Huu tunaomfanyia Dr Ulimboka ni unafiki, ujinga na upumbafu uliokithiri!

Ulimboka alisema na kutaja ndio lakini kumbuka wakati ule alikuwa na maumivu na hata ongea yake ilitia shaka kama kweli mentally yupo okey au la!

Mkuu, ushawahi sikia Dying Declaration? Kama Dr. Ulimboka angekufa, je polisi walishachukua dying declaration? Yaani piga ua polisi/usalama wa taifa/serikali walihusika kwenye hili. Wamekaa kimya tu!

Ki kawaida mtu akifikishwa mahtuti polisi kama alivyokuwa Dr. Ulimboka askari wa ngazi fulani kama sikosei sergeant na kwenda juu anatakiwa achukue statement ya huyo mahtuti in case akifa huo ndo ushahidi wa aliyemsababishia kifo
 
Solidarity poor, uko sahihi mkuu. Tunapenda majungu na kila mtu ni mbinasfi anajali la kwake. Tuwe na hasira kwenye mambo kama haya lililompata mnyonge huyu leo litakupata mnyonge wewe kesho.Upole umefanya kodi zetu watu wazichakachue kama kawa.
 
hta vyuon huwa wanafunz weng wanasubiria muhamasishaji wa mapambano ktk kudai hak yao wote!

So ishu hapa ni nani wa kumfunga paka kengele like Lumumba, Mandela, Che Guevera n the so forth? ili twendelee mbele?

Mama Bisimba should bell the cat.
 
Ulimboka alisema na kutaja ndio lakini kumbuka wakati ule alikuwa na maumivu na hata ongea yake ilitia shaka kama kweli mentally yupo okey au la! aliporejea akiwa Airport aliahidi kuwa ataanika wazi kila kitu sasa hapo ndipo tunataka aseme akiwa na akili zake timamu ataje majina mazingira na kila kilichotokea na pia aombe utaratibu wa kisheria uanze dhidi ya watekaji wake sasa yeye kaja anajificha haongei what follows???

wewe ni mtu wa ajabu sana tena sana..katika video ile kwa dakika 19 zote na sekunde kama 37 ulimboka aliongea kwa sauti na nilimsikia neno kwa neno....unaposema ongea yake ilitia shaka wapi ilitia shaka??..na pia unaposema mentally hakuwa safi vipi aliwea kukumbuka namba za dk deo asubuhi akiwa porini??..hivi ungekuwa wewe ungeweza kukumbuka namba hata za mkeo au demu wako?..ongeeni vitu vinavyoeleweka sio maji taka haya mnayoleta humu jf.....taifa limejaa watu wazandiki, wanafiki na wapumbavu wakubwa, wachonganishi na wavivu wa kufikiri..mtu alishasema yote mkashindwa kumuunga mkono leo amerudi mnataka arudie yale yale chini ya mwavuli kwamba wakati ule alikuwa hasikiki na akili yake haikuwa sawa.!!!!!..kweli!!!

mkoje nyie watanzania?..mbona humu muliambiwa kabisa kuwa kova atataleta watu wengine ili kuilinda serikali..kweli baada ya siku mbili akamleta joshua mlundi raia wa kenya....mpo tu wala hamkusema lolote....mmelishwa ujinga nanyi mmeutafuna..hamuoni mbele wala mawazo yenu hayafunguki!!!....kijana wa watu alieza kila mtu akasikia bado gazeti (mwanahalisi) likarudia likaandika na likaenda mbali zaid ya kutaja majina na namna mawasiliano yalivokuwa..mkasoma na kubaki na nakalaya gazeti huku mkipia mitaani na kusema mwanahalisi limemtaja ramadhani ighondu.....matokeo yake limefungiwa ....na ninyi kama wananchi mkanung'unika na kusikitka lakini kama kawaida yenu hakuna lolote mlilodai juu ya taarifa ile...

ndio maana mleta thread anaposema taifa la wapumbavu ni kweli....hata huko malawi mmepeleka watu wasiojua lolote , mkutano wa siku tano lakini siku ya tatu watanznaia hawana hoja na wala hawana cha kuongea mkutanoni.wamebaki kubishi tu wakisema mpka unapita katikati ya ziwa na tanznaia inamili asilimi 50 ya ziwa!!! ..taifa lina watu wa ajabu sana
 
Sisi yakimpata mabaya mwingine tunataka ajililie mwenyewe, ....Yakitupata sisi tunataka wengine watuhurumie!... Je, huyu ULIMBOKA akitueleza lolote la ziada kama tunavyomdai na kumlaumu,.. Tuafanya lipi la ziada?............
 
'Mimi na Mwenyezimungu pekee ndio tunaojua ukweli wa kutekwa kwangu'-Dkt Ulimboka. Haya maneno kayasema mchana kweupe siku aliporejea toka Matibabuni Afrika ya Kusini sasa tusaidieni nyinyi mnaojifanya mnajua ukweli je ndo Mungu wa Ulimboka alosema anaujua ukweli?
mimi nilimpokea Ulimboka,hakusema hvyo
 
SAWA. Lakini kwanini Dr Ulimboka akae kimya mpaka leo?? Hata kama mtu unataka kumtetea utaanzia wapi..?? Haya mambo ya kimbea mnayosema, yanasababishwa na yeye mwenyewe kukaa kimya?? Afunguke, asipoteze ujasiri. Kitu kingine kinachofanya waTZ kuwa hivi ni namna ya Utawala na Upatikanaji wa Haki nchini, my be katiba mpya itatubadirishia mifumo mingi.

Inawezekana Ulimboka alitegemea kupata support kubwa alivyorudi, lakini labda amekuta mazingira mengine kabisa. Inawezekana kabisa hana wakumuamini kwani, madaktari wenzie wamesharudi kazini. Naamini kabisa maneno aliyosema wakati akiwa mahututi ni ya kweli; nahisi aliyatoa yote akitegemea anaweza asipone. It is also true; mtu huwa unasema ukweli at your weakest point. Sasa amerudi mzima; labda ameshapewa briefing ya mambo yalivyokuwa alipokuwa hayupo; na sasa amekuwa na question mark ya watu/watanzania waliokuwa wanampa support.

Ni ngumu sana kwa yeye kupigana kama Ulimboka kwasasa kwani; atahitaji kujiweka sawa kiuchumi kwaajili yakuweka Lawyer, ulinzi kwake na familia yake, kutunza/kulisha familia yake etc. Na kama hana kazi kwasasa ni ngumu sana kusimama imara. Ninachoona kwasasa asikubali kutumika kisiasa, kuweka alliance na enemy, au kutoa habari kwaajili ya kuuza magazeti. Watu wakimbana na maswali awaulize- ile information ya kwanza wameifanyia kazi?? Anachotakiwa kusema ni kwamba; hana information tofauti za kile alichozungumza mwanzo. Sioni kwanini tunataka aongee tena ili iweje?

Kama walivyosema wengine, ile information ya kwanza tumeifanyia nini? Tunataka kujua zaidi ili iweje?

 
Hapa ndipo unajua mtanzania ni nani ,kila mmoja analaumu watanzania na kusema naunga mkono hoja
100%,bunge limetuharibu!sasa sijui anelaumiwa hajachukua hatua ni nani.Tuache unafiki na tunyamaze.Na wewe Ulimboka
nyamaza,aliyekuwa na uwezo wa kuthubutu ni Kubenea peke yake nae kanyamazishwa kwa nguvu,so
tufanye filamu ya Ulimboka imesha na sterling hajafa.

Nafikiri kwakuwa wengi wanaunga mkono hoja haimaanishi kulaumu. Inawezekana wengi tunakubaliana na mtoa mada lakini swali ambalo wengi hatujaweza kuja na jibu ni hili; Sasa haya yote yametokea tufanye nini? Nini sasa kifanyike na kwa vipi?
 
Sio sawa kuwalaumu watanzania wote kwa ishu ya Ulimboka, kwani unafaahamu kilichompa kigugumizi kuwataja walio mdhuru baada ya kurudi kwenye matibabu?
 
Nina imani Dr. SU aliko anajiandaa vyema, hataki kukurupuka. Siku ya siku ikifika mtaniamini. Anaandaa kitu cha uhakika. Kumbuka alisema ataongea baada ya siku arobaini tangu alipotua. Alikuwa na maana yake, tumsubiri, tusikate tamaa. Hawezi kunymazia unyama ule,kama vile mimi ambavyo siwezi kabisa kuukubali hata kwa tone la maji.
 
Hv, kwani LHRC au wanasheria wengne hawawezi kufile Private prosecution dhidi ya yule bwana aliyetajwa na Mwanahalisi kwa kutumia ushahidi uliopo, na wengne waliokwisha bainishwa na Dr Uli, ikizingatiwa shahidi mkuu yupo na anawafaham?
 
JAMANI TANZANIA NI ZAIDI TUIJUAVYO. KUNA WANASIASA WAWILI WALIITISHA PRESS CONFERENCE KUELEZA SIRI WAKAISHIA KUBWABWAJA TU BILA KUSEMA. HAO NI PAMOJA NA A. L. MREMA KUHUSU GOLD NA FAMILY YA MWINYI AIRPORT NA LATE O.S. KAMBONA. SEMBUSE DR. ULI, Ova.
 
baluhya M.

unaonaje wewe ukawa mtu wa kwanza kupigiwa mfano uende pale makao makuu ya police ukamtafute kova ukiwa na waandishi wa habari ueleze haya unayoeleza hapa JF ili wengine tufuate
 
Last edited by a moderator:
Kaka umenena! Wanaotaka Uli aongee wengi wao ni wanafiki na Watu wenye nia mbaya, tumezoea krona mtu anafanya hayo wanayoyapenda wao, daktari atulie ajipange sababu vita yake ni kubwa sana na yeye pekee ndo anaoweza......tusianze kumpa mbinu za kumpoteza.... I HAVE FAITH IN ULIMBOKA AND WHAT HE IS DOING
 
NASHAURI WALAU KWA HILI LA ULIMBOKA TUONEHENI UMOJA WETU. WANAHABARI, WANAHARAKATI, MADAKTARI, WANANCHI WOTE, VYAMA VYA SIASA( NA HAPA NAOMBA UPINZANI WOTE WAZUNGUMZE KAULI MOJA TUISHINIKIZE SERIKALI TUPATE UHALISIA WA JAMBO HILI. LAZIMA TUITIE SERIKALI MSHIKEMSHIKE MPAKA WAKUBALI PAWEPO NA TUME HURU KUSAIDIA KUJUA NI NI KILITOKEA.

USIKUBALI LIPITE HIVI HIVI. hEBU TULISHIKIENI BANGO WALAU HILI MOJA. MTOA MADA AMENIGUSA SANA SANA MPAKA NIKATOKWA MACHOZI KWA HASIRA ZA UJINGA NA WOGA WETU WATANZANIA. tUACHE KUMWEKA ULIMBOKA KWENYE PRESHA ISIYOKUWA NA SABABU. AKIWA NA LA ZIADA ATASEMA TU.

TUONESHE KWAMBA TUPO NAYE KWA VITENDO ILI APATE NGUVU YA KUFICHUA AMBAYO ANAYAKUMBUKA. SIO KUMSUKUMIA YEYE MZIGO WOTE HUKU WENGINE TUKICHEKELEA NYUMA YA KEYBOARDS. TUFANYE KITU KUKOMESHA HII TABIA ONCE AND FOR ALL.
 
Back
Top Bottom