Huu tunaomfanyia Dr Ulimboka ni unafiki, ujinga na upumbafu uliokithiri!

baluhya M.

Member
Apr 22, 2011
33
79
Tumekuwa nchi ya kijinga sana, nchi ya kinafiki sana, nchi ya watu wasiothaminiana, nchi ya ambayo Raia wake wanafanikiwa kwa kusema uongo, nchi ambayo raia wake wanaosema ukweli wanakwamishwa katka nyanja zote za maisha, nilikuwa na naendelea kuamini kwamba Dr. Ulimboka steven aliyetekwa,kuteswa na kutupwa katika msitu wa pande alianika taarifa zote za msingi kuhusu kutekwa kwake kabla ya kwendaSouth africa kutibiwa, alifanya mahojiano ambayo yalirekodiwa na yako katka mtandao wa U-tube, amesema kuanzia nani aliyempigia simu,amesema aliyempigia simu anafanya kazi wapi, ameeleza vizuri jinsi alivyotekwa na kuteswa na watu ambao yeye aliwaita kuwa wako trained,[ni kutokana alivyowaona yeye], alieleza jinsi alivyopelekwa kwenye jumba ambalo pamoja na yeye [ulimboka] kupiga kelele hakuna mtu aliyejitokeza kumsaidia. Gazeti la Mwanahalisi lilikuja na namba na majina ya watu waliofanya mawasiliano na Doctor Ulimboka kwa mara ya mwisho, lenyewe limeishia kufungiwa tu!

Lakini leo kila mtu anahoji ukimya wa Dr. Ulimboka,mfano wandishi/wananchi/ wanaharakati/wanasiasa/ n.k wanahoji kwa nini Ulimboka hawataji waliomteka, wengne wanaenda mbali na kusema Ulimboka kanyamazishwa na watu wanaowaita vigogo n.k, huu ni upumbafu, unafiki, unaweza kuongeza majina mengne yanayomanisha tabia za kipumbafu na kinafiki, jiulize, je sisi kama taifa na kama wananchi wanyonge tumezifanyia kazi kwa kiwango gani taarifa ambazo tayari Doctor katoa?? Je tumedai kwa kiasi gani kukamatwa kwa watu/ mtu aliyempigia simu doctor mara mwisho kabla ya kutekwa? Tumedai kwa kiasi gani serikali kuruhusu tume huru?? Kama tumeshndwa kama taifa kuinuka na kutaka wahusika wote wakamatwe na matokeo yake watu wameishia kukamata Joshua mlundi tu,tunapata wapi ujasiri wa kuendelea kumshinikiza Doctor ulimboka atoke hadharani na kuwataja wahusika?

Kumbuka Doctor ulimboka pamoja na maumivu aliyokuwa nayo alijitahdi kuelezea scenario ya kutekwa kwake yote,lakn kwa sababu taifa letu limekuwa la wanafiki na wapumbafu tumeshndwa kufanyia kazi taarifa ambazo zipo tayari na matokeo yake tumejikita katika kumlazimisha ulimboka aache kupumzika ili aje kutoa taarifa za kutekwa kwake! Ambazo kimsingi haziwezi kuwa tofauti na zile ambazo ziko u-tube na ambazo mwanahalisi liliandika.

Huu tunaomfanyia Dr Ulimboka steven ni unafiki,ujinga na upumbafu uliokisiri. Na kama taifa tumeonesha kwa kiwango kisichotia shaka kwamba hatuna uwezo wa kurisk maisha yetu kwa kiwango chochote kwa ajili ya kuteteana wanyonge kwa wanyonge. Mwisho kabisa nataka ieleweke kwamba mtu yeyote awe wa serikalin, CCM,CDM, CUF, TLP,MAGAZETINI, NGOs ,KANISANI, TELEVISION akisimama na kusema anahitaji taarifa zaidi kutoka kwa Doctor Ulimboka juu ya kutekwa kwake mtu huyo apelekwe Milembe mara moja.

 
Tanzania ushabiki mwingi! Huwa wanapenda vitu vipya kila siku na kutupa vya jana! Watanzania wanapenda 'umbea' na 'majungu' hapo humtoi! Ila kushinikuza, kufikiri kwa nguvu na kuamua kwa busara wengi wao hawajui. Binafsi yangu naungana nawe kwa 100%.
 
