Huu UDHAIFU tusiuchulie Kiwepesi....

Borat69

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
2,526
1,757
​Siku hizi kila kukicha tunasikia viongozi wa Jamuhuri wakiwa wanatuhumiwa kuhusika na mambo machafu yanayopotosha maadili ya tamaduni na heshima zetu Watanzania.
Mimi binafsi nafikiri umefika wakati wa kuwawajibisha hawa jamaa.
Inapofikia kiongozi kufumaniwa na KAHABA au MKE wa mtu hii nafikiri ni hatari kwa jamii yetu.
Viongozi ni kioo cha jamii...sasa hapa hawa maNINJA wanatufundisha nini wapiga KURA?

Inaonekana imekuwa Jambo la kawaida sana siku hizi kwa hawa Viongozi watu kufanya madudu hadharani,halafu wanategemea kuheshimiwa! Heshima itatoka wapi kwa matendo yenu katika Jamii!!???
Miaka ya uongozi wa Mwalimu(R.I.P) kulikuwa hakuna upuuzi kama huu. Unakutana na Mh. Waziri kwenye ukumbi wa taarabu saa nane za usiku!!! Halafu kesho yake anataka heshima..itatokea wapi!!???

Leo hii mtu anatumia neno DHAIFU mnaona mmetukanwa!!! Kwa sababu ya madudu na utovu wa Nidhamu wenu nyinyi Viongozi. Watanzania walio wengi TUMECHOKAAAAAAAA.

Imefikia wakati wa Viongozi wenye utovu wa NIDHAMU kuwajibika. Mbona zamani mwanafunzi alipokuwa mtovu wa Nidhamu shule alisimamishwa shule au kufukuzwa kabisa!!??? Iweje Leo hii hawa Viongozi wa nchi watupeleke KIHUNI hivi!!????
Kwa yoyote inayomhusu...Tafakari.
 
Back
Top Bottom