mahitaji mbalimbali kulingana na mwenendo wa maisha ya sasa. Pamoja na kwamba serikali iliongeza kodi ya uchakavu kwenye magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 8 iliyopita, nilijikamua na kulipia gharama zote za ushuru.

Cha kushangaza pendekezo hilo kwa sasa limekataliwa na bunge na sijajua utaratibu unakuwaje kwa watanzania ambao wamekumbwa na tatizo hilo la kulipia ushuru ambao haukuwa umepata baraka za bunge. Anyway, tatizo langu la msingi hapa ni kwamba baada ya gari kufika bandarini na kukaa kama wiki moja kabla ya kutolewa, gari ilikutwa imeibiwa control box na power-window.

Baada ya kuhoji sana nikapewa document na bandari inayoonesha eti gari ilipokelewa bila control box na power-window wakati vitu vyote hivyo vilikuwepo wakati gari inasafirishwa hadi inafika bandarini Dar. Baada ya kuzama kwa undani zaidi nikagundua kumbe kuna mtandao kamili. Mkaguzi wa bandari anaweza kusema kitu X hakipo katika fomu ya ukaguzi wakati siyo kweli halafu baadae anawaambia vijana wake wakavyofoe vitu hivyo katika gari husika nafikiri kwa ushurikiano na agent.

Kibaya zaidi ni kwamba wanafanya unyama huo huku mmiliki wa gari tayari ameshalipia gharama zote za storage ikiwa ni pamoja na faini ya siku zilizozidi. Naamini tatizo hili si langu tu bali watanzania wengi limeshawapata, sasa tufanyeje wadau?. Je watanzania wakianza kupitishia mizigo yao bandari za nchi za jirani kama Kenya walaumiwe?.
 
Mkuu inauma sana hii tabia wabongo na serikali yetu legelege!
 
Hata majumbani siku hizi wanaiba wanaacha gari kama chuma chakavu. Njaa imekithiri mitaani watu wanakuwa wadokozi
 
Huu udokozi sijui utakwisha lini kwa kweli inaudhi sana,pole sana mkuu
 
Mkuu mimi walilamba CD changer!

Hawa nyangau wamezoea sana huo mchezo naona apo Mwakyembe itabidi atusaidie mwenye namba pls ili hii msg aforwdiwe, Bse atleast imefanywa kwako mtz imagine huwa wanawafanyia ata wacongo such that kuna jamaa aliwaambia uko uko Japan ngoeni power window mtume separately.

Wajapan walimuuliza why akasema bandarini watazingoa so kheri wazingolee uko uko
AIBU AIBU
 
Kuna haja ya kutumia bandari za nchi jirani, maana hii tabia inakera sana
 
Mi jamaa walikomaa wakalegeza nati za propela shaft ya defender yangu pale bandari, yani ningechelewa kidogo tu kuitoa bandarini ningekuta propela shaft ya nyuma imekwenda.
 
mkuu pole sana Bandarini ni mahali pa wezi!!, niliingiza RAV4 2010 wakang'oa redio, mwaka huu pick up wakadhani kuna mzigo nyuma, ilikuwa imefunikwa wakavunja lile hard board
 
Ivi ni kweli ili Tatizo haliwezi kuwa solved?

Kwa nini wahusika bandarini wasiwe wanahusika na huo upotevu!
Haingii akilini eti mtu nasema gari imekuja haina power window au wanazani uko nje kuna vishoka wezi kama apo bandari.

Nilishakiamuliaga gari zangu zote hupitia mombasa maana apa Bandari salama si salama tena
 
Gari ikiwa imefika bila hivyo vifaa, inatakiwa isiteremshwe melini kabla ya kujaza fomu za mapungufu baina ya bandari na agent wa meli, ukiiteremsha melini kabla ya kuwajulisha agents, ambao wanatakiwa wawepo wakati magari au mizigo yoyote inateremshwa, inakuwa kosa ni lako uliyeteremsha na umeshapokea huo mzigo ukiwa salama na hapo inatakiwa bandari wakulipe.

Tanzania ni ubabaishaji na wizi wa huko Barbarian, ni kweli Mwakyembe kwa kuwa hizi bandari zipo chini yake, inatakiwa afanye kazi ya ziada.

Kinachonishangaza ni haya makundi ya kutetea haki za binaadam na hawa mawaziri vivuli, kwanini huwa hawasimamii kuelimisha raia mambo ya kufanya katika hali kama hizi. Ikiwwa Waziri husika kashindwa basi hata kivuli chake nacho kimeshindwa? na kazi yake ndio hiyo ya kusimamia mapungufu na kuyaainisha? na waziri kivuli si bungeni tu, ni kila siku.
 
Wale vijana ambao wanakaa karibu na geti watakuuzia vitu vyako ... Solution ni kushushia mizigo Mombasa. Bei nafuu zaidi, TRA unachagua (Tanga, Kilimanjaro au Musoma).. Bandari la Dar ni mateso tuu... Nimewakoma
 
Kimsingi wamejitahidi tahidi kupunguza naona mkuu bahati mbaya ilikuwa kwako tu. Jamaa yangu kaingiza Verosa bahati mbaya wao ktk ushushaji wakakwangua bumper la mbele walimlipa,waliitunza gari kwa gharama zao wakaagiza bumper lingine hadi limefika ndo ikafungwa na jamaa akakabidhiwa gari
 
Back
Top Bottom