Mimi nawalaumu akina mama Bisimba. Ofisi yake LHRC ilitoa tamko kali ambalo nikiwa karibu na computer nitaweka hapa. Tamko linaloitaka serikali ishughulikie suala hilo na hata walipendekeza utaratibu ambao ufuatwe

Mama Bisimba yupo wapi? Pia napenda kusema kwamba mama Bisimba na serikali wote wajue kwamba hili suala la Dr. Ulimboka siyo suala kati ya hizo mbili tu na sisi wananchi ni wadau hapo ukizingatia kwamba serikali ambayo inaendeshwa kwa kodi zetu ndo inatumiwa kufanya unyama huu.
 
misingi ya upole,inyenyekevu,utii wa viongozi na wala sio sheria tulivyoachiwa na baba wa taifa mwlm jk vimetufanya tuwe wanafiki sana.pia kaulu mbiu ya kikwete kuhusu kulinda amani ya kwenye makaratasi inatutia uoga wa ajabu.
ukihoji mambo ya msingi kuhusu mstakabali wa taifa unaonekana mvunjifu wa amani.mbaya zaidi umaskini tunaoubeba kila kukicha unamfanya mtanzania wa kawaida kuona kuwa kuhoji mambo ya msingi ni kupoteza bora akae chini apange dili zisizo halal cha maana apate pesa ya kula leo kesho atajua ikifika.
lakini pamoja na hayo,tutaishi hivi mpa lini????????????
 
Mkuu,

Nakubaliana na wewe vizuri mno mgomo tu wa madaktari na walimu,kuzama kwa meli zote kwa uzembe wa serikali,mgao wa umeme mara zote mbili nchi ikawa gizani,epa,kagoda,richimond na mengine madudu mengi yaliyofanywa na serikali je wananchi wa Tanzania waliitikia vipi? Kama walipiga zogo tu bila vitendo maana yake ni mazuzu kwa kuwa mwisho wa siku waathirika ni wao ndio maana huwa na sema tatizo la msingi mkuu ni wananchi kukubali upumbafu wa serikali hali wakijua uwezo wa kuiwajibisha wanao kwa kutoka majumbani mwao nakukaa barabarani tu basi hatima ya nchi hii ipo mikononi mwa wananchi wenyewe na uwezo wanao kama hawataki lawama ya nini maana kama kiongozi hakubaliki kuna njia nyingi tu za kumtoa nasema kiongozi mbovu hawezi kuongoza wananchi wanaojitambua,werevu hasirani.
 
Tunaenda kubaya sana,hakuna mfumo wa kuteteana wanyonge kwa wanyonge,fikiria Ulimboka angekuwa mtoto wa.....................watu wangapi wangekuwa segerea ??

We acha tu sisi wa TZ ni wabinafsi mno shida ya mwenzio unaiona si yako na kwa wakubwa zaidi ni kujipendekeza ili waonekane...!
Nachukia sana tabia hii sijui tumeirithi wapi kwa kweli!
 
Tangu nijiunge jf leo nimekutana na ukweli mia kwa mia.KWELI KABISA!!! Hivi nini kipya kinatarajiwa kutoka kwa ulimboka? kitu kimoja cha ukweli kabisa ni kwamba waliohusika wanajulikana hata wakane kwa HERUFI KUBWA. WAKO PEUPEEE MWANZO MWISHO.
 
hapa pagumu sana mpaka naogopa kutia neno
ukweli upo mwisho wa siku najua wtz tutabadilika na
kufanya maamuzi
 
mkuu wewe ni highly talented.. Umenena! Bila shaka uzi huu utabadili mawazo ya wengi hasa wale walioukua wanataka tu DR. aongee ilhali alisha toa habari tena akiwa na maumivu..

Wa tz neno hli linauma ila ndo ukweli.. Tuache UPUMBAVU..
Tena vyombo vya habari ndo mkome kabisa na UPUMBAVU.

Heshma kwako baluhya M.
 
Last edited by a moderator:
Mwambieni Dr Ulimboka afunguke upya, kwa akili timamu, bila woga sasa. Alisema siku ile anapokelewa pale Airport kwamba yuko tayari kwa lolote. Anawafahamu waliomtesa. Aende mahakamani. Aende amtoe hata yule jamaa aliyekamatwa kule kwa Gwajima kwamba sie. Hatukulimaliza lile la Harison Mwakyembe, la Mwandosya na hata hili la Ulimboka hatutalimaliza sisi ambao hatukuteswa.
 
Kenyata aliwahi kumwambia nyerere kuwa anaongoza MAITI...ulichozungumza mkuu ni ukweli kabisa...sisi ni MAITI TUNAOTEMBEA
kwa binadamu mwenzio hasa katika ngazi za uongozi kukutamkia haya ni maneno mazito sana lakini yanapogundulika kuwa na ukweli yanaongeza masikitiko mara mbili!
 
Imani ya kweli ni kuamini juu ya kitendo,Watanzania wengi na siyo wote hawalijui hili na hata wakilijuwa kulitekeleza kwao ni ngumu sana.Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom