huu ni utamaduni au utumwaduni ??

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Huu ni utumwaduni si utamaduni
TUNAAMBIWA na wataalamu kuwa utamaduni maana yake ni jumla ya yale anayofanya binadamu katika maisha yake. Kwa maana hiyo mambo yote aliyotengeneza binadamu kukabiliana na mazingira yake tunaweza kuita ni utamaduni.
Na kwa hali hiyo hata wanyama nao wana utamaduni wao. Na hapa nisistize kwamba mbali na wanyama wote katika mbuga kuwa na utamaduni mmoja pia kila mnyama ana utamaduni wake unaomtofautisha na wanyama wengine.
Mathalani ni utamaduni wa chui kukwea mti na kwenda kujipumzisha huko au kula nyama yake ambayo amepata katika mawindo yake ili simba asije kumdoea. Wakati huo huo si utamaduni wa simba kupanda mti.
Siku simba atakapojidai kuiga utamaduni wa chui wa kupanda mti hatafika hata katikati, atarudi au ataanguka na anaweza kuumia au la. Hivyo jaribio lake la kutaka kuiga utamaduni litakuwa limeshindwa.
Vivyo hivyo binadamu wote duniani wana utamaduni mmoja unaofanana, kwamba binadamu wote ni lazima wavau nguo ili kujitofautisha na wanyama.
Lakini pamoja na kuwa na utamaduni huo mmoja binadamu wana utamaduni tofauti ambao unawafanya wavae nguo tofauti tofauti kulingana na mazingira yao.
Mathalani mtu yeyote mweusi kutoka Afrika ana utamaduni tofauti wa kimavazi na mtu yeyote mweupe kutoka Ulaya au Marekani.
Kwa upeo wangu wa ufahamu, nchi za kiafrika zina mavazi yake ya kitaifa, Marekani sijui kama ina vazi maalumu la kitaifa. Kwa bara la Ulaya kuna nchi utamaduni wao ni kuvaa sketi eti kwa jinsi zote bila kujali mwanamke au mwanamme.
Kama ilivyo kwa baadhi ya Waafrika kutopenda kuiga utamaduni wa kimavazi kutoka Marekani au Ulaya kwa sababu wanaona utawadunisha na ndiyo ilivyo kwa baadhi ya watu weupe kutopenda kuvaa nguo za kiafrika kwa sababu wanaona utamaduni huo utawadunisha au hauwaweki katika hali fulani wanayotaka.
Mimi naona mtu mweupe nimfananishe na simba kwani baada ya kuona kuwa hawezi kuiga utamaduni wa mtu mweusi kimavazi ameamua kuachana nao. Hataki kujilazimisha tofauti na sisi waafrika pamoja na kujua wazi kuwa hatuwezi kuiga utamaduni wa wenzetu tunajilazimisha kuuiga na matokeo yake tunaangamia.
Pamoja na kwamba tunasema tunakwenda na wakati lakini tuangalie kwenda huko na wakati kusitugeuze watumwa. Kwa mfano, unaweza kukutana na kijana amevaa suruali yenye kiuno kikubwa kukiko chake.
Akitembea kila kila mara utaona akiipandisha isije kumdondoka akabaki kwenye aibu kubwa. Suruali hii wala isingemfanya mtumwa kama angevaa yenye kiuono sawa na chake.
Sasa hivi tunashuhudia anguko kubwa la utamaduni wa mtu mweusi ambaye ambaye anaona utamaduni wake kama umepitwa na wakati. Kama kijana wa sasa hajui hata chakula kikuu, vazi au kinywaji cha kabila lake kinaitwaje tunatarajia nini?
Lakini kijana huyo muulize kinywaji kinachoitwa Vodka kinatengenezwa wapi? Usipopata jibu sahihi ni bahati mbaya.
Kuna mvutano wa chinichini unaendelea kati ya ukale na usasa ambapo vijana wanaona kuwa chanzo cha kumung'onyoka kwa maadili ni matokeo ya malezi ya wazazi na wakati huo huo wazazi wanarudisha shutuma hizo kwa vijana kwa kupenda kuiga utamaduni wa kigeni. Hapa sitaki kutia neno nisije nikaonekana kuwa ninapendelea kundi fulani.
Utawasikia wazazi wakiwatupia lawama vijana kwamba wana tabia mbaya zisizoridhisha. Sasa mtu unaweza kujiuliza kwani huyo kijana amelelewa na nani mpaka awe na tabia zisizoridhisha. Hapa wazazi wamesahau methali ya Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo au Samaki mkunje angali mbichi.
Wakati mabishano yakiendelea sasa hivi tunaona kwa macho yetu utamaduni wa ajabu ukiendelea katika bara letu la Afrika na huu ni wa wanaume kufanya mapenzi na wanaume wenzao (mashoga) na kwa upande wa wanawake vivyo hivyo. Hili sijui tutasingizia wazazi au utandawazi. Sitaki kutia neno.
Zamani mtoto mdogo akipishana na mtu mzima lazima shikamoo imtoke, hata kama hawafahamiani. Lakini tofauti kabisa na siku hizo ambapo wanapishana tu utafikiri sio binadamu wamekutana.
Siku hizi shida ndiyo inamfanya mtoto kumsalimia mtu mzima. Utamsikia 'shikamoo naomba hela'. Jamani hata sisimizi wanatushinda! Ukiwachunguza sisimizi ni nadra sana wakutane wasisabahiane.
Wazazi wajue kwamba ubora wa kizazi cha kesho ni matokeo ya hatua nzuri zilizochukuliwa na kizazi cha sasa hivi na tabia za kizazi cha sasa ni matokeo ya kizazi kilichopita.
Mimi ninaamini kabisa kwamba utamaduni unabadilika kutokana na kuiga mambo mbalimbali kutoka utamaduni mwingine, lakini sitaki kuamini kwamba kuiga huko kutaufanya utamaduni huo ufe.
Waafrika tujiulize kama Wazungu wameweza kuiga mambo mazuri kutoka kwenye utamaduni wetu. Sisi tunashindwa nini kuiga mambo yanayofaa kutoka kwenye utamaduni wao?
Wazungu wanakuja kwetu Afrika na kununua vitu mbalimbali vya kitamaduni kama picha za kuchora na vinyago. Ukipata bahati ya kutembelea majumbani mwao huko Ulaya utakuta wamezibandika ukutani na zinavutia kweli kweli.
Sisi tunachoiga kutoka kwao ni kununua magazeti ya wanawake walio watupu, tunakata picha zao na kuzibandika kwenye kuta majumbani mwetu. Halafu wakati huo huo tunawalaumu vijana na watoto kutofuata maadili ya Mwafrika kana kwamba vijana na watoto ndio walioruhusu magazeti hayo yaingie nchini mwetu.
Tukirudi kidogo katika historia tunaambiwa kuwa bara letu la Afrika kabla ya kuvamiwa na wageni tulikuwa na dini zetu zilizowaunganisha watu pamoja na kuwafanya Waafrika wafanye kazi kwa pamoja kama vile kulima.
Lakini baada ya kuja kwa Wazungu na Waarabu tulizipa mgongo dini zetu na kupokea dini mpya kama za Kikristo na Kiislamu, matokeo yake ni vifo vinavyosababishwa na vurugu za kidini katika bara letu la Afrika kama vile Nigeria.
Waafrika inatupasa kufanya upembuzi makini juu ya mambo mbalimbali kuhusu utamaduni wa kigeni la sivyo tutaendelea kulalamika kumomonyoka kwa maadili mpaka mwisho wa safari.
Kwa upande mwingine ni mara nyingi tumesikia viongozi wetu wakihimiza wananchi wawe na utamaduni wa kununua bidhaa zilizozalishwa hapa hapa Tanzania kama vile nguo na vyakula ili kukuza viwanda vya ndani, soko na uchumi pia. Ni vizuri zaidi kama viongozi wetu wangeanza kwa kuonesha mfano.
Watanzania badala ya kununua maji ya matunda kutoka Afrika Kusini ambayo hatujui ni jinsi gani yalivyotengenezwa ni bora tununue machungwa yanayotoka pale Tanga tukatengeneze maji ya matunda wenyewe majumbani mwetu.
Wanaomiliki hoteli kubwa hapa nchini wapewe somo kwamba nchi hii imejaliwa kuwa na mifugo mingi katika Afrika, hivyo waache kuagiza nyama kutoka nje.
 
Mkuu
Matokeo ya uliberali hayo. Yataendelea mpaka kila mtu kwa wakati wake aoneshe nia ya kuchukia...Tusipokasirika watendelea...Mzee Mwanakijiji
 
Ahsante sana Shy,this is areal good thread,keep it up!Ambaye hata elewa ni mpumbavu,hawezi kufundishika.

Back
Top Bottom