Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Hebu ndugu unayesoma habari hii fikiria vizuri hiki kitu. Banks zinafanya biashara ya kukopesha ela, na biashara hiyo inalipiwa kodi. Ina maana bank wakinipa mimi mkopo nifanye biashara, tayari biashara hiyo imeshalipiwa kodi na bank. Kwa maana hiyo sipaswi tena mimi nakadaiwe kodi nyingine kwenye ile biashara, au hata nikidaiwa, basi iwe kidogo...
Ngoja nitoe mfano kama hujaelewa;
Mr X na Mr Y wanafungua kiwanda vya kutengeneza juice kwa kutumia mtaji unaolingana. Mr X anatumia mtaji wa fedha yake mwenyewe, na Mr Y anatumia mtaji wa fedha aliyokopa bank. Mauzo ya kwenye viwanda yanasababisha faida ya sh 100,000 kwa kila kiwanda kwa mwezi. Kati ya laki moja, Mr X analipa sh 20,000 kama kodi yake TRA... Mr. Y nae analipa sh 20,000 kama kodi. Mr Y ana deni bank, hivyo pengine anatakiwa alipe sh 50,000 kila mwezi. Hivyo kwenye ile laki moja, alitoa 20,000 kulipa TRA, alafu anatoa 50,000 kurudisha bank. Kati ya hizi 50,000 elfu 20 pendine ni riba (faida ya bank). Kwenye hii faida ya bank (20,000), TRA wanachaji hapo kodi ya tsh 5,000 labda. Hii elfu kumi na tano iliyobaki kama faida ya bank, kiasi fulani (labda 10,000) kinatumika kulipa wafanyakazi na kununua vitu. Kwenye mishahara ya wafanyakazi wa bank, na vitu ambavyo bank inanunua, kuna kodi ya TRA.
Kwa maana hiyo utaona Mr X ambaye hakutumia mkopo, analipa sh 20,000 tu TRA, lakini Mr Y ambaye kachukua mkopo, analipa pengine 30,000 TRA.
Madhara yake
Inakuwa ngumu sana kwa biashara inayofanywa kwa fedha ya mkopo kuingiza faida. Kutokana na hilo inasababisha kuwepo na biashara zinazotumia mitaji haramu na pia inasababisha ugumu katika biashara na uwekezaji.
Ushauri wangu
Serikali iwe na utaratibu wa kupunguza kiasi cha kodi kwa uwekezaji unaotumia mitaji inayotokana na vyombo vya vyedha ambavyo vinalipa kodi. Kwa kuwa uwekezaji wowote ni mtaji, basi kuwepo na tofauti kati ya tozo kwa uwekezaji ambao unatumia mtaji ambao unalipiwa kodi ukifananisha na uwekezaji ambao unatumia mitaji isiyolipiwa kodi
Faida yake
Itahamasisha ujasiriamali, kwani uwezekano wa kuwa na uwekezaji wenye tija utakuwa mkubwa
Itakuza ufanisi wa taasisi za fedha kwani watu wengi watajitokeza kukopa
Itaongeza soko kwa taasisi za fedha za hapa nchini maana kama mwekezaji atatumia mtaji aliokopa nje (kwenye taasisi isilipa kodo TRA), basi atahesabiwa anatumia mtaji usiolipiwa kodi, wakati akitumia mtaji unaotokana na kukopa kwenye taasisi za ndani, kodi yake itapungua.
Tahadhari
Kutatakiwa kuwe na uwazi katika mitaji na soko la mitaji...
NB; Mawazo haya nimeyatoa tu kwa fikira zangu kwani sijasoma mambo ya uchumi wala mitaji. Naomba wenye taaluma yao wajisikie huru kunielimisha na kunikosoa...