Kabakabana
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 5,551
- 1,159
Kuna mtu kanikera kweli leo,.Kuna jamaa yake wa karibu kanipigia simu eti anafanya kazi airport na amepokea mzigo wangu kutoka kwa huyo mtu ambaye kwa sasa yuko nairobi na mzigo umetokea marekani.Sasa inabidi mzigo huo usafirishwe kutoka jk nyerere international airport unifikie hapa arusha. Huyo jamaa wa huyo mtu akaniambia inabidi nilipe dola kadhaa ili mzigo wangu usafirishwe na precision air kesho.Kiukweli hizo hela sina na nimemwambia kuwa ausafirishe tu kwenye ngorika unifikie.,hakuafiki. Basi nikatafuta alternative ya kumwambia kuwa kesho rafiki yangu aende kuangalia kama upo na atalipia itakuwa cheaper bado kakataa na kusema huo sio utaratibu wa kazi.Sasa mimi sijaelewa kuwa kwani ni lazima utumwe kwa ndege?au ni lazima ufike arusha?na kwanini huyu mtu hakuulipia unifikie bila matatizo? Yani nawaza hapa sipati jibu