Huu umagharibi una mashiko ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,776
Kwa wenzetu wanaoitwa wamagharibi (wazungu) hii tamaduni ya mtu kutoka na ama Mke au girl friend wa rafiki yake wa karibu, ni kitu cha kawaida.
NOTE :- Kutoka huku simaanishi kufanyanae mapenzi laa!.
Kutoka huku kunahusisha kwende na mwanamke wa rafikie kunako maeneo ya burudani ambako huko watavinjari kwa kunywa, kudansi N.k.
Kinachofanyika ni mwenye mwanamke kumruhusu kwa ridhaa (kwa kua wanaminiana) yake mwenyewe mali zake zikavinjari na rafiki yake na baadae mwanamke anarudishwa! Mf. Mwanamke anaondoka na jamaa saa 12 jioni anarudishwa saa 5-6 usiku.
Kwa macho yangu nimeshaliona mara kadhaa.
Wadau hii maneno imekaa njema kweli ?
 
Hapana kwa kweli hata kama watakuwa waaminifu ule muda bado ulitakiwa uwe wa kwangu na yeye.
 
Kama wanaaminiana na mmoja anataka kwenda sehemu wakati mwenzake ana shughuli nyingine waende tu. Hata ukisema aende na mwenyewe kama ni wanaume/wanawake anataka atakutana nao huko tu.
 
Kama wanaaminiana na mmoja anataka kwenda sehemu wakati mwenzake ana shughuli nyingine waende tu. Hata ukisema aende na mwenyewe kama ni wanaume/wanawake anataka atakutana nao huko tu.

Privacy ya two difference gendar always hutoa matokeo ya hisia! Lakini mi nishaona mtu anamegewa demu wake na analetewa data hakubali kuamini.
 
Nmh, mimi siamini kama hao wazungu wanafanya hivyo kissana! Labda iwe imetokea mume kasafiri, kaenda mji mwingine ambapo kuna huyo shosti wa mkewe au GF wake!
 
Nmh, mimi siamini kama hao wazungu wanafanya hivyo kissana! Labda iwe imetokea mume kasafiri, kaenda mji mwingine ambapo kuna huyo shosti wa mkewe au GF wake!

Wanafanya sana mie nimeshuhudia mara chungu nzima. Wote wameoa mmoja anaenda Mikumi badala ya kwenda na mkewe anamuomba mwenzie asafiri na mke wa mwenzie na kulikuwa hakuna lalam. Thubutu umwambie Mbongo unaenda kula kuku kwa mrija sehemu sehemu hivyo umuombe uende na mkewe kama atakuelewa!!! Na urafiki ndio utafika tamati siku hiyo.

 
Hmmm hapa labda tuzungumzie ki-anecdotally tu maana mimi na kuishi kwangu kote na hao so called Wamagharibi sijawahi shuhudia hayo pasipo na tafrani.

Vivyo hivyo, nyumbani nimeshashuhudia mjomba wangu akienda baa na mke wa jirani yetu mara nyingi tu tena kwa ufahamu wa mumewe. Walikuwa wakienda baa mida ya jioni jioni mishale ya saa kumi na mbili au saa moja usiku na kurudi mishale ya saa tano tano hivi.

Nadhani kuna mengi sana ambayo tunawa-stereotype hao Wamgharibi na wao kuna mengi tu ambayo wanatu-stereotype wakati ukweli wa mambo ni kwamba haya mambo yanahusu zaidi watu binafsi na mienendo yao kuliko jamii nzima kwa ujumla wake.
 
Bongo ninamjua baba mmoja ambae ana urafiki wa karibu na mwanamke mmoja mke wa mtu mwengine.

Huyo mwanamke huenda nyumbani kwa huyo baba, na hukaribishwa na mkewe na watoto, kisha hujichimbia chemba kwa masaa wanazungumza, na hakuna longolongo.

Mama mwenye nyumba kama alikuwa na mishemishe zake hutoka na kuwaacha ndani

Kwa hiyo naamini ni mtu na mtu, sio umagharibi per say
 
Hawa Wazungu (Wadanish/Waswedish) tulikuwa ofisi moja na pale ofisini hili la kwenda short vacation na mke wa mtu mwingine lilikuwa gumzo kubwa, halafu kuna jamaa yangu pia alikuwa anafanya na wa Danish aliwahi kuniambia kwamba ofisini kwao pia hao wazungu walikuwa na kawaida kama hiyo, labda si Wazungu wote lakini baadhi yao ambao hawaoni tatizo mkewe aende kujirusha sehemu sehemu na rafikiye.
 
Sasa BAK kama lilikuwa gumzo kubwa kwenye nchi ya Magharibi uliyopo, huoni kuwa inamaanisha hilo tukio si la kawaida?
 
Sasa BAK kama lilikuwa gumzo kubwa kwenye nchi ya Magharibi uliyopo, huoni kuwa inamaanisha hilo tukio si la kawaida?

G hii niliyoandika ilitokea Bongo hao Wazungu walikuja kama MATX
 
BAK, vacation ni kitu kingine. Lakini mie binafsi naweza toka na mtu mwingine na mwenzangu halikadhalika. The difference ni kuwa not necessarily iwe a pair, but might be a group of male and female friends. I don't see it a big deal as long as we are having a smooth relationship at home.
 
G hii niliyoandika ilitokea Bongo hao Wazungu walikuja kama MATX

Aaah okay.

Mie Wazungu nawaona wana wivu vibaya, sema huwa wanajilazimisha kuwa civil tu sometime, tofauti na sie
 
G hii niliyoandika ilitokea Bongo hao Wazungu walikuja kama MATX

I bet they were a statistical anomaly!

Mimi nishawahi kuwa na landlady aliyekuwa na boyfriend ambaye ni nudist. Nilikuwa live-in tenant. Siku na sign lease agreement huyo mama akaniambia kabisa.

Siku moja nimetoka zangu kwenye mishe mishe za boksi...lahaula la kwata namkuta boyfriend wa landlady kainama na yuko na nguo zake za kuzaliwa anaweka kitu kwenye oven lol.

Ilinibidi niivunje lease. Wakati na sign nilidhani nitaweza ku handle. I was dead wrong. Hiyo tajiriba yangu ya kuishi nao haikunifanya nihitimishe kuwa Wamagharibi wote wako hivyo.

Kwa hiyo na hapa ni hivyo hivyo. Nadhani Wamagharibi wengi hawafagilii hayo mambo ya kutoka na ku get cozy na mwenza wa mtu mwingine.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom