Huu wimbo wa aladji (Kiduku) Umekaaje?

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,879
2,369
Wana JF, kuna huu wimbo wa kiduku (Aladji) sijui kama nimepatia jina lake, kwa maoni yangu hauna maadili ya kitanzania ingawa unarushwa laivu kwenye Ma TV.

Kuna siku nimekaa sitting room na watoto ukaanza kupigwa ikabidi nitokomee chumbani maana ni aibu. Hivi kwa nini baraza la sanaa lisiupige marufuku kuonyeshwa kwenye TV?
 
mbona uko poa tu ...si hata rais wako anachezaga sana hivi viduku akipata upenyo
 
Mbona hauna tatizo? Au hao watoto uliokaa nao sitting room ndio waliofanya mambo ya aibu?
 
wakawaida sana...
Unawaogopa wanao badala ya wao kukuogopa wewe?
 
Hivi wale wanaocheza mwanamke mbele anamkatikia mwanaume nyuma na mwanaume naye anakuwa kama ndo yuko chumbani anavyokatikia ile burunguti, manaona sawa tu kwa maadili yetu?
 
Wana JF, kuna huu wimbo wa kiduku (Aladji) sijui kama nimepatia jina lake, kwa maoni yangu hauna maadili ya kitanzania ingawa unarushwa laivu kwenye Ma TV.

Kuna siku nimekaa sitting room na watoto ukaanza kupigwa ikabidi nitokomee chumbani maana ni aibu. Hivi kwa nini baraza la sanaa lisiupige marufuku kuonyeshwa kwenye TV?

Sasa kutokomea chumbani nakuacha watoto wanaendele kuangalia ndo maadili gani uliwafundisha. Bora ungezima au kubadilisha channel wangejua si kitu kizuri.
 
Sahara voice upo, mambo ya kiduku eeeh!!!
Daaa na ndo watoto wanapenda kwelikwel.
 
Yesi saa!! Ktk swala la maadili, kuna mambo ya ujumla kwamba ktu hk hakika hakifai, na kuna mambo ya binafsi kadiri ya kabila na kabila. Sasa ktk wimbo wa alaji hauna maadili. Wewe uly great thinker, ukiona alaj utakubaliana na mtoa mada kuwa haufai kimaadil
 
Au wametoa remix mimi habari? maadili yangu ndio yanashida? mbona mi nauona poa jamani
 
Wala huna haja ya kuusemea kiduku tu, kuna miziki kibao hapa bongo haina maadili na bado inaendelea kuvulumishwa maredioni na ktk TV
 
uwekeni hapa basi,mie nimeenda youtube,nakutana na nyimbo za wawest tu....ni wa kiswahili au?:twitch:
 
Sasa kutokomea chumbani nakuacha watoto wanaendele kuangalia ndo maadili gani uliwafundisha. Bora ungezima au kubadilisha channel wangejua si kitu kizuri.
watoto wa siku hizi sio wa ndiyo mzee bora alijiondokea kwani wangemtaka awape sababu za kurisha za kuwazimia tv wakati wanahaki ya kuiangali vinginevyo angekuwa na kazi ya kuwaelewesha ubaya wa wimbo huo
 
Duh kazi ipo, ndo watoto wa .com hao.
 
Mi naona ni mwimbo wa kawaida tu tena naupenda sana video sijaiona na watoto wanaupenda sana
 
Back
Top Bottom