Judgement
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 10,327
- 4,779
Ninasibishe misemo hii miwili na ninachokisemea hapa.
"Tembea uyaone" na
"Hujafa hujaumbika"
Hii ni kauli iliyobeba malalamiko lukuki kutoka kwa Baba (mzazi) kwenda kwa kijana wake wa kiume :-
"Huyu mtoto nimemsomesha kwa gharama zangu , nikijinyima mambo kadha wa kadha , nikijua nawekeza kwa mwanangu.
Matarajio ni aje kunilea pale mie nitakapofikia kuchoka.
Umefika wakati sasa nimechoka nahitaji nipate mafao yalionifanya niwekeze kwake hali imekua kinyume na matarajio.
Mwanangu ana kazi nzuri ni Boss Pale TRA , lakini sina faida nae! .
Wanaonufaika na pesa zake ni wanawake malaya na wenye ma'Bar, yeye ni pombe , pombe na yeye.
Hivi majuzi tumetoleana nae maneno , tumebishana sana akiwa kalewa ananiambia mimi sikumsomesha, bali kasomeshwa na walimu shuleni, namnukuu "kwani pesa zako ulizokua unalipa bila walimu ningesoma?" mwisho nukuu.
Wadau ubishi wa nani kamsomesha kijana baina ya Baba na Mwalimu tuusemeeje ?
Kijana ndiyo yuko sahihi au Baba?
Kwa maana ya kusema kila mmoja kati yao apaswa aishi kivyakevyake?
Nawasilisha